Miaka 54 ya uhuru lakini mambo si mambo

Miaka 54 ya uhuru lakini mambo si mambo

Hivii hayo mabadiliko mnayotaka ni yapi?? Mnataka mjee muwekewe fedha mfukoni?? Tatzo vijana wakitanzania ni wavivu fursa zipo lakin hamzitumii. Kama umeshndwa kujikomboa usitegeme hiyoo UKAWA itakuja kukupa mtaji. Nauhakika MAGUFULI ni bora zaidi ya LOWASA
 
Habari ndugu zangu wa JF,

Me ni mgeni kwa maana ya kuandika uzi lkn ni mkongwe kwa kufatilia jf naomba kwa akili ya chini kabsa tutafakari haya kwa miaka 54 ua uhuru.

Ukienda shule kuna walimu ila hakuna elim hospital kuna wauguzi lkn hakuna tiba, mashambani kuna wakulima ila hakuna kilimo, airports kuna viwanja ila ndege hatuna, mahakamani kuna sheria lkn hakuna haki, polisi kuna askari lkn hakuna usalama, maofisini kuna watumishi lkn hakuna huduma, madukani kuna bidhaa lkn pesa hatuna, ukisafiri njia zipo ila barabara ndo hakuna. Hata haya nayo hatujiongezi, bado tunahitaji darubini kuona?

Ama calculator kung'amua? It doesn't need a rocket science to understand, sawa watanzania akili hatuna,hata macho jamaniii?

Yaani umeniharibia siku. Unasema eti kuna polisi hakuna usalama? Ebo! Hebu nenda Nigeria, Kenya, Afghanistan, Syria ukafanye study toure! Usiseme kabisa kuhusu jeshi kipenzi chetu. Linajitahidi mnooo! Hivi kwa nini hadi leo hii tunakunywa bar hadi swalaa, harusi zimepangwa foleni uliwahi kuona wanakodiwa askari na bunduki huko tunakokesha na kumeremeteshana? Hivi hao wanaokamatwa kila siku tanga, stakishari, na wengine kibao husikii? Hivi vita ya kagera kumtoa nduli ulikuwepo duniani? Hivi chezea jeshi la tz weye? Heshimaaaa mbeleeee. ..hao ndiyo wanaume wa shoka Africa!
 
Gud umegusa pazur sn,kwa umri tulionao km taifa kwa nn tusiwe na viwanda vyetu had twendde singapore? afu huko singapore bc tungeenda ht na ndege ya ATC bc,binafc nmeganya jtihada kubwaa kupga hatua tatzo mm c mbinafs kuuna wengne wanaonizunguka na kila nnapojarib kuwasaidia nakwama ukifatilia unakuta kuna tatizo kubwa la msing lilillotokn na mfumo mbovu uliojengwa na ccm
 
Duuuu! Kweli umenifumbua kuliko kawaida ndugu yangu. Ngoja MAGAMBA waje uone walivyojazwa ufisi kichwani. Wao hawaoni hayo kabisi.

Hahaaa kwanza nimecheka kwa art yako uliyotumia kujibu hoja. Sasa mimi niulize hivi kumbe kuna ndoto kwamba ikiwezekana watu wanapozaliwa basi wakute kila kitu kama mbinguni kwamba nyumba ipo, gari upewe tu, ule ulale jasho hapana, ikibidi na mke upewe tu bila kutongoza yaani uvivu uvivu tu mwanzo mwisho! Yaani tunatamani kuishi kwenye nchi ambayo wewe na mimi hatutafikiri na kufanya kazi tena? Mimi nadhani kazi iliyobakia tuimalize kwa kuchagua viongozi bora sasa ili nasi tuwe washirika wa kutendea haki maisha yetu siyo kustarehe tu.

Kwani hao mnaosema hawafai walichaguliwa na nani kama siyo sisi wananchi tunaolalamika leo? Au ufisadi ni chain hadi kwa wachaguaji? Kila kitu na wakati wake. Sasa umefika wakati wa KAZI TU kwani mazingira yote yanaruhusu. Usichague mtu anayeota kwenda kuanza kufanya review ya yaliyopita badala ya KAZI TU. Muda utaisha bado anatueleza nani alifanya nini lini? SASA KAZI TU...ilikuwa ikawa peleka kuleèee
 
Miaka 54 waheshimiwa wanasafirisha Twiga , walalahoi tunavutwa mikwanja yetu kujenga maabara.
 
Gud umegusa pazur sn,kwa umri tulionao km taifa kwa nn tusiwe na viwanda vyetu had twendde singapore? afu huko singapore bc tungeenda ht na ndege ya ATC bc,binafc nmeganya jtihada kubwaa kupga hatua tatzo mm c mbinafs kuuna wengne wanaonizunguka na kila nnapojarib kuwasaidia nakwama ukifatilia unakuta kuna tatizo kubwa la msing lilillotokn na mfumo mbovu uliojengwa na ccm

Swali zuri rafiki. Sasa nikuelimishe tu maana hakuna jinsi; sasa tangu lini nchi ikaendelea bila hatua za kihistoria? Yaani tangu lini mtoto akazaliwa tu halafu huyo anaenda kuolewa au kuoa hata balehe bado. Yaani kuendeleza taifa ni hatua ndiyo maana mwenye busara mmoja amesema kwamba SASA KILA KITU TAYARI KILICHOBAKIA NI KAZI TU! Hili neno ni kubwa sana tatizo unaogopa mabadiliko ya kazi unataka mabadiliko ya chama. Kazi kweli.
 
Hivi na uchumi nao ulisoma wapi rafiki? Kama samaki afuatavyo mkondo wa maji ndivyo na bidhaa sokoni hufuata wanunuzi. Hivi darubini yako haioni vitu vilivyojazana madukani huku wauzaji kila siku wakipanga foleni airport kwenda Singapore na dubai kuleta vingine? Hivi wakivileta huwa wanamuuzia nani? Hivi huoni shamrashamra za magraduation na maharusi ya bei mbaya? Hivi unadhani wanatumia nini kama siyo pesa? Tatizo liko kwako kwamba hukutumia fursa tele kwa sababu una shida ya darubini yako kwamba haina focus nzuri. Ama huna jitihada unasubiri pesa zijazwe mfukoni kwako. Punguza kulala usingizi, sasa amka, changamka, jichanganye, pambana. Hata ulaya baadhi ya wasomi wanaosha masufuria. Kuna factors nyingi sana za ku analyse kwa nini uko au tuko hivi tulivyo. Lipi tumechangia mimi na wewe na kipi kimechangiwa na yule na wale. Hakuna serikali duniani inayokuja eti na majawabu. Serikali inaweka mazingira halafu wewe na mimi tunatakiwa kuyaona na kuyatendea haki. "Watu wangu wanapotea kwa kukosa maarifa". "Millions saw apple fall but only newton asked why". Hivi ulikuwa kundi gani enzi hizo?!
Khaa!! Huu ndiyo ukweli. Nakugongea one million likes
 
Hivii hayo mabadiliko mnayotaka ni yapi?? Mnataka mjee muwekewe fedha mfukoni?? Tatzo vijana wakitanzania ni wavivu fursa zipo lakin hamzitumii. Kama umeshndwa kujikomboa usitegeme hiyoo UKAWA itakuja kukupa mtaji. Nauhakika MAGUFULI ni bora zaidi ya LOWASA

Wengine hizo fursa za kukwapua mali na wizi kupitia ccm atuko tayari kuzitumia ila tuko tayari kufanya kazi halali mkuu.
 
Yaani umeniharibia siku. Unasema eti kuna polisi hakuna usalama? Ebo! Hebu nenda Nigeria, Kenya, Afghanistan, Syria ukafanye study toure! Usiseme kabisa kuhusu jeshi kipenzi chetu. Linajitahidi mnooo! Hivi kwa nini hadi leo hii tunakunywa bar hadi swalaa, harusi zimepangwa foleni uliwahi kuona wanakodiwa askari na bunduki huko tunakokesha na kumeremeteshana? Hivi hao wanaokamatwa kila siku tanga, stakishari, na wengine kibao husikii? Hivi vita ya kagera kumtoa nduli ulikuwepo duniani? Hivi chezea jeshi la tz weye? Heshimaaaa mbeleeee. ..hao ndiyo wanaume wa shoka Africa!

