Miaka inaenda simuoni ninaempenda

Miaka inaenda simuoni ninaempenda

jiwekuu770

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2015
Posts
2,246
Reaction score
1,646
Oyooooo,

Mimi ni mvulana miaka 29 najishughulisha na kazi za hapa na pale zinazonipa kipato. Bila shaka unajua kupenda ni nini? Nimekua nikiona watu wakio tu kwa sababu ya umri kwenda, wengine wameoa alafu wanakuja baadae wanampenda mtu mwingne kitu ambacho sitaki kitokee kwangu.

Nimeshakua na wapenzi kadhaa lakini hamna ambae nishampenda nakua nao tu ili kunikidhia haja tena wengine ni '‘wife material'' kweli kweli lakini nakua sijawapenda nawaacha. Nashindwa kuelewa yale mapenzi niliyokua nayafikiria wakati nikikua au yale ninayoyaona kwenye movie yapo kweli au vipi maana mimi sikutani hata wakunishika akili kidogo tu simuoni.

Naombeni ushauri kwenu
 
Wewe umasubiri mpaka uone mapenzi ya movie?
 
jiwekuu770

Usihofu Muda unified kill kits litajipambanua.
 
Last edited by a moderator:
Endelea kuchagua mwisho upate Koroma.
 
Acha kuangalia tamthilia za kifilipino kijana zina-script zile.

Anyway kama humuoni wa kumpenda,jipende mwenyewe tu.
 
Vipi na hao mademu zako wote uliowahi kua nao walikua wanaridhika na ww. Au unamatatizo flani ya ndani ww
 
Oyooooo,

Mimi ni mvulana miaka 29najishughulisha na kazi za hapa na pale zinazonipa kipato. Bila shaka unajua kupenda ni nini? Nimekua nikiona watu wakio tu kwa sababu ya umri kwenda, wengine wameoa alafu wanakuja baadae wanampenda mtu mwingne kitu ambacho sitaki kitokee kwangu.

Nimeshakua na wapenzi kadhaa lakini hamna ambae nishampenda nakua nao tu ili kunikidhia haja tena wengine ni ‘‘wife material’’ kweli kweli lakini nakua sijawapenda nawaacha. Nashindwa kuelewa yale mapenzi niliyokua nayafikiria wakati nikikua au yale ninayoyaona kwenye movie yapo kweli au vipi maana mimi sikutani hata wakunishika akili kidogo tu simuoni.

Naombeni ushauri kwenu

Miaka 29 unajiita mvulana.? Bila shaka hujitambui wewe.!
 
Mkuu inaonyesha unachagua sana hiyo ndio shida, inabidi umkubali mmoja then ufanye maamuzi. Lakini pia wakati mwingine usikilize moyo wako, maana unaweza sema ngoja nioe huyu kwa ajili umri unakwenda ukajikuta umefanikiwa kudumu nae siku ya HoneyMoon tu.
 
jiwekuu770

Kwanza sinauhakika kama wanaume wanakitu "Kupenda" wanaume hutamani hutaka, wanawake waliowengi ndiyo wanahicho kitu "kupenda" na ni rahisi sana kumpenda mwanampe kwa moyo wote, wanaume sina neno zuri la kueleza namna wanavyomchukulia mwanamke ila hicho kinachoitwa kupendwa ni kutamani na husukumwa na kutamani kufanya tendo la ndoa,

ndiyo maana kwa wanawake watakubaliana na mimi kuwa wakitoka na mwanamme baada ya kumaliza tendo la ndoa kwa kawaida hakuna majadiliano, kama wapo nyumba ya wageni mwanaume atajitahidi waondoke huku bibie akitaka waongee mambo ya maisha, ninafikiri wewe hujapata mwanamke mrembo, mzuri n.k ila kama unasubiri hilo utangoja sana
 
Last edited by a moderator:
Atakuja tuu,mie mpaka leo bado sijampata wa kunipenda ila namuomba sana Mungu aniletee wakunifuta machozi.sasa basi kama unaona mtu anakupenda basi na wewe muonyeshe ushirikiano kuliko kumpotezea muda mtu.

inaelekea unachagua sana as if ur a perfect man.ila nahisi muda ukifika atakuja tu.
 
atakuja tuu,mie mpaka leo bado sijampata wa kunipenda ila namuomba sana Mungu aniletee wakunifuta machozi.sasa basi kama unaona mtu anakupenda basi na wewe muonyeshe ushirikiano kuliko kumpotezea muda mtu.

inaelekea unachagua sana as if ur a perfect man.ila nahisi muda ukifika atakuja tu.

Wewe hujapata vipi wakati Mimi nipo jamani?????
Au sina sifa....???
 
Wewe hujapata vipi wakati Mimi nipo jamani?????
Au sina sifa....???

mamaeeee, umepotelea wapi baby,sidhani kama humu kuna mtu anaweza akakupenda milele,yani sijaona mwanaume mwenye mapenzi ya dhati.
 
Back
Top Bottom