Miaka 7 bila ndoa

Miaka 7 bila ndoa

Sigara Kali

JF-Expert Member
Joined
May 28, 2017
Posts
3,708
Reaction score
8,746
Wakuu salaam

R.I.P Godzilla

Daaaah sometimes mwenzenu nakaa nawaza sana ,yaani umaskini ni mbaya sana kwa kweli

Mi ni baba wa watoto wawili,mmoja wa kike mkubwa na mwingine wa kiume miezi kadhaa

Kitu kinachonifanya sometimes nikae na mawazo na kujiona sitendi haki kwa mwenzangu ni hii hali ya kukaa nae miaka mingi takribani 7 bila ndoa,barua ya posa wala kutambulishana rasmi

Huyu mama watoto nlikutana nae enzi nipo Chuo ,ila yeye alishamaliza certificate so akihangaika kutafuta kazi ,basi tukaanza kudate hadi alipopata kibarua mkoani DSM Maisha yakaendelea na mwisho nikampa mimba,tulipanga iwe hivyo.

Ikabidi niwape taarifa kwao kwamba nimempa mimba binti yao,hapo wazazi wake hawanijui,mamake kanimind kinyama nikamwambia kama vipi mkae basi na binti yenu na mimba yake,ila baadae babake akaingilia kati mambo yakaa sawa

Nikaenda kwa mamake mdogo kukamilisha baadhi ya taratibu za kwao nikaanza kukaa nae rasmi ghetto kazi ikamshinda kutokana na mimba kuendelea kukua,nikamfungulia biashara kwa hela yangu ya boom Maisha yakaendelea vizuri

Nimekaa nae ghetto akaitwa interview flani na mimba yake ya miezi 8 nikamsafirisha hadi DSM akapiga interview akarudi ,ilipofika miezi 9 akajifungua mtoto wa kike,tulifurahi sana nikaendelea kukaa nae ghetto mamake Mdogo akawa anakuja anamkanda na kumpa huduma zingine Maisha yakaendelea

Baada ya miezi 3 tangu mwanangu azaliwe mama mtoto akapata ajira rasmi kupitia ile interview aliyoifanya tena kazi yenye mshahara mnono

Nikampa hela akaenda kuripoti kazini mkoa wa mbali na nilipo,wakati huo nimeshamaliza Chuo na ramani zimeanza kugoma

Baada ya muda nikamtembelea mama mtoto na likizo moja nikaenda kwao nikaonana na wazazi na ndugu zake wengine wakanitambua kama ndio mimi nimmemzalisha mwanao,basi nikaendelea kupewa heshima zote

Maisha yakaendelea hadi tumepata mtoto wa pili,huyu binti nyumbani kwa ndugu zangu hawajawahi kumwona physically zaidi ya kwenye picha na kuzungumza nao kwenye simu na anapewa heshima zote na ndugu zangu

Kitu ambacho kinaniwazisha ni hali yangu ya kiuchumi hadi nimeshindwa kumpeleka home manake ni distance inatakiwa nijipange kweli kweli na nikichek mbele sioni dalili ya kuwa stable kichumi kwa wakati huu,naishi kwa kuunga unga tu natuma matumizi kidogo kidogo ya watoto

Sasa nawaza miaka 7 yote kwao sijapeleka mahari,wala barua ya posa, home kwa ndugu zangu sijampeleka manake wazazi wangu walishadead kitambo sana

Nakosaga raha sana kitendo cha kukosa hela ya mahari ya kimlipia huyu binti ingawa kwao sijapewa kiwango cha kulipa kwa maana hata barua ya posa sijapeleka kwa miaka yote 7

Nishaurini wakuu nifanyaje nipate hela ya kutosha nikajitambulishe kwao na kutoa japo kishika uchumba,manake naona heshima itapotea kabisa kwa wakwe zangu na ndugu zake kisa sijalipa mahari wala kishika uchumba na hii ni kwa sababu hali yangu ya kipato ni ndogo mno naweza kulipa kodi,kula na kidogo kutuma kwa watoto .

Ushauri please

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama mwanamke iko poa financially, tell her,either achukue mkopo ukafanye biashara
 
Kama mwanamke iko poa financially, tell her,either achukue mkopo ukafanye biashara
Yuko poa alichukua mkopo wa kwanza M 15 ila daaaah yote akaipiga kivyake mi sikutaka kumwingilia kwenye fedha zake ,now kaniambia atachukua mwingine ndo namsikilizia anikopeshe kiasi nipambane na biashara nna hasira kinyama na kutafuta hela ila mtaji ndo mtihani!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nyinyi ni dini gani? Kama ni wa Wakatoliki nendeni kwa padri muandikishe ndoa. Mnafunga ya kati kati ya wiki baada ya misa ya kwanza. Nyinyi na mashahidi wenu tu lakini mtaishi kwa haki mbele ya macho ya Mungu.
Mkuu hapa napo ni utata manake mi muislam yeye mkristo na kwao wanaulokole flani na yeye kubadili Dini hataki ,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom