Miaka 52 ya uhuru wagonjwa wanabebwa kwenye machela

Miaka 52 ya uhuru wagonjwa wanabebwa kwenye machela

Mlyafinono

Senior Member
Joined
Apr 6, 2012
Posts
177
Reaction score
48
DSC04409.JPG Mgonjwa aliyebebwa kwenye machela ni mkazi wa kijiji cha Uleling'ombe kitongoji cha Lengewaha,Jimbo la Mikumi.Kunauchimbaji wa Dhahabu na Shaba unafanyika huko lakini miundombinu bado ni duni.Madini yanachukuliwa huku wananchi wakiachiwa mashimo.Ni rasilimali za taifa lakini wanataifa hawanufaiki nazo.Hali hii mpaka lini? inauma sana.
 
mapenzi mema kwa CCM yatawacost sana...si unaona jamaa ana kofia ya kijani hapo..
acha waendelee kuumia..
 
Inasikitisha sana tunasaini a lot of international declaration kama vile Abuja declaration but we can not budget 15% for health budget zaidi ya kuingiza fedha kwenye chai. Watanzania twafa wao watibiwa India. Poa tu kwa Mungu wote sawa ufie Mwananyala au Appolo India udongo utalba tu
 
sitawasamehe watz kwa kuichagua CCM, na Mungu ataendelea kututia Bakora hadi tutakapopata Akili ya kujua kutenganisha mema na mabaya.
 
Wale wanaotupa tabasamu la nguvu wanatiwa na kubadilishiwa damu kila siku majuu kwa kodi zetu. Sisi tunakufa kubebwa kwenye makapu kama kuku. Kisha ni ujinga tu wa kutoweza kuwachagua viongozi wenye uchungu na nchi yetu. Huyu Kikwete na genge lake la wezi wametusaidia nini? Wanakopa matrilioni wanajinufaisha, wanawekeza Uswizi, wanatibiwa India na kwingineko sisi wanatuacha katika hali hi. Wanagawa dhahabu, gasi asilia, makaa ya mawe, pembe za ndovu, n.k. kwa wageni tena bure huku watanzania wengi tukifa bila iidadi kwa kukosa tu mahitaji muhimu yakiwepo matibabu. Tuache upuuzi watanzania huyu raisi ni wa kuulia mbali na CCM yake. Tuweke watu wengine madarakani halafu tuwahukumu kwa kile watakachokifanya.
 
Imekuwa ni kawaida kwa watanzania wanaoishi wilaya za Kyela na Ileje kuvuka mpaka na kwenda kutibiwa nchi jirani ya Malawi kwa sababu kule huduma ya afya ni bora zaidi, Na Wamalawi hawana kinyongo na hilo wameendelea kuwasaidia Watanzania wenzetu.

Hilo limethibitishwa pia na Mbunge wa Ileje Ndg. Aliko Kibona katika ufunguzi wa zahanati moja iliyoko mpakani mwa Tanzania na Malawi. Ameishukuru serikali ya Malawi kwa kuendelea kuwahudumia watanzania

Nawasilisha
 
Ni kweli kabisa , na hata ikitokea bahati mbaya kwa mgonjwa kutoka Tz kufariki kwenye hospitali hizo , Malawi Govt hu provide hata usafiri wa gari la maiti hadi mpakani , nina ushahidi wa jambo hilo hasa kwa Wilaya ya Kyela , vijiji vya Mpakani kama Isaki ,Kasumulu , Kabanga , Katumbasongwe nk ni kama vile ni sehemu ya Malawi kwa matibabu , siku za nyuma kidogo hata bei nzuri ya mazao ilipatikana Malawi , Watz wengi sana wameuza Korosho Malawi , mwenye kumbukumbu hawezi kusahau haya .
 
Ndugu wasomi wa jf katika mtandao wetu tusishindane kwa matusi mashindani yetu yaunganishwe kwa hoja nzito na ushahidi wa kutosha.Na yule anayepinga hoja ya mtu ni sawa ila atoe ya kwakwe na ushahidi wakutosha.

Mfano,mtoa mada hapo juu amesema tanzania tokea ipate uhuru ni miaka 50.hapo panaonesha pana udhaifu elimu,kutojifunza na kutosoma ulioambatana na uvivu wa kutataka kuelewa mambo.

Ndungu yangu mtoa maada usione kama ninakuzalilisha ila nataka nikuweke na kufanye kuwa mwangalifu unapoweka maada hapa jf.Naomba nikukumbushe kua tanzania haikupata uhuru iliyopata uhuru ni tanganyika 9.12.1961.kwaheri
 
sio geni hilo hasa kwa ukaribu wa hizi nchi zetu sasa ata hao majiran ishu nyengine wanafanya huku kwetu
 
Ni kweli. Na hata wanyasa wanategemea vitu kadhaa kutoka wilaya zetu za mpakani na Tanzania kwa ujumla. Ndiyo ujirani ufaao - kusaidiana.

Ndiyo maana mgogoro wa ziwa unatakiwa utatuliwe kwa njia zisizo za kivita.

Lengo la mchango huu sio kuwatetea watendaji wa Tanzania kwa huduma za afya (au nyinginezo)zilizo duni.
 
hawa jamaa na ugomvi wa mipaka hawata chomwa sindano ya sumu
 
Back
Top Bottom