Miaka miwili ya Magufuli sikuthubutu kusema neno, sababu...

Miaka miwili ya Magufuli sikuthubutu kusema neno, sababu...

"Domokasia" inapigwa Vita maana inafanya wakubwa wanapokula wapaliwe! Watu wanataka kujihakikishia wanakula bila kupigiwa makelele halafu nyie mnaleta domokasia humu!!
 
ndani ya kipindi cha miaka miwili ni kilio toka kwenye elimu,ajira,mapambano ya rushwa nk. hakuna jipya kwa maisha ya watu. kwangu jpm karudisha maisha ya wananchi katika umasikini mkubwa.kama mkapa na jk wanaunga mkono haya dhambi hii haitawaacha salama.lengo la uongozi wowote ule uwe ni ustawi wa watu na si vinginevyo.
 
Tatizo la chadema ni too much walawala,maujinga pipa akili kisoda,ukiwa unaishi kwa kuhisi unaonewa ata aje mtu kukuambia" hapo ulipo kaa kuna nyoka" bado utamuona ni adui, wakati kaja kukuokoa,komaeni na siasa zenu za kiitikadi tuone tutafika wapi.
 
Ushauri wangu ni huu kwa CCM , hakuna mtu aliyewahi fanikiwa kwa kuzuia mtu mwingine asiongee. Kwanza unamfanya yule aliyenyamaza kujinandaa vizuri na siku akipata nafasi na akaitumia vizuri utalia.
Pili. Binadamu hata ukimfanyia vyote vizuri hata kama unakesha kufanya mazuri ikiwa hujampa nafasi ya Uhuru yote ni bure kabisa, kumbuka zipo nyumba Mme anampa mke kila kitu mwisho mwanamke anafanya ngono na muuza mkaa au mchuuzi wa mchicha au houseboy haujiulizi?

Ushauri

CCM Tanzania ya Leo sio ya miaka ya 1980s kwa kweli hata mjenge barabara za juu toka ubungo mpama mwanza siku mkiweka usawa katika siasa ndio mwisho wenu wa kutawala.
 
Mkuu umetoa maekezo mengi kana wakati mipango hiyo inafanywa wewe ulikuwepo.
Lakini kwa mujibu wa ccm,rais Magufuli abatekeleza ilani ya ccm 2015/2020 na imeainishwa kimaandishi,sasa huu upupu inaoutoa wewe upo kwenye maandishi gani?
Ni nini chanzo cha habari yako?
Kuhama kwa wanachama kutoka kimoja kwenda kingine kumeanza wakati wa utawala wa Magufuli?
Marehemu Karume alifananisha siasa sawasawa na koti,likikubana unalivua.

Kwahiyo kutumia mamilioni ya pesa za walipa kodi wakati wa Kikwete katika mchakato wa KATIBA MPYA ilikuwa ni ILANI ya CCM. Na kuutupilia mbali mpango huo wakati wa Magufuli ni mpango wa CCM katika ILANI YAO.

Kama hivyo ndivyo usemavyo, wananchi wamepata nini? Na hasara hiyo atabebeshwa nani?

Kwa hiyo CCM ni chama cha kihuni, kinacholeta ilani, na kutumia mamilioni ya pesa za wananchi huku kesho ikiwaambia wananchi kuwa mpango huo ulikuwa feki na wananchi waendelee kukiona chama cha CCM kuwa chama bora.

Aisee wa LUMUMBA mna mambo. kAMA SI CHAMA CHA KITAPELI NI NINI?
 
Tunakwenda huko ambako semokrasia na siasa za kihuni hazina nafasi, na ndio maana chadema hawatakuwepo kwakuwa makazi yao yatakuwa makaburini kwa kukumbukwa

Hivi ni chama gani gani kina siasa za kihuni zaidi ya CCM. Niambie kitu kimoja, ni nani waliahidi Katiba mpya na ni nani wamezima mpango huo. Kama si uhuni ni nini? Ni tritlioni ngapi za walipa kodi zimetumika hapo. Ukijua kuwatafuta waajiriwa hewa uwe na kumbukumbu za ahadi na ilani zako hewa unazowapa wananchi na kupoteza matrilioni ya pesa.
 
