Kwa nini tunapiga miayo ? sina jibu la kitaalam; subiri utajibiwa...
Wanyama kupiga miayo ? ndio wanapiga, wewe chunguza mwenyewe ....paka, mbwa hasa pale wanapokua katika hali ya uchovu, usingizi au njaa.
Kwa nini tunapiga miayo ? sina jibu la kitaalam; subiri utajibiwa...
Wanyama kupiga miayo ? ndio wanapiga, wewe chunguza mwenyewe ....paka, mbwa hasa pale wanapokua katika hali ya uchovu, usingizi au njaa.
Yaani nilivyoisoma tu hii Thread miayo imenijia mfululizo..
Nadhani uchovu pamoja na kuwa na usingizi ni miongoni mwa sababu..
Lakini kuna mazoea ya mtu kupiga mwayo pale anapoona mwenzake amepiga, sijui huwa inakuwaje hapo....
Wataalamu hebu tupeni majibu ya kitaalamu tafwadhali....
Kupiga miayo, kunahusishwa sana na uchovu, stress, overwork, lack of stimulation, and boredom. Tafiti chache zimefanywa kuhusiana na sababu ya upigaji miayo...!
Tafiti zilizofanywa za kiadhari kwenye fizioloji, wanasema kuwa upigaji miayo kunasababishwa na upungufu wa hewa ya oksijeni kwenye damu. Kuna watafiti wengine wanalipinga ili, kwani wao wansema kuwa upigaji wa miayo kunapunguza uchukuwaji wa hewa ya oksijeni mwilini ukilinganisha na upumuwaji wa kawaida.
Wale wenye kuunga mkono nadharia ya mageuzi ya kimaumbo, Evolution Theory, wao wanasema kuwa upigaji miayo ni urithi kutoka kwa mababu zetu wa kale (ancestors), ambao walikuwa na tabia ya kukenua vinywa vyao na kuonyesha meno yao ili kuwatisha wengine, kwa ufupi hapa, wanajaribu kutufahamisha kuwa upigaji wa miayo ni urithi tu, kutoka binadamu wa kale.
Pia kuna wale wenye kuamini nadhalia ya uchovu: Hawa wanasema kuwa upigaji wa miayo kunasababishwa na uchovu au utepetevu. Ni kawaida kupiga miayo kama tunaonyesha dalili ya uchovu au usingizi, lakini nadhalia hii haielezi kwanini wanariadha wengi upiga miayo kabla ya kuanza mashindano.