Kweli alie shiba amkumbuki mwenye njaa . Albino wanauawa na polisi inavamiwa eti usalama
Tumieni ubongo kufikiri nasi moyo mkuu
 
Khaa!! Huu ndiyo ukweli. Nakugongea one million likes

Nawasingapore wangapi wanapanga foreni airport pale singapore kuja kununua bidhaa Tanzania? Alafu utakuta na wewe eti una dugwirii
 
Mm pia nafanya kazi halalii. Kwhyo kila aliyefanikiwa ni mwizi kupitia ccm?? Basi hata huyo Mboye,Lowassa,Ndesamburo ni wezi kupitia ccm. Endelea kusubiri mabadiliko kupitia UKAWA halaf ubweteke ndani kama hujaendelea kuwa masikinii
 
Wewe ndo ufanye kazi halali au unamsemea mwingine. Ata siku moja na ndo linawafanya muogope maana no more chance for illegal business dude!Madawa ya kulevya na list ya wauzaji vipi?
 
Mleta uzi kapagawa kama haoni kilichofanyika hata wakija malaika atawaponda tu acha kukariri
 
SISUBIRI MIUJIZA!!
“Ni jamii iliyochoka na kuchakaa; ni jamii iliyooza na kuchoma pua kwa harufu ya uvundo wa rushwa na kujaza nzi wakubwa wa rangi ya Kijani, Ni jamii yenye ufisadi na ukandamizaji; ni jamii isiyojua mbele wala nyuma, ni jamii iliyokosa dira”. Bunge lipo kwa jina tu kwa sababu limewekwa kwapani na watawala; Madaraka ya Rais ni makubwa kwa kiwango cha kupora demokrasia: Utajiri wa nchi upo mikononi mwa kikundi kidogo cha “wateule” na watawala kilichowageuza wananchi wadunda kazi wasiofaidi jasho lao. Na pale maandamano ya wanawake, wanaume na vijana wenye njaa yanapopita karibu na Makazi ya Wenye nacho,Malodilofa husimama ghorofani, wakawatazama na kuuliza, “kulikoni?”. Na walipoambiwa kwamba yalikuwa ya “malofa” wenye njaa waliokosa mkate wa kila siku, wao walijibu: “Kama ni hivyo, kwa nini wasile nyasi na mihogo?”Vijana wanaangamia kwa kukosa maarifa mashuleni na wanaishia kubwia "unga" ambao ni biashara pendwa ya Malodilofa,vijana wasanii wenye vipaji mbalimbali wanageuka ombaomba na wakati wa Kampeni wanakuwa "lulu" kwa kutumika kujaza “nyomi” katika mikutano,wakulima wanazeeka kwa kazi ngumu mashambani na kukosa pembejeo za kisasa na mazao yao yanaishia kukopwa kwa bei ndogo ajabu,wavuvi wanachomewa nyavu zao walizonunua kwa wafanyabiashara wajanja wenye meno,wawindaji wa vitoweo wanaambiwa ni majangili huku tembo wakiuwawa kwa tama ya meno yao na twiga wakipandishwa ndege kwenda ulaya na Asia..Dah! wagonjwa wanakufa huku wamelala mzungu wanne sakafuni mahospitalini kwa kukosa madawa,wakina mama wanajifungulia vichochoroni kwa ubovu wa barabara, Na wanapoona malofa wanawapigia kelele kwa madai yao sahihi wanaamuru majeshi ya ndugu zao wanyonge wawapige mabomu ya machozi na kuwaua na kuwasababishia vilema vya maisha na kuwatesa waandishi wa habari zao za kilofa.Watawala wetu hivi leo wanatuhumiwa kumiliki mabilioni ya fedha wanayomiliki huku wakiyaita ni “vijisenti”, au “fedha ya mboga”, wakati kipato cha Watanzania walio wengi ni chini ya shilingi mia nane kwa siku. Wananchi wanapopiga kelele kugugumia bei kubwa ya kivuko wanaambiwa “Wapige mbizi” na pale ndege ya Rais na rada chakavu inaponunuliwa kwa pesa nyingi zenye asilimia kumi za wajanja wanaambiwa “Ni heri wale nyasi”…Pamoja na mikakati mikubwa na yakutumia fedha na rasilimali nyingi za walala hoi kwa ajili ya kuvuruga "Mabadiliko" kwa kuwanunua wanasiasa uchwara na kuwakashfu kuwa ni “wapumbavu,amlofa na mbumbumbu”. Wakati umefika,chama kilichokuwa na dhamana ya haya yote kipumzishwe,ili kijitafakari,kitakapokuja kwa mara nyingine (MUNGU akikijaalia) kije kikiwa kamili....Kwa wakati huu,nathubutu kusema,Naichagua UKAWA,...sio kwa sababu za uimara wa CDM,CUF,NLD,NCCR MAGEUZI ama Uimara wa UKAWA la hasha!!Ila ni kwa sababu ya udhaifu wa CCM na ahadi ilizoshindwa kuzitekeleza kwa miaka 54 mfululizo.“ALUTA Continua, Victoria Ascerta”.... “The Struggle Continues, Victory is Certain”; ...Mapambano yanaendelea, Ushindi unakuja!! ≠HapaNimakwenziTu!!
 