Tunakwenda huko ambako semokrasia na siasa za kihuni hazina nafasi, na ndio maana chadema hawatakuwepo kwakuwa makazi yao yatakuwa makaburini kwa kukumbukwa

Kwa taarifa yako sasa kama kuna kipindi ccm itaanguka kirahisi ni sasa kwasababu haifanyi tena siasa bali ubabe ili kibakie madarakani. Kosa kubwa wapinzani nao wanatumia nguvu kupambana na ccm. Kilichopo sasa hivi kwa kuwa ccm imeshazeeka na tabia ya vijana ambao ndio wengi na nguvu kazi ya taifa ni kuwaahidi mambo mazuri tu ya maendeleo ili wachague chama cha kileo. Ni juu ya viongozi wa upinzani kuwa na waongeaje wazuri wenye mvuto kama Zitto, John Mnyika nk kutumia platform yoyote ile kumwaga ahadi nyingi iwapo wataingia madarani. Kisha kuponda kidogo haya maigizo ya ccm ya kuongopea kwamba kuna miradi mikubwa sana ambay iko kwenye hatua za awali kama SGR na stiegler gorge ambayo hata kuanza bado. Kuongelea kiimo cha kisasa kwa kugawa matractor bure kila kijiji, kushusha bei za vifaa vya ujenzi ili kila mtu na hasa kijana ajenge nyuma bora. Kuahidi kurudisha uhusiano bora na wafanyabiashara. Ukiingia na hadithi kama hizi na vile ccm ni chama kizee lazima upate uungwaji mkono na vijana. Hakuna kijana sasa hivi anaenda kucheza miziki ya Ottu jazz (ccm) wakati kuna miziki kibao ya kizazi kipya ya akina Alikiba (Cdm) Diamond (ACT) Hapa ccm lazima wakae.
 
Hivi ni chama gani gani kina siasa za kihuni zaidi ya CCM. Niambie kitu kimoja, ni nani waliahidi Katiba mpya na ni nani wamezima mpango huo. Kama si uhuni ni nini? Ni tritlioni ngapi za walipa kodi zimetumika hapo. Ukijua kuwatafuta waajiriwa hewa uwe na kumbukumbu za ahadi na ilani zako hewa unazowapa wananchi na kupoteza matrilioni ya pesa.

Tena mkuu kuna ile iliitwa kuondoa kazini wenye vyeti fake, pale wapinzani wakiweza kutoa ufafanuzi vizuri utakuta sio vyeti fake kweli bali ni redundancy. Sasa hapo ni rahisi kuchongea kwa kusema kama kweli waliofukuzwa ilikuwa vyeti fake, basi walipaswa kuajiri wenye vyeti halisi. Na ufafanuzi zaidi ni kutaja vyombo vya ulinzi na usalama mbona hakukukaguliwa vyeti fake, na kumaliza goli kwa kisigino unamtaja na Bashite alivyolindwa. Hii inaitwa kumkaanga nguruwe na mafuta yake.
 
Tatizo la chadema ni too much walawala,maujinga pipa akili kisoda,ukiwa unaishi kwa kuhisi unaonewa ata aje mtu kukuambia" hapo ulipo kaa kuna nyoka" bado utamuona ni adui, wakati kaja kukuokoa,komaeni na siasa zenu za kiitikadi tuone tutafika wapi.

Tatizo kubwa la CCM na wanachama wake ikiwa pamoja na wakereketwa wao kudhani kuwa matatizo ya Tanzania ni CHADEMA au CUF. Hayo ni mawazo mfu.

CCM iwaangalie watanzania wenye manunguniko, waliokata tamaa namipango isiyo na tija ya CCM na waliojawa na kero zilizotokana na CCM.

Ni muhimu kwa wanaCCM kufahamu kuwa si kila aliyekatishwa tamaa na CCM ni mwana CHADEMA. Kuna ambao hawana hawana mwamko na siasa kabisa, chanzo cha malalamiko ya mtu huyu ni ugumu wa maisha yake yatokanayo na mipango mibovu ya CCM. Kundi hili haliwaamini wanasiasa wote lakini hii haimaanishi kuwa maisha yao hayajaathirika kutokana na maamuzi mabovu ya Wanasiasa hususan CCM iliyokuwa madarakani toka UHURU.

CCM ikijikita hapa itaweza kujitathimini kwa uzuri kabisa.
 
Anachoamini Pole pole ni kwamba ukishawapata viongozi toka upinzani na kuwaingiza CCM ndio unakuwa umewatatulia matatizo yao watanzania na ni ushindi mkubwa kwa CCM. Mawazo hayo yamepewa baraka na Mwenyekiti wake.

