Miaka yangu 10 ndani ya JF

Miaka yangu 10 ndani ya JF

Tangu nijiunge Jf na mtoto wangu wa kiume wanalingana umri!
Nakumbuka nilijuunga jf 2016 kiutani utani kipindi dogo anazaliwa na changamoto mbili tatu nikaja kuombea msaada humu nikasaidika!
2024 anaingia darasa la pili

Thanks all members! Founder and all moderators
 
Hongera sana, ingawa jf siku hizi imebadilika
Mabadiliko hayana budi kutokea maana dunia haisimami inaenda mbio mbio na watu tunaongeza miaka na majukumu

Lakini pamoja na yote hayo, watu wema bado wapo na wataendelea kuwepo
 
Hello mabibi na mabwana, natumai mko vyedi kabisa.

Ikiwa imebaki masaa machache tupindue mwaka napenda kushuru kama ifuatavyo kwa jinsi platform hii ilivokua msaada mkubwa sana kwangu.

Kipekee kabisa nianze kumshukuru mwenyezi Mungu kwa wingi na fadhila zake kwangu/kwetu.

Ashukuriwe zaidi kwa wazo/ubunifu aliouweka ndani ya mwanzilishi wa platform hii Maxence Melo kwani ni mtandao umekua msaada mkubwa sana kwetu katika kuelimika, kuburudika, kupata connection mbalimbali na kubwa zaidi marafiki wema ambao wengine huenda mbali zaidi na kua familia

Nikizungumzia marafiki wema kwa upande wangu nimefaidika nao mno mno mno wana mchango mkubwa sana katika kubadilisha maisha yangu from nothing to something

Katika nyakati hizi mabaya yanaongezeka lakini marafiki wema bado wapo. Wakati najiunga jf sikua mtu mwenye mtazamo chanya kama nilivo sasa kifupi I was nothing na ukizingatia ni std7 ndo kabisaaa sikua naona mambo vile nionavo kwasasa.

Ni mara nyingi tumeona mada negative humu kua JF ni kichaka, JF sio pakuaminika, JF this, JF that n.k, lakini sio ukweli uliokamilika jamani

JF itakupatia kile unachokitaka, ukitaka mazuri itakupa mazuri inategemea tu na vile wewe unatakaje.

Wakati nimejiunga jf nilipokelewa na watu wastarabu na makini, Arusha wing, baadhi yao ni kina Preta marejesho Filipo Arusha One.... Team hii bado nawapenda sana na asanteni kwa wema wenu kwangu

JF imenipa marafiki wengi na wenye impact positive kwangu baadhi yao ni Nyani Ngabu Kambaku Kisambo Luv Nkanini.

List ni ndefu wengine spelling za I'd zenu zinanichenga mnisamehe bure ila jueni tu mmeweka alama nzuri sana maishani mwangu, na ninawaombea mema siku zote na Mungu awabariki mno.

Funzo nililolipata; usimdharau mtu wa mtandaoni hata siku moja. Yaani kwakuwa tunatumia id fake haitupi certificate kuwa tuwe huru ku treat mtu in negatively way. Huwezi jua mtu huyo ni daraja la wewe kuendea hatma yako.

Happy new year in advance.

2024 ukawe mwaka wa mafanikio, tukaongezeke kiuchumi, upendo na mshikamano.
Hongera sana milima na mabonde!
 
JF itakupatia kile unachotaka, hili ni neno la siku. Na ni la ukweli 100%

Happy new year valentina.
Kabisa my dear

Ukiwa chanya tegemea mazuri toka humu

Na ukiwa hasi ndo vile tena

Jf kuna watu wazuri sana wamoyo jamani

Kuna watu humu wamekua nami katika vipindi tofauti tofauti kila nipatapo changamoto

Wengine hatujawahi kuonana zaidi ya mawasiliano tu lakini mtu anabeba shida yako kwa moyo mmoja na kukusaidia kuvuka
 
Back
Top Bottom