Miaka miwili ya Magufuli sikuthubutu kusema neno, sababu...

Miaka miwili ya Magufuli sikuthubutu kusema neno, sababu...

Wengi wameandika baada ya mwaka mmoja na hata miwili ya utendaji wa Rais Magufuli. Sikufanya hivyo, kwasababu sikujua tunakoelekea lakini leo ninajua anakotupeleka na hata jina la kituo au mji ukipenda.

Kwanza nianze kwa kusema ni makosa makubwa kudhani kuwa kinachotokea Ikulu ni mawazo ya Magu tu, nilichokigundua mimi ni kwamba huo ni mpango wa CCM kwa kipindi cha miaka 5. Msiaminishwe hata kidogo kuwa Kinana, Mwinyi, Kikwete, Mkapa na wajumbe wa kamati kuu ya CCM hawakuwa pamoja katika kupanga yote yaliyotokea kipindi cha miaka miwili cha Magu akiwa madarakani. Na ndio maana wamekaa kimya kwa yote yanayotokea.

Kama Nape kwa hasira alivyodokeza kuwa CCM ilikuwa inakwenda shimoni, huu ni ukweli ambao wote wakubwa wa CCM walilifamu kutokana na RUSHWA NA UFISADI vitu ambavyo upinzani ilivipigia tarumbeta. Yafuatayo ndio Maamuzi ya wakubwa CCM.

1) Ni muhimu kuchagua kiongozi ambaye hatakuwa na urafiki na wana CCM, ili avunje mazoea ya kujuana. Akachaguliwa Magufuli

2) Kiongozi huyu apewe majukumu makali na atoe maamuzi makali si yenye tija kwa watanzania ila yawe na tija kwa CCM.
- ahakikishe demokrasia inatokomea, ikiwa ni pamoja na kuzuia upinzani kutoa mawazo yao na watanzania kwa jumla
-Kuzuia haki ya mamlaka ya mihimili mikuu ya nchi
-Kurubuni viongozi wa upinzani kuhamia CCM
- Kuvuruga upinzani kwa kuleta ugomvi ndani ya vyama hivyo.
3. Kuwaaminisha watanzania kuwa huwezi kupambana na RUSHWA NA UFISADI ila sharti uvunje demokrasia.

Hivyo tunakoenda si kwingine ila ni kujenga nchi ya chama kimoja kitachochukua hatamu.

Swali ni kwamba, hivi dunia na watanzania wapo tayari kwa hilo, hata kama tutafanikiwa zaidi kiuchumi?
Umesema ukweli wote ndugu nami nakuunga mkono. Nami naongezea kwa kusema kwamba nyundo ya mwisho kuwagonga wapinzani wanyamaze ni mswada utakaopelekwa bungeni siku za karibuni wa sheria ya kuwepo chama kimoja tu - CCM. Bungeni mswada huo utapitishwa kwa spidi ya roketi hakuna nguvu kubwa ya kuupinga labda minong'ono tu ya huyu na yule.Ndio maana wabunge wa upinzani wananunuliwa kwa wingi kwa bei yoyote!
 
Binafsi nipo tayari kwa chama kimoja, maana ruzuku zitakua salama kabisa
 
Wanaomsupport leo kesho watamshutumu.Tumuachie aendelee atafika mahali atakwama.

Aliyehujumu kwenye away zote mbili aliyokuwemo leo anayejiita nabii.Aliyesababisha kununuliwa kivuko kibovu leo anaitwa Mzalendo.Acha akina Trump watutukane tu
 
Kwahiyo kutumia mamilioni ya pesa za walipa kodi wakati wa Kikwete katika mchakato wa KATIBA MPYA ilikuwa ni ILANI ya CCM. Na kuutupilia mbali mpango huo wakati wa Magufuli ni mpango wa CCM katika ILANI YAO.

Kama hivyo ndivyo usemavyo, wananchi wamepata nini? Na hasara hiyo atabebeshwa nani?

Kwa hiyo CCM ni chama cha kihuni, kinacholeta ilani, na kutumia mamilioni ya pesa za wananchi huku kesho ikiwaambia wananchi kuwa mpango huo ulikuwa feki na wananchi waendelee kukiona chama cha CCM kuwa chama bora.

