Michango ya matibabu ya Ruge: Kuna mambo yanafikirisha kidogo...

Michango ya matibabu ya Ruge: Kuna mambo yanafikirisha kidogo...

Madimba jr

JF-Expert Member
Joined
Aug 12, 2017
Posts
1,585
Reaction score
3,182
Kuumwa tumeumbiwa binadamu,simlaumu hata kidogo na namtakia apone haraka sana.

Hoja zangu chache ni hizi ambazo zinaweza kuwa za kipuuzi kwako ila kwa mwingine ni za kufikirisha kidogo

1.Mwanzoni kuumwa kwa Ruge kulifanywa siri sana,mana yake ninkwamba familia haikuhitaji umma ufahamu chochote,je kwa nini lei umma uliofichwa leo hii uonekane wa muhimu sana hadi kuombwa msaada wa michango?

2.Ruge huyu ni mtu wote tunafahamu kwamba ni kiongozi mkubwa na ana Kampuni zaidi ya Moja zenye kumuingiziq mamilioni ya pesa kila siku je ameshindwaje kugharamia hizo gharama?

3.Wakati anaenda kwenye hiyo hospitali ni wazi kabisa alijua gharama za hiyo hospital iko juu sana aliwezaje kukubali kutibiwa hapo ilihali zipo hospitali nzuri nyingi mno duniani na gharama zake ni affordable?

4.Kwa ufahamu wangu ugonjwa wa figo unatibikia kwa urahisi sana nchini india tena kwa kubadilisha figo na kuwekewa zingine,watu kibao yltena wa kipato cha kawaida wameenda huko na kutibiwa hivi sasa wamepona tupo nao.kitaani,yeye kwa nini kashindwa kwenda kutibiwa India?

5.Kwenye mahojiano ya mdogo wake Ruge sijaona mahali akielezea status ya afya ya Ruge kwamba amepata nafuu au bado hali tete na ataendelea kukaa hospitalini hadi lini? je kuna mtu hadi sasa anafahamu hali ya kiafya ya Ruge? mahututi au amerecover?

6.Ukiachilia mchango wa Mh.Rais je kwa nini Serikali,madon wakubwa bongo kama Mo,Bakhresa,Mengi ambao wanauwezo wa kuchanga hela nyingi sana pasi watanzania wa kawaida kuhusishwa hawajaonyesha kushtushwa na taarifa za Ruge wala kuonyesha kutamani kumchangia?
 
Clouds media wanasema hadi sasa wametumia karibia milioni mia 500 kwa mujibu wa maelezo ya mdogo wake Ruge,swali kama hivyo ndivyo ina maana familia hata Ruge mwenyewe hajatoa pesa yake mfukoni....why now michango ya wananchi? Get Well Soon Ruge.
 
Mbona unateseka na mtu kusaidiwa? Gharama za matibabu ni kubwa na hata hivyo hakuwa bilionea kama unavyodhani
 
Boss anaumwa

Mambo mengine ni confidential katika taaluma ya utabibu maadili ni pamoja na kutunza siri ya mgonjwa

hujafa hujaumbika kama unaweza kutoa msaada toa kama huwezi basi piga kimya usikatishe tamaa wengine watoaji.

Najua hata familia hawafurahii kupitisha michango ila maisha ni mitihani
 
Wale wafanyakazi wa Clouds wanabidi wajihoji kama Mtu wanamuita BOSS anashindwa kujilipia matibabu yake. Je wao hali zao zikoje? Na sisi tuanze kujihoji kama watu wenye connection na jina kama Ruge wanachemsha kujilipia matibabu ina maana asilimia 80% ya wagonjwa wa figo nchini wapo kwenye time bomb. Suluhisho ni kuacha siasa na kutufuta pesa kibao.
 
Wale wafanyakazi wa Clouds wanabidi wajihoji kama Mtu wanamuita BOSS anashindwa kujilipia matibabu yake. Je wao hali zao zikoje? Na sisi tuanze kujihoji kama watu wenye connection na jina kama Ruge wanachemsha kujilipia matibabu ina maana asilimia 80% ya wagonjwa wa figo nchini wapo kwenye time bomb. Suluhisho ni kuacha siasa na kutufuta pesa kibao.
Maskini Bii21
 
Back
Top Bottom