GAZETI
JF-Expert Member
- Feb 24, 2011
- 5,281
- 6,703
Nimeshtuka sana wakuu na pia nimekosa raha, kwa sababu sina kabisa
mambo ya kishirikina.
Ni miaka mingi sasa imepita toka nimchumbie yule binti, si hivyo tu nilimlipia
ada ya chuo baada ya wazazi wake kushindwa, tena nilijibana kwelikweli kwani
nilitegemea atakuwa mama wa watoto wangu.
Tatizo lilikuja kujitokeza alipopata kazi, kuna mwarabu koko aliingilia kati uhusiano wetu
na kumnunulia gari la kutembelea. Kwa kifupi mimi nikafutwa kwenye himaya yake.
Nilipoulizia inakuwaje? Nikaambiwa nipige hesabu gharama zangu nirudishiwe,
wakuu sikudai chochote mpaka hii leo!
Juzi nimepigiwa simu na mdogo wake akiniomba kama kuna kitu nimefanya basi
nimsamehe dada yake kwani anateseka sana. Nilijaribu sana kumuuliza kimetokea nini
hakunijibu ameishia kulia tu!
Jana baada ya kufanya uchunguzi wa kina ndipo nikagundua kuwa yule binti kwa sasa
haoni na amepofuka kabisa macho yake, si hivyo tu ndoa yake na yule mwarabu imevunjika
baada ya tatizo hilo. Kinachonikera ni kuwa ndugu wote wanaamini kuwa mimi ndie
niliyemroga.
Sasa Toka mwaka 2006 mpaka leo mbona muda mrefu umepita? Mimi nilishamsahau
huyu binti kwa alichonifanyia na kwa sasa nimeoa. INANIUMA SANA WADAU.