Kumpokea mwanachama mmoja toka upinzani, inakubidi ukusanye viongozi wakubwa 20 wa CCM kumpokea, huku ni kukosa kazi na kuzorotesha mawazo ya Watanzania. Kwanini msipokeane huko ofisini kwenu?
Hahahaha huwa namuonea huruma slowslow kama si yule wa katiba mpya.yaani nilivyosikia kawa wa ccm nikajua demokrasia itakua kupita ya mkwere sasa kinyume chake wanamerudi nyuma kwa speed ya ajabu kilichobakia ni kuua watu ovyo na marisasi au kuwapoteza kama anavyojitapa jerry muro.hivi wewe slowslow huna unanoliona la kumshauri mwenyekiti wako?mbona anayoyatenda mengine mnajiaibisha? au wote ni vipofu wa demokrasia?maana kipofu hawezi kumuuongoza kipofu mwenzie
 
Wengi wameandika baada ya mwaka mmoja na hata miwili ya utendaji wa Rais Magufuli. Sikufanya hivyo, kwasababu sikujua tunakoelekea lakini leo ninajua anakotupeleka na hata jina la kituo au mji ukipenda.

Kwanza nianze kwa kusema ni makosa makubwa kudhani kuwa kinachotokea Ikulu ni mawazo ya Magu tu, nilichokigundua mimi ni kwamba huo ni mpango wa CCM kwa kipindi cha miaka 5. Msiaminishwe hata kidogo kuwa Kinana, Mwinyi, Kikwete, Mkapa na wajumbe wa kamati kuu ya CCM hawakuwa pamoja katika kupanga yote yaliyotokea kipindi cha miaka miwili cha Magu akiwa madarakani. Na ndio maana wamekaa kimya kwa yote yanayotokea.

Kama Nape kwa hasira alivyodokeza kuwa CCM ilikuwa inakwenda shimoni, huu ni ukweli ambao wote wakubwa wa CCM walilifamu kutokana na RUSHWA NA UFISADI vitu ambavyo upinzani ilivipigia tarumbeta. Yafuatayo ndio Maamuzi ya wakubwa CCM.

1) Ni muhimu kuchagua kiongozi ambaye hatakuwa na urafiki na wana CCM, ili avunje mazoea ya kujuana. Akachaguliwa Magufuli

2) Kiongozi huyu apewe majukumu makali na atoe maamuzi makali si yenye tija kwa watanzania ila yawe na tija kwa CCM.
- ahakikishe demokrasia inatokomea, ikiwa ni pamoja na kuzuia upinzani kutoa mawazo yao na watanzania kwa jumla
-Kuzuia haki ya mamlaka ya mihimili mikuu ya nchi
-Kurubuni viongozi wa upinzani kuhamia CCM
- Kuvuruga upinzani kwa kuleta ugomvi ndani ya vyama hivyo.
3. Kuwaaminisha watanzania kuwa huwezi kupambana na RUSHWA NA UFISADI ila sharti uvunje demokrasia.

Hivyo tunakoenda si kwingine ila ni kujenga nchi ya chama kimoja kitachochukua hatamu.

Swali ni kwamba, hivi dunia na watanzania wapo tayari kwa hilo, hata kama tutafanikiwa zaidi kiuchumi?
Alichokiongea trump kuhusu Africa hakukosea
 
....
Kama Nape kwa hasira alivyodokeza kuwa CCM ilikuwa inakwenda shimoni, huu ni ukweli ambao wote wakubwa wa CCM walilifamu kutokana na RUSHWA NA UFISADI vitu ambavyo upinzani ilivipigia tarumbeta. Yafuatayo ndio Maamuzi ya wakubwa CCM.
....

Mimi pia nimefikiria hivyo.

CCM imekuwa mahututi ikisubiri kifo kwa muda sasa. Hali yake ilidhihilika kuwa mbaya sana kuelekea uchaguzi wa 2015.

Hii inaelezeka vizuri kwa kuangalia nguvu (mabavu ya dola, udanganyifu na fedha) zilizotumika na viongozi wa chama hicho, na zinazoendelea kutumika ku-uminya upinzani na sauti yoyote ile inayoenyesha kuwa CCM na viongozi wake;

1. wameharibu nchi, na wameshindwa kutatatua matatizo ya msingi ya wananchi.
2. wamehishiwa mbinu za kurekebisha na. 1 na hivyo hawafai kushika dola.

Njia pekee ya CCM mahututi kuweza kubaki hai ni kwa kuwekewa mashine za kusukuma siku kwa;

- kuua kabisa chama mbadala chochote,
- kufuta kabisa sauti ya upinzani kutoka katika vyama vya siasa au wananchi wa kawaida,
- kuhakikisha sauti inayosikika ni ile ya Mema tu ya CCM na uongozi wake, hata kama hayana ukweli au mantiki, kupitia radio, luninga, mitandao na magazeti.

