Michango mashuleni itolewe ufafanuzi

Michango mashuleni itolewe ufafanuzi

Mparee2

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2012
Posts
3,290
Reaction score
5,769
MIMI NAUNGA MKONO KWA ASILIMIA 100% KAULI YA MUHESHIMIWA RAIS KUWA KUSIWE NA MICHANGO KATIKA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI ZA UMMA.

Hata hivyo Rais ametoa hiyo kauli kama Management hivyo nafikiri sasa ni wakati wa wasaidizi wake (Administrators) kutolea ufafanuzi wa namna ya utekelezaji ili kuruhusu michango iliyo halali na kuzuia michango isiyotakiwa;

Kwa mtazamo wangu baadhi ya michango inayo weza kuendelea kuwepo ni;
1. Wazazi wakikubaliana wanaweza kuchangia chakula cha mchana kwa watoto wao.
2. Wazazi wataendelea kuwanunulia watoto wao Sare, Madaftari na kalamu.
3. Wazazi wataendelea kushiriki katika uimarishaji wa shule kama watakavyo kubaliana mf. ujenzi wa vyoo, madawati, nyumba za walimu nk.
 
  • Thanks
Reactions: lup
Back
Top Bottom