Miaka miwili ya Magufuli sikuthubutu kusema neno, sababu...

Miaka miwili ya Magufuli sikuthubutu kusema neno, sababu...

Wengi wameandika baada ya mwaka mmoja na hata miwili ya utendaji wa Rais Magufuli. Sikufanya hivyo, kwasababu sikujua tunakoelekea lakini leo ninajua anakotupeleka na hata jina la kituo au mji ukipenda.

Kwanza nianze kwa kusema ni makosa makubwa kudhani kuwa kinachotokea Ikulu ni mawazo ya Magu tu, nilichokigundua mimi ni kwamba huo ni mpango wa CCM kwa kipindi cha miaka 5. Msiaminishwe hata kidogo kuwa Kinana, Mwinyi, Kikwete, Mkapa na wajumbe wa kamati kuu ya CCM hawakuwa pamoja katika kupanga yote yaliyotokea kipindi cha miaka miwili cha Magu akiwa madarakani. Na ndio maana wamekaa kimya kwa yote yanayotokea.

Kama Nape kwa hasira alivyodokeza kuwa CCM ilikuwa inakwenda shimoni, huu ni ukweli ambao wote wakubwa wa CCM walilifamu kutokana na RUSHWA NA UFISADI vitu ambavyo upinzani ilivipigia tarumbeta. Yafuatayo ndio Maamuzi ya wakubwa CCM.

1) Ni muhimu kuchagua kiongozi ambaye hatakuwa na urafiki na wana CCM, ili avunje mazoea ya kujuana. Akachaguliwa Magufuli

2) Kiongozi huyu apewe majukumu makali na atoe maamuzi makali si yenye tija kwa watanzania ila yawe na tija kwa CCM.
- ahakikishe demokrasia inatokomea, ikiwa ni pamoja na kuzuia upinzani kutoa mawazo yao na watanzania kwa jumla
-Kuzuia haki ya mamlaka ya mihimili mikuu ya nchi
-Kurubuni viongozi wa upinzani kuhamia CCM
- Kuvuruga upinzani kwa kuleta ugomvi ndani ya vyama hivyo.
3. Kuwaaminisha watanzania kuwa huwezi kupambana na RUSHWA NA UFISADI ila sharti uvunje demokrasia.

Hivyo tunakoenda si kwingine ila ni kujenga nchi ya chama kimoja kitachochukua hatamu.

Swali ni kwamba, hivi dunia na watanzania wapo tayari kwa hilo, hata kama tutafanikiwa zaidi kiuchumi?
Hii serikali yetu na rais wetu ccm kwanza nchi baadae,yaani inatia hasira basi tu
 
Pole sana, naona kelele zako za hapa jf unafikiri kwamba zinamzuia magufuli kuwa rais wa tz au zinazuia watu kuhamia ccm, yani umzuie mtu ambaye ana utajiri wa kuanzia wapiga kura, wabunge, polisi, jeshi, eti kwa sababu unaandika jf pole sanatafuteni option nyingine, ili next time ccm itoke madarakani lkn hizi kelele za kwenye keyboard hazisaidii,ni watanzania wachache sana waliyooko juu ya keyboard, hlf siyo lazima wote tulingane mawazo, ndo maana ya upinzani, bila hivyo mi na wewe tusinge kutana hapa kubadilishana mawazo mkuu, hivyo naheshimu mtazamo wako wewe pia heshimu wangu, make mi kikubwa nilichosema ni kuwa kura zingekuwa zinapigwa jf...huko nje wanao wapenda hizi habari zinazoandikwa humu wengi hawazipati, tafuteni njia ya kuwafikishia ujumbe, kma kampeni zimezuiwa.

Asante, naona umenielewa vizuri sana. Hisia za utoaji hoja zako zinajionyesha. Kikubwa ni kwamba ujumbe umefika, au mkuu mwenyewe Magu apendavyo kusema Meseji sent. Nitanukuu baadhi ya maandiko yako yanayothibitisha ukweli wa hoja zetu.

Unasema: "yani umzuie mtu ambaye ana utajiri wa kuanzia .........wabunge, polisi, jeshi, na unaendelea "kama kampeni zimezuiwa". Na hapo ndipo nilitaka ufike. Kwa hayo maneno mimi na wewe tupo pamoja kabisa katika mjadala huu. Asante kwa kunisaidia kunyambulisha na kuweka bayani hoja kuu

Kifupi umekubaliana nasi juu ya jinsi gani hii nchi inaendeshwa. Mkuu nakupa salute, we ni bonge la muelewa.
 
Hlf hpo mwishowe umesema asilimia 15, ujue kwamba hao asilimia 15 siyo kwamba wote ni wafuasi wako, unaweza ukawa na 1/3, ccm pia 1/3 na 1/3 wengine ni wale ambao hawapigi kura, ukwrli unabaki pale pale kuwa asilimia kubwa hawana habari bisha na hilo.

Nafurahi kwa uchambuzi wako. Kumbuka hizi habari za JF zinawalenga zaidi CCM, NA hao wasiopiga kura.

Pengine nikueleze wazi tu, kwa upinzani nia si tu kushinda hata kama watu 10 wamepiga kura (mfano uchaguzi wa marudio Zanzibar) bali kuhakikisha watanzania wote wenye haki ya kupiga kura wanashiriki katika zoezi hilo. Yaani suala kubwa ni ushiriki wa maendeleo yake. Kujua kuwa kinachotokea Ikulu, Lumumba au kizota kitamuathiri kila mtanzania. Wakilijua hilo washiriki watakuwa wengi.

Kwa hiyo lengo kubwa ya haya ninayoyaandika niwewe mwana CCM na asiyekuwa na chama. Kwasababu wanachadema, CUF na wapinzani wengine haya wanayajua.

Nashukuru sana kwa uchambuzi wako, kwani hao uliowataja ndio tunaowataka. Kama hapa pangekuwa ni pahala pa wanaCHADEMA AU WANAUKAWA basi wahusika wangepata kijineno siri maalum cha kuingilia hapa nawe mwana CCM usingethubutu kuona wala kusoma habari hizi. Karibuni.
 
Back
Top Bottom