Aisee wa LUMUMBA mna mambo. kAMA SI CHAMA CHA KITAPELI NI NINI?
Mkuu hakuna kiwango cha fedha,kinachoweza kukithi,dhana ya demokrasia.
Kuhusu katiba mpya hilo siliongelei kwa sasa,nilichochangia mimi ni kuwa rais Magufuli anatekeleza mkataba wake wa ahadi alizotoa wakati wa kampaini.
Sikumsikia akiongelea ahadi ya katiba mpya katika akiomba kura kwa Watanzania.
Swala ni kusubili kuona,tatizo lako hata hicho alichoahidi na kukitekeleza wewe unaita maigizo,ukisoma ilani ya ccm 2015/2020 inaongelea kulifufua shirika la ndege,ndege zikiletwa zinafananishwa na bajaj kwa namna ya kejeli.
Ilani yao inazungumzia kujenga standard gauge railway line,inaanza kutekelezwa mnasema sio kipaumbele,wengianzia kilimo.
Ilani yao inazungumzia juu ya kupiga vita rushwa,ufisadi,uwajibikaji wa utumishi wa umma,vikitekelezwa mnasema toeni ushahi juu ya ufisadi na rushwa sio kufukuza watu bila ushahidi
Ilani yao inazungumzia juu ya kukuza uchumi na madini yasaidie nchi na sio wawekezaji pekee,hatua zikichukuliwa kurekebisha hali hiyo ili nchi inufaike,mnasema Tanzania itashitakiwa kimataifa kwa kuwabugudhi wawekezaji kwa mkataba uliokubaliwa na pande zote,Wawekezaji kakisema kweli kuna umuhimu wa kurekebisha ,mnasema wanashughulikia makanikia,wanaacha dhahabu.
Hivyo mkuu,kwa utaratibu mliojiwekea serikali ya ccm hakuna kitakacho fanyika mkaona ni kizuri.
 
Tulieni muone maendeleo, sasa wanatafutwa watu wa kuendana na speed yake/ wanaomwelewa anataka nini.
 
Binafsi nipo tayari kwa chama kimoja, maana ruzuku zitakua salama kabisa
Hizo ruzuku zilishakulalamikia kwamba ziko hatarini?Hicho chama kimoja unachokiomba ndio kitatafuna hizo ruzuku, na hakitatosheka kitakuambia utoe zako mfukoni ukipe.
 
Mkuu hakuna kiwango cha fedha,kinachoweza kukithi,dhana ya demokrasia.
Kuhusu katiba mpya hilo siliongelei kwa sasa,nilichochangia mimi ni kuwa rais Magufuli anatekeleza mkataba wake wa ahadi alizotoa wakati wa kampaini.
Sikumsikia akiongelea ahadi ya katiba mpya katika akiomba kura kwa Watanzania.
Swala ni kusubili kuona,tatizo lako hata hicho alichoahidi na kukitekeleza wewe unaita maigizo,ukisoma ilani ya ccm 2015/2020 inaongelea kulifufua shirika la ndege,ndege zikiletwa zinafananishwa na bajaj kwa namna ya kejeli.
Ilani yao inazungumzia kujenga standard gauge railway line,inaanza kutekelezwa mnasema sio kipaumbele,wengianzia kilimo.
Ilani yao inazungumzia juu ya kupiga vita rushwa,ufisadi,uwajibikaji wa utumishi wa umma,vikitekelezwa mnasema toeni ushahi juu ya ufisadi na rushwa sio kufukuza watu bila ushahidi
Ilani yao inazungumzia juu ya kukuza uchumi na madini yasaidie nchi na sio wawekezaji pekee,hatua zikichukuliwa kurekebisha hali hiyo ili nchi inufaike,mnasema Tanzania itashitakiwa kimataifa kwa kuwabugudhi wawekezaji kwa mkataba uliokubaliwa na pande zote,Wawekezaji kakisema kweli kuna umuhimu wa kurekebisha ,mnasema wanashughulikia makanikia,wanaacha dhahabu.
Hivyo mkuu,kwa utaratibu mliojiwekea serikali ya ccm hakuna kitakacho fanyika mkaona ni kizuri.

