balimar
JF-Expert Member
- Sep 18, 2015
- 7,690
- 13,578
Salaam!!
Napenda kupongeza zoezi la kuwashirikisha wadau mbalimbali katika uchangiaji wa madawati kwa wanafunzi. Hapa kwetu nimependa ingawa inauma kwamba kila mwalimu anatakiwa achangie tsh.30,000/= na wafanyakazi wengine kutoka kila idara, makanisa, misikitini, wafanyibiashara na wananchi wote kwa pamoja. Na kutoa kiwango cha madawati kutoka taasisi zote za fedha kama nyingine zimepewa hadi madawati 300.
Hili zoezi ni zuri sana likisimamiwa naona tatizo la madawati likiota mbawa hapa kwetu maana yatasambazwa mpaka shule za umma za vijijini.
Ushauri:
Kama mlivyowekeza nguvu kwenye kukusanya michango nguvu hiyo hiyo itumike kuleta madawati bora na yenye viwango na walete mrejesho kwa washika dau wote.
Hongereni wazo ni zuri viongozi wangu mbunge, mkuu wa wilaya, ded, deo na madiwani, waratibu na wengine wote mnaoshiriki kutimiza wazo hili na ndipo tunapokubaliana kuwa Elimu Bure Haipo maana hela tunalipa sasa.
Mkimaliza hilo mje na swala la mwalimu sasa hasa madaraja mapunjo na uboreshaji wa mazingira ya kufundisha na kujifunzia. Inawezekana tushirikiana.
Nawasilisha Mimi.