Nawasingapore wangapi wanapanga foreni airport pale singapore kuja kununua bidhaa Tanzania? Alafu utakuta na wewe eti una dugwirii

Hivi rafiki unafahamu maana ya utandawazi? Hivi kama hatua zote za maendeleo zingefanyika yote yakaisha kusingekuwa na sababu ya wewe kuwepo tena? Hivi unajua hata huko mbinguni kazi hazijaisha kwa sababu kuna kukesha ukiimba na kusifu? Sasa sijui wewe utaishi wapi kusiko na masalia ya kazi. Funguka. Badilika mtazamo na siyo chama. Wakati wa KAZI TU UMEFIKA.
 
Hata marekani wenye miaka zaidi ya 300 ya Uhuru bado kuna maskini wanaokulia kwenye makopo tena mpaka leo bado ubaguzi uko pale pale ..wewe unakuja kushangaa hapa TZ? na hata sie tukifa vizazi vijavyo watakuwepo maskini na watakuwepo matajiri labda uishi pekee yako hapa duniani
 
Hata marekani wenye miaka zaidi ya 300 ya Uhuru bado kuna maskini wanaokulia kwenye makopo tena mpaka leo bado ubaguzi uko pale pale ..wewe unakuja kushangaa hapa TZ? na hata sie tukifa vizazi vijavyo watakuwepo maskini na watakuwepo matajiri labda uishi pekee yako hapa duniani

Afadhali Rweye wewe unatazama mambo kwa mtazamo mpana. KAZI TU zikishaanza wewe utafika mbali maana unaona kwa jicho la busara. Hawa wengine wanaotazama kwa jicho la chuki na hasira wataendelea kubadilisha vyama kila baada ya miaka 5 lakini mifuko yao hawatajaza kitu maana sharti watoke jasho kwa kuzitendea haki fursa zitakazokuwepo. Hao wenyewe wasaka ikulu hawali hawalali wanaumiza vichwa leo wasindikizaji tunataka mteremko tuu. .NI KAZI TU ndiyo jibu! Saafi sana waeleze kuwa hata ulaya wapo tu weeengi
 
Nawasingapore wangapi wanapanga foreni airport pale singapore kuja kununua bidhaa Tanzania? Alafu utakuta na wewe eti una dugwirii

Tatizo lako umekimbia kijijini kwenye mashamba umekimbilia mjini sijui kufuata nini sasa. Hebu waulize wenzio wenye nyumba za bati, TV, friji, smart phone na mazaga kibao huku wa kivuta hewa safi huko kijijini huwa wanapata wapi pesa za maendeleo? Hivi wa singapore wanahitaji kweli kuja huku au kuagiza tu vitu vinapakiwa? Sisi wa bongo tunaenda huko kama sehemu ya kuosha macho eti.
 
Back
Top Bottom