Miaka 60 ya Uhuru wa Tanganyika 1961: Alhaji Tambaza anamweleza Mama Daisy

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,915
30,259
MIAKA 60 YA UHURU WA TANGANYIKA 1961: SIMULIZI ZA ALHAJI TAMBAZA "MWAMVUA MRISHO MPIGANIA UHURU..."

Katika kuadhimisha miaka 60 ya uhuru wa Tanganyika leo nimekutana na makala aliyoandika Abdallah Tambaza katika gazeti Tanzania Tanganyika akieleza historia ya Mama Daisy katika kupigania uhuru wa Tanganyika.

Mama Daisy ni maarufu kwa wasomaji wangu nimemtaja sana.

Yeye alihifadhi historia nyingi sana ya kuasisiwa kwa TANU kwani aiikuwa mke wa Abdul Sykes.

Hili ni gazeti Tanzania Tanganyika ndiyo leo nimelitia machoni.

Hakika makala hii imetoka siku muafaka kabisa wakati wa sherehe za miaka 60 ya uhuru wa Tanganyika.

Lakini kubwa ni kuwa jana usiku katika hotuba ya Rais Samia Suuhu Hassan kwa taifa katika kuadhimisha miaka 60 ya uhuru wa Tanganyika, Rais aliwaadhimisha waasisi 17 waliounda TANU kwa kuwataja wazalendo hawa kwa majina yao ndani ya hotuba yake.

Haikuwa kama ilivyozoeleka ile ya "Nyerere na wenzake."

Hili alilofanya Rais halikupata kufanyika huko nyuma kiasi ikawa inaonekana kama vile waasisi wa TANU hawakuwa na umuhimu wowote katika historia ya Tanzania.

Mwaka wa 1968 Abdul Sykes alipofariki magazeti ya TANU, Uhuru na Nationalist hawakuchapa taazia yoyote kama vile aliyefariki hakuwa na uzito wowote kwa TANU.

Mhariri wa magazeti haya ya TANU wakati ule alikuwa William Benjamin Mkapa.

Jambo hili la kupuuzwa baba yake lilimuudhi sana binti yake Abdul Sykes, Daisy kiasi cha kutaka kuandika kitabu cha maisha ya baba yake ili aeleze mchango wa baba yake si kwa TANU peke yake bali hata kwa Julius Nyerere.

Wakati ule Daisy alikuwa mwanafunzi University of East Africa, Dar es Salaam Campus akisoma Education and Histrory.

Mwalimu wake wa historia, John Iliffe alimwambia kuwa afanye subira alipe somo hilo muda atakuja kuandika baadae.

Huu ndiyo ukawa mwisho wa kitabu hicho kilichokusudiwa na Daisy.

Juu ya haya yote Brendon Grimshaw mhariri wa Tanganyika Standard yeye alichapa taazia ya kupendeza sana ya Abdul Sykes akimwita marehemu, ''Abdul Sykes was a TANU Pioneer,'' yaani Abdul Sykes alikuwa muasisi wa chama cha TANU.

Taazia hii iliwaudhi baadi ya viongozi wa juu ndani ya TANU.

Mwaka wa 1988 gazeti la African Events takriban toleo lote lililoingia Tanzania lilikusanywa na inaaminika sababu ni kumtaja Abdul Sykes kama muasisi wa TANU.

Hakika historia inataka kupewa muda.

Jana Rais Samia Suluhu Hassan kawaadhimisha waasisi wote wa TANU kwa majina yao katika kuadhimisha miaka 60 ya uhuru wa Tanganyika.

Kama Daisy bado ana hamu ya kuandika historia ya baba yake basi wakati ni huu nusu karne baada ya kifo cha AbdulSykes.

Alhaji Tambaza akimjua vyema Mama Daisy na kaeleza hili vizuri sana katika makala yake.

Alhaji Tambaza katika hii makala yake amenifanya nami nimkumbuke mama yetu huyu baada ya kusoma kipande alichomweleza jinsi alivyokuwa akiwakirimu watu maarufu waliokuwa wakija kumtembelea mumewe wengi wao machifu wakubwa kutoka makabila makubwa ya Tanganyika.

Ilikuwa Mama Daisy ndiye katika mazungumzo yetu aliyeniambia kuwa Abdul Sykes alitaka sana David Kidaha Makwaia ajiunge na TAA wampe urais wa TAA kisha waunde TANU.

Mama Daisy alikuwa na mengi sana katika historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika.

Allah hakika ni muweza.

Leo tunaadhimisha miaka 60 ya uhuru wa Tanganyika serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Rais Samia Suluhu Hassan inawataja waasisi wa TANU kwa marefu na mapana na gazeti linachapa makala ya Bi. Mwamvua bint Mrisho mke wa Abdul Sykes.

Screenshot_20211210-060745_Facebook.jpg
 
Asalaam alyekum mzee wetu.
Naomba unitajie majina ya hawa watu pichani,
Je, Alhaji Jumbe Tambaza Mrisho ni namba ngapi hapo?
Ni namba 3 au namba 9?
Tunaomba ututajie na majina ya hao wengineo wasalaam.
51962246_1352592584883110_4181891733493121024_n.jpg
 
Back
Top Bottom