Nasikitika kwa vile umeshindwa kusoma between the lines.

Kwa kukusaidia ni hivi: Kwa tanzania yeyote yule anafahamu kuwa Tanzania imeongozwa na CCM toka uhuru (nikimaanisha viongozi watokanao na chama hicho hicho au dada au mama chama)

Unachotaka kutueleza ni kwamba ilani ya CCM ya mwaka 2010/2015 inapingana na ilani ya mwaka 2015/2020. Na kwa mawazo yako hivyo ndivyo nchi inavyobidi iongozwe. Kwa mfano suala la KATIBA ambalo unasema Magu hakuzungumza lolote katika kampeni yake.

Kifupi unachotueleza ni kwamba, ni RUKSA KABISA NCHI kuendeshwa KISANII SANII. Yaani Kikwete amlaumu Mkapa na Mahita kwa kukuza ujambazi naye, naye akaushughulikia mpaka ukatokomea, na Magufuli amshutumu Kikwete kwa kuruhusu mchakato wa katiba naye aumalize mpango huo na lawama nyingine kibao. Sijui Rais ajae toka CCM (KAMA WATAPATA tena nafasi ya Urais) atamlaumu Magufuli kwa kuitokomeza demokrasia na kuua uchumi wa Tanzania na vingine uvijuavyo ambavyo watanzania hawavipendi.

Usanii huu ndio unaoukubali wewe kama hawa viongozi wanatoka vyama tofauti. Hivi CCM haina dira moja?
 
Umesema ukweli wote ndugu nami nakuunga mkono. Nami naongezea kwa kusema kwamba nyundo ya mwisho kuwagonga wapinzani wanyamaze ni mswada utakaopelekwa bungeni siku za karibuni wa sheria ya kuwepo chama kimoja tu - CCM. Bungeni mswada huo utapitishwa kwa spidi ya roketi hakuna nguvu kubwa ya kuupinga labda minong'ono tu ya huyu na yule.Ndio maana wabunge wa upinzani wananunuliwa kwa wingi kwa bei yoyote!

Ni vyema kama mngemnunua kwanza Dr SHIKA.

MOJA HILI LIZINGATIE: Mara ukiwaonjesha watu/wananchi wako kitu kiitwacho Demokrasia basi kamwe hata kwa bunduki huwezi ukawarudisha nyuma. Utachoweza kufanya ni kuwacheleweshea tu muda wa kufikia lengo lao.
 
Kura zingekuwa zinapigwa hapa JF, kwa mawazo yaliyoko ccm ingetoka lkn zinapigwa huko nje na vijijini, na yote yanayoandikwa hapa huko vijijini ni weupe, ndo mchango wangu.

Mchango wako ningeuunga mkono kama viongozi wa CCM wangelala usingizi kwa kelele za hapa JF. lAKINI hapana, mpaka nilimsikia Rais Magufuli alipenda Malaika washuke ili waje kuifungia mitandao yate ya kijamii. Sijui mwenzangu ulimsikia.

Kwa taarifa yako asilimia 15 ya watanzania washiriki wazuri wa mitandao ya kijamii. Kama unaidharau hiyo idadi lakini CCM hawaidharau. Kwa maana kila mmoja kati ya watiaji amezungukwa na watu wasiopungua 10. Hii inamaanisha karibu asilimia 40 ya watanzania wanahabariwa yanayorjiri mitandaoni.

Ndio maana wanahangaika na masheria kibao huko bungeni. Na ni kwa sababu ya uoga huu ndio uliosababisha kumweka ndani na kumfungulia mashtaka muanzilishi wa JF.
 
Nini agenda ya chadema kwa sasa.?

