Mkulungwa01
JF-Expert Member
- Jul 14, 2021
- 3,977
- 5,352
Chai sijanywa kutokana na kushangazwa na haya!
Nina miaka zaidi ya 10 ninamiliki silaha ya moto kisheria, na ninaihifadhi chumbani.
Mke wangu hafahamu hata kuhisi kwa muda wote huo.
Siyo mke wangu tu, hata watoto wangu hawafahamu kabisa.
Nilifanya haya ili kuondoa hofu ambayo inaweza kuwepo ikiwa watoto wakifahamu nina silaha ya moto, hasa ninaoishi nao.
Pia nilifanya haya kuondoa hofu kutoka kwa mke wangu, kwamba nina silaha ya moto.
Kisa cha mke aliyefikiria kum 'shoot' mumewe kwa kutumia silaha ya mumewe baada ya kukosana (hapa hapa Tanzania), kiligongelea nyundo kabisa mimi kuendelea kuificha silaha yangu.
Hivi kuna faida gani kwa kumuonesha onesha mkeo au watoto wako silaha yako ya moto?
Mimi nimetoa sababu za kuficha silaha yangu kwa miaka 10+. Je, wewe una sababu yoyote ya msingi ya kuining'iniza hiyo silaha yako kama vidole vyako au funguo yako ya gari?
Kwa nini unai expose kwa mke wako na kuwatishia watu bar?
Sifahamu faida za kuionesha onesha hasa kwa mke na watoto. Tafadhali, naomba nifahamishwe ikibidi, ili haya mawazo yangu yanayoniambia kuwa ni 'washamba' tu 'and nothing more' yatoke.
Nikajilazimishe kunywa chai sasa!
NB
Maneno ndani ya funga semi si rasmi, au ni ya kiingereza.