Michael Richard Wambura na Soka la Bongo

Chukwu emeka

JF-Expert Member
Jan 12, 2018
23,389
36,512
WAMBURA NA MPIRA!

1997, uwanja wa Uhuru ulifanyiwa ukarabati na baadaye yakafanyika mashindano maalumu kwa ajili ya kuuzindua. Kamati iliyosimamia hayo, iliongozwa na mtu mmoja aliyeitwa Michael Richard Wambura! Huo ndiyo ukawa mwanzo wa mtu huyu kuingia kwenye mfumo wa mpira wa Tanzania.

1999, mtu huyu akataka kugombea ukatibu mkuu wa FAT lakini uchaguzi ulikwama hadi 2001 ulipofanyika kwenye ukumbi wa AICC Arusha. Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi, Mudhihir Mudhihir, akamtangaza Wambura mshindi wa nafasi ya ukatibu akimuangusha Ismail Aden Rage.

2002, Wambura kama katibu mkuu, hakupeleka CAF majina ya wawakilishi wa Tanzania kwenye mashindano ya Afrika. Wawakilishi hao walikuwa Simba SC( Ligi ya Mabingwa), Mlandege(Kombe la CAF) na JKT Ruvu (Kombe la Washindi). Simba walipeleka wenyewe jina lao pamoja na udhibitisho wa ushiriki...sijui walijuaje kama FAT haikupeleka majina!

2003, kamati ya utendaji ya FAT ikamhoji Wambura kwa kosa lake...akasema alisahau hivyo asamehewe. Kamati haikuridhika na utetezi huo, ikamtoa katika nafasi yake. Hakukubali, akaenda mahakamani kupinga, mahakama ikamrudisha.

2004 akagombea urais wa TFF, akashindwa na Tenga. 2006 akateuliwa kuongoza kamati ya mpito ya Simba baada ya mwenyekiti Ayoub Chamshana na katibu mkuu Hassan Hassanoo, kuondolewa madarakani kimabavu.

Alitakiwa aandae mazingira ya kufanyika kwa uchaguzi lakini akaingia tamaa kutaka kugombea yeye mwenyewe...akakatwa kwa kosa la kwenda mahakamani 2003 akiwa FAT.

2008 akataka kugombea urais wa TFF, akakatwa kwa sababu za kimaadili baada ya kubainika kwamba alipokuwa katibu mkuu, aliipa tenda kadhaa za TFF kampuni yake.

2010, akataka kugombea urais wa Simba, akakatwa kwa kosa la kwenda mahakamani 2003. Akaenda tena mahakamani...akavuliwa uanachama!

2013 akataka kugombea umakamu wa Rais wa TFF, akakatwa kwa sababu za kimaadili...zile zile za 2008.

2014, akagombea urais wa Simba, akakatwa kwa kuwa alishavuliwa uanachama 2010. Akakata rufaa TFF, akarudishwa. Baadaye akakatwa kwa kuanza kampeni mapema.

2016 akagombea umakamu wa Rais wa TFF akashinda. 2018, akafungiwa maisha na kamati ya rufaa za maadili. 2019, FIFA imekazia hukumu ile. Atarudi?

Credit goes to Zaka Zakazi
 
2
 
It was just a matter of time......hakukuwa na namna, ilibidi aondoke tu, jamaa amekuwa sumu na kirusi sugu kwenye tasnia ya soka kwa muda mrefu Tanzania.
 
Jamaa ana bahati mbaya na soka la Tanzania nadhani ni muda wa kukaa pembeni na akajaribu kwingine hasa Siasa kama Mwakalebela.
 
WAMBURA NA MPIRA!

1997, uwanja wa Uhuru ulifanyiwa ukarabati na baadaye yakafanyika mashindano maalumu kwa ajili ya kuuzindua. Kamati iliyosimamia hayo, iliongozwa na mtu mmoja aliyeitwa Michael Richard Wambura! Huo ndiyo ukawa mwanzo wa mtu huyu kuingia kwenye mfumo wa mpira wa Tanzania.

1999, mtu huyu akataka kugombea ukatibu mkuu wa FAT lakini uchaguzi ulikwama hadi 2001 ulipofanyika kwenye ukumbi wa AICC Arusha. Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi, Mudhihir Mudhihir, akamtangaza Wambura mshindi wa nafasi ya ukatibu akimuangusha Ismail Aden Rage.

2002, Wambura kama katibu mkuu, hakupeleka CAF majina ya wawakilishi wa Tanzania kwenye mashindano ya Afrika. Wawakilishi hao walikuwa Simba SC( Ligi ya Mabingwa), Mlandege(Kombe la CAF) na JKT Ruvu (Kombe la Washindi). Simba walipeleka wenyewe jina lao pamoja na udhibitisho wa ushiriki...sijui walijuaje kama FAT haikupeleka majina!

2003, kamati ya utendaji ya FAT ikamhoji Wambura kwa kosa lake...akasema alisahau hivyo asamehewe. Kamati haikuridhika na utetezi huo, ikamtoa katika nafasi yake. Hakukubali, akaenda mahakamani kupinga, mahakama ikamrudisha.

2004 akagombea urais wa TFF, akashindwa na Tenga. 2006 akateuliwa kuongoza kamati ya mpito ya Simba baada ya mwenyekiti Ayoub Chamshana na katibu mkuu Hassan Hassanoo, kuondolewa madarakani kimabavu.

Alitakiwa aandae mazingira ya kufanyika kwa uchaguzi lakini akaingia tamaa kutaka kugombea yeye mwenyewe...akakatwa kwa kosa la kwenda mahakamani 2003 akiwa FAT.

2008 akataka kugombea urais wa TFF, akakatwa kwa sababu za kimaadili baada ya kubainika kwamba alipokuwa katibu mkuu, aliipa tenda kadhaa za TFF kampuni yake.

2010, akataka kugombea urais wa Simba, akakatwa kwa kosa la kwenda mahakamani 2003. Akaenda tena mahakamani...akavuliwa uanachama!

2013 akataka kugombea umakamu wa Rais wa TFF, akakatwa kwa sababu za kimaadili...zile zile za 2008.

2014, akagombea urais wa Simba, akakatwa kwa kuwa alishavuliwa uanachama 2010. Akakata rufaa TFF, akarudishwa. Baadaye akakatwa kwa kuanza kampeni mapema.

2016 akagombea umakamu wa Rais wa TFF akashinda. 2018, akafungiwa maisha na kamati ya rufaa za maadili. 2019, FIFA imekazia hukumu ile. Atarudi?

Credit goes to Zaka Zakazi
3
Kwa kosa hilo hakupaswa tena kurudi katika soka

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Atarudi.Ataenda mahakama ya ICC
 
Huyo jamaa atakuwa na matatizo binafsi.
Siyo mifumo ya uongozi haiwezekani kila pambano upigwe knockout na nia yake kwenye uongozi ni kufanya upigaji tu

Sent using Jamii Forums mobile app
Baada ya kupambana sana ikiwemo kuenguliwa mara kadhaa hatimaye alifanikiwa kuwa makamu rais wa Tff raia wakajua sasa atatulia maana kapata mnofu kumbe wapi leo kapigwa chini kweli tatizo ni yeye sio mfumo.
 
Back
Top Bottom