  • Katiba mpya
  • Demokrasia
  • Haki za binadamu, kipao mbele haki ya kuishi.
  • Uchaguzi ulio huru na usawa kwa vyama vyote
  • Uhuru wa kujieleza (Mikutano, maandamano)
  • Ajira kwa vijana
  • Ukuzaji wa wafanya biashara (soma ripoti ya benki ya dunia/ukuaji uchumi Tanzania)
  • Kukuza kilimo ikiwa pamoja kukuza bei za mazao kwa wakulima(mwaka huu mkulima hoi, bei zimeshuka)
 
Kifupi, watanzania wanamanunguniko kwa tawala zote za CCM. Ni muhimu kwa CCM kama wanataka kubaki madarakani bila kuwekwa na mapolisi na wanajeshi, ni lazima watatue matatizo na kero za wananchi.

Mabavu si njia nzuri ya kubaki madarakani.

Ni aibu kwani wakati wa uchaguzi nchi nzima inakuwa kama police state.
 
Mchango wako ningeuunga mkono kama viongozi wa CCM wangelala usingizi kwa kelele za hapa JF. lAKINI hapana, mpaka nilimsikia Rais Magufuli alipenda Malaika washuke ili waje kuifungia mitandao yate ya kijamii. Sijui mwenzangu ulimsikia.

Kwa taarifa yako asilimia 15 ya watanzania washiriki wazuri wa mitandao ya kijamii. Kama unaidharau hiyo idadi lakini CCM hawaidharau. Kwa maana kila mmoja kati ya watiaji amezungukwa na watu wasiopungua 10. Hii inamaanisha karibu asilimia 40 ya watanzania wanahabariwa yanayorjiri mitandaoni.

Ndio maana wanahangaika na masheria kibao huko bungeni. Na ni kwa sababu ya uoga huu ndio uliosababisha kumweka ndani na kumfungulia mashtaka muanzilishi wa JF.
Pole sana, naona kelele zako za hapa jf unafikiri kwamba zinamzuia magufuli kuwa rais wa tz au zinazuia watu kuhamia ccm, yani umzuie mtu ambaye ana utajiri wa kuanzia wapiga kura, wabunge, polisi, jeshi, eti kwa sababu unaandika jf pole sanatafuteni option nyingine, ili next time ccm itoke madarakani lkn hizi kelele za kwenye keyboard hazisaidii,ni watanzania wachache sana waliyooko juu ya keyboard, hlf siyo lazima wote tulingane mawazo, ndo maana ya upinzani, bila hivyo mi na wewe tusinge kutana hapa kubadilishana mawazo mkuu, hivyo naheshimu mtazamo wako wewe pia heshimu wangu, make mi kikubwa nilichosema ni kuwa kura zingekuwa zinapigwa jf...huko nje wanao wapenda hizi habari zinazoandikwa humu wengi hawazipati, tafuteni njia ya kuwafikishia ujumbe, kma kampeni zimezuiwa.
 
Mchango wako ningeuunga mkono kama viongozi wa CCM wangelala usingizi kwa kelele za hapa JF. lAKINI hapana, mpaka nilimsikia Rais Magufuli alipenda Malaika washuke ili waje kuifungia mitandao yate ya kijamii. Sijui mwenzangu ulimsikia.

Kwa taarifa yako asilimia 15 ya watanzania washiriki wazuri wa mitandao ya kijamii. Kama unaidharau hiyo idadi lakini CCM hawaidharau. Kwa maana kila mmoja kati ya watiaji amezungukwa na watu wasiopungua 10. Hii inamaanisha karibu asilimia 40 ya watanzania wanahabariwa yanayorjiri mitandaoni.

Ndio maana wanahangaika na masheria kibao huko bungeni. Na ni kwa sababu ya uoga huu ndio uliosababisha kumweka ndani na kumfungulia mashtaka muanzilishi wa JF.
Hlf hpo mwishowe umesema asilimia 15, ujue kwamba hao asilimia 15 siyo kwamba wote ni wafuasi wako, unaweza ukawa na 1/3, ccm pia 1/3 na 1/3 wengine ni wale ambao hawapigi kura, ukwrli unabaki pale pale kuwa asilimia kubwa hawana habari bisha na hilo.
 
Adui wa maendeleo yetu na mchawi wa umaskini wetu ni WANACCM.

OVA.
 
Adui wa maendeleo yetu na mchawi wa umaskini wetu ni WANACCM.

OVA.
 
Back
Top Bottom