Uongozi wa CCM unaoneka kushindwa kutambua kuwa CCM ni mahututi kwa kuwa IMEPITWA NA WAKATI. Haiendani kabisa na nyakati tulizonazo;

1. Inategemea sana mabavu na udanganyifu na sio nguvu ya hoja, uwazi na ukweli, Hivyo - kwa mfano, viongozi wake hawawajibiki na hawahitaji kuwa na mantiki/logic katima maamuzi au matamko yao.

2. Inategemea sana "umbumbumbu" wa wananchi ili kuendelea kushika dola, lakini sasa wananchi wanazidi kuamka na hii inawatisha sana,

3. Haina jinsi ya kupata masuluhisho ya matatizo ya msingi na ziada ya wananchi - piga ua, CCM haina rasimali watu wenye uwezo huu, na mfumo wake wa uendeshaji unategemea sana uongozi wa juu wa chama kuwa na uwezo wa mkubwa kiakili (genious like) ili kufanikiwa. Watasubiri sana kumpata wa namna hii.

4. Haina rasimili watu wa kuifanya iwe ya kisasa (kuondokana na 1, 2 na 3) na haina nia, mipango/utaratibu wa kuipata rasimali hiyo.

- etc.

Kifupi kifo cha CCM hakiepukiki, ni swala la muda tu.
 
Ushauri wangu ni huu kwa CCM , hakuna mtu aliyewahi fanikiwa kwa kuzuia mtu mwingine asiongee. Kwanza unamfanya yule aliyenyamaza kujinandaa vizuri na siku akipata nafasi na akaitumia vizuri utalia.
Pili. Binadamu hata ukimfanyia vyote vizuri hata kama unakesha kufanya mazuri ikiwa hujampa nafasi ya Uhuru yote ni bure kabisa, kumbuka zipo nyumba Mme anampa mke kila kitu mwisho mwanamke anafanya ngono na muuza mkaa au mchuuzi wa mchicha au houseboy haujiulizi?

Ushauri

CCM Tanzania ya Leo sio ya miaka ya 1980s kwa kweli hata mjenge barabara za juu toka ubungo mpama mwanza siku mkiweka usawa katika siasa ndio mwisho wenu wa kutawala.

Sidhani kama watakusikiliza. CCM imepitwa na wakati.
 
Kwa taarifa yako sasa kama kuna kipindi ccm itaanguka kirahisi ni sasa kwasababu haifanyi tena siasa bali ubabe ili kibakie madarakani. Kosa kubwa wapinzani nao wanatumia nguvu kupambana na ccm. Kilichopo sasa hivi kwa kuwa ccm imeshazeeka na tabia ya vijana ambao ndio wengi na nguvu kazi ya taifa ni kuwaahidi mambo mazuri tu ya maendeleo ili wachague chama cha kileo. Ni juu ya viongozi wa upinzani kuwa na waongeaje wazuri wenye mvuto kama Zitto, John Mnyika nk kutumia platform yoyote ile kumwaga ahadi nyingi iwapo wataingia madarani. Kisha kuponda kidogo haya maigizo ya ccm ya kuongopea kwamba kuna miradi mikubwa sana ambay iko kwenye hatua za awali kama SGR na stiegler gorge ambayo hata kuanza bado. Kuongelea kiimo cha kisasa kwa kugawa matractor bure kila kijiji, kushusha bei za vifaa vya ujenzi ili kila mtu na hasa kijana ajenge nyuma bora. Kuahidi kurudisha uhusiano bora na wafanyabiashara. Ukiingia na hadithi kama hizi na vile ccm ni chama kizee lazima upate uungwaji mkono na vijana. Hakuna kijana sasa hivi anaenda kucheza miziki ya Ottu jazz (ccm) wakati kuna miziki kibao ya kizazi kipya ya akina Alikiba (Cdm) Diamond (ACT) Hapa ccm lazima wakae.

Haswa. CCM imepitwa na wakati na muda wake wa kifo umefika.
 
Wamesahau kaabisa kumaliza matatizo ya wananchi huku wamebaki kuweka mikakati ya kulinda ugali wao tu, Kujisifia for nothing, kuziba midomo woote wanaoweza kutamka chochote kuihusu serikali, kuptz wat. nk sera ambazo in deed hazina mashiko kwa kizazi hiki. Walah hawa jamaa kifo chao kitakuwa kama cha Mende [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kura zingekuwa zinapigwa hapa JF, kwa mawazo yaliyoko ccm ingetoka lkn zinapigwa huko nje na vijijini, na yote yanayoandikwa hapa huko vijijini ni weupe, ndo mchango wangu.
 
Back
Top Bottom