Zitto
Former MP Kigoma Urban
- Mar 2, 2007
- 1,562
- 10,880
Miaka 6 ya majaribu mengi katika maisha yetu ya kila siku, Watanzania. ACT Wazalendo tumekuwa upande wa Wananchi muda wote, wakati wote bila kujali ‘Consequences’.
ACT Wazalendo ni chama cha Watu. Ni Chama chako. Ni chama chenu. Ni chama chetu. Leo kimetimiza miaka 6 tangu kusajiliwa kwake hapo tarehe 5-5-2014.
ACT Wazalendo itaendelea kuwa upande wa Wananchi. Ninaomba tuendelee kwa MSHIKAMANO kupigania Uchaguzi Huru, wa Haki na unaoaminika. Ninaowaomba muipe dhamana ACT Wazalendo ili ijenge Tanzania yenye Watu wenye Raha na Furaha #KaziNaBata
Zitto Kabwe
Kiongozi ACT Wazalendo
May 5, 2020.
- Tumekuwa na Wazanzibari walipoporwa haki yao ya kuchagua Kiongozi wanayemtaka!
- Tumekuwa na Wakulima wa Mbaazi, Korosho, Pamba, Tumbaku na Karafuu walipoharibiwa masoko ya Bidhaa zao na kudhulimiwa Fedha zao zinazotokana na jasho lao.
- Tumekuwa na Wavuvi wa Baharini na Ziwani - walipochomewa nyavu zao na kuharibiwa maisha yao
- Tumekuwa na Wafugaji walipovamiwa kuondolewa eneo la malisho ya Mifugo yao.
- Tumekuwa na Wafanyabiashara wanabambikiwa Kodi kubwa, kutolipwa Fedha zao za marejesho na kufunguliwa kesi za utakatishaji
- Tumekuwa na Wanaharakati wa Haki za Binaadamu na Waandishi wa Habari wanapobambikiwa kesi na kuwekwa jela, kutekwa, kupotea na hata kuuawa.
- Tumesimamia Uhuru wa Taasisi za Uwajibikaji kama CAG na kuhakikisha Katiba ya Tanzania inalindwa na kuheshimiwa
- Tumekuwa na Wanasiasa wenzetu wanapoonewa na kunyimwa haki zao bila kujali Vyama vyao.
- Tumekuwa na Wananchi kuwaelemisha kujikinga na virusi vya Korona ili kuzuia vifo vya Watu wetu na kuiwajibisha Serikali kwa kushindwa kuongoza vyema Vita dhidi ya Ugonjwa wa COVID 19.