William J. Malecela
R I P
- Apr 27, 2006
- 26,584
- 10,466
Watanzania tunaposherehekea Miaka 52 toka tupate uhuru siku ya Desemba 9, 1961 kutoka kwa Waingereza, wakiongozwa na Gavana Richard Turnbull aliyeukabidhi rasmi kwa Waziri Mkuu wa kwanza Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere katika Uwanja wa zamani wa Taifa mjini Dar es saalam. Tanzania tulipata Uhuru wetu tukiwa tunaongozwa na Chama cha TANU ambacho Baba wa Taifa alikuwa ndiye mmoja wa Waasisi wake na Mwenyekiti wake wa kwanza ndani ya uhuru, chama hicho baadaye kilifungua mlango na kupasia kijiti kwa Chama kipya cha Mapinduzi CCM ambacho kilikuwa ni matokeo ya kuungana kwa TANU na Chama Tawala cha Zanzibar Afro Shiraz Party na kuzaliwa Februari 5, 1977. Leo CCM ni chama ambacho kinashikilia rekodi ya guiness kwa kutawala kwa muda mrefu kuliko vyama vyote vilivyoko madarakani barani Africa.
Baba wa Taifa ambaye pia ndiye muasisi na muanzilishi wa kwanza wa CCM, alikuwa na ndoto kubwa za kukiona chama hicho alichokipenda kuliko kitu chochote katika maisha yake kikisimama kidete kama kimbilio la wanyonge nchini. Mtoto hazaliwi siku moja na kutembea siku hiyo hiyo, katika miaka 52 ya utawala wake kwa hili taifa CCM imefanya makosa machache yanayozungumzika na lakini pia mazuri makubwa mengi sana ikiwa ni pamoja na kukubali kuwepo kwa vyama vingi vya siasa nchini mwaka 1992. Ni dhana hii ambayo aliisimamia mwenyewe Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere, licha ya wananchi Asilimia 80 wa taifa hili kutoa maoni yao kwa kutumia kura maoni kukataa kuwa tayari kwa siasa za vyama vingi. Kuwepo kwa vyama vingi nchini mpaka sasa kumekisaidia sana kukiimarisha Chama Cha Mapinduzi zaidi kuliko kuvisaidia vyama hivyo ambavyo vimekuwa vikienda bila ya dira maalum wala mipango makini ya ushawishi kwa wananchi na kuishia kuwa msaada mkubwa wa kuiimarisha chama hicho tawala. Ndoto ya Baba wa Taifa kwa chama chake Cha Mapinduzi ilikuwa ni pamoja na kukiona siku moja kinakuwa bingwa wa new African Socialism yaani Ujamaa na Kujitegemea na kuwa chama ambacho kinakuwa na mrengo wa kushoto zaidi.
Ingawa leo chama hicho kikongwe Afrika, kimechukua mrengo mpya wa neoliberal ambao umepelekea kuwa na siasa za economic modernization na free market policies kama njia za ku-raise standards of living kwa wananchi wa Tanzania, moja kati ya nchi masikini sana Duniani. CCM hopes to continue privatize and modernize ili kuhakikisha kwamba ina:- inoangeza uzalishaji ili kuongeza pato la taifa, kuongeza ajira kwa vijana na uongozi ulio bora, kupata njia mpya za kiteknologia na za kisasa zaidi, kupanua soko la bidhaa zatu nje na hapa nyumbani, kuiimarisha sekta ya binafsi ambayo ndio engine ya uchumi wa Taifa huku Serikali yake ikijipanga vyema kwenye social services, infrastructure, security and governance of the state. Kwenye siasa za nje CCM major foreign policy focus ni economic diplomacy katika nyanja za kimataifa na kuishi kwa amani majirani zetu wote.
Rushwa ndio pungufu kubwa sana ambalo Chama Cha Mapinduzi kimekuwa kikishutumiwa sana na wananchi na hasa wafadhili wetu wakubwa kutoka nje na jumuiya za kimataifa. Rushwa limekuwa ni tatizo kubwa sana linaloisumbua Serikali na CCM kwa ujumla katika utawala wake wa Miaka 52 kwa taifa hili. Tatizo hili lilianza kuamsha hisia za Viongozi wa Taifa toka Miaka ya 70, wakati wa utawala wake Baba wa Taifa aliyeiiita rushwa kuwa ni a form of oppression that undermined egalitarian values ingawa ripoti za kutumia madaraka vibaya hasa katika sekta ya vyama vya ushirika na mashirika ya umma ziliongezeka sana kufuatia mpango wa Serikali kupanua uchumi. Katika kilichofuatia cha utawala wa Rais Mwinyi mwaka (1985 - 1995), rushwa iliongezeka kwa kasi kubwa sana mpaka kupelekea wafadhili wa kimataifa kusimamisha misaada yao mwishoni mwa mwaka 1994.
Wakati wa uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi vya siasa Mwaka 1995, vyama vya upinzani vilijaribu kila njia kutumia rushwa kama dhana yao ya kukubalika na wananchi, lakini CCM ikawa na akili nyingi sana za kuwaweka pembeni viongozi wake wote waliokuwa na tuhuma za rushwa na kuwaweka wasiokuwa na tuhuma na kuishia kuwashinda wapinzani kwa asilimia kubwa sana. Mgombea urais wa CCM Mh. Benjamin Mkapa alitumia kampeni za uchaguzi kuweka msimamo mpya wa CCM kupigana na rushwa na kweli katika utawala wake baada ya kuunda kamati maalum ya rushwa alijitahidi sana kupigana na rushwa kufuatia mapendekezo maalum ya kamati ile na kwa mara ya kwanza wafadhili wakaridhia na kurudisha tena misaada yao kwa taifa na hata kutufutia deni la Dola za Kimarekani USD $ 3 Billion ambalo kwa wakati ule lilikuwa ni nusu ya deni zima la Taifa. Matokeo ya juhudi za Mkapa kuondoa rushwa ni suala linalojadilika kutegemea na kona ya msimamo wa siasa ya anayejadili, lakini ni kitu kinachokubalika na wananchi wengi kwamba angalau now rushwa is not tolerated as it was before na aliweza kubadilisha njia za kirahisi rahisi zilizokuwa zikitumika katika kuomba rushwa kwa wahusika.
Pia katika miaka yake 52 ya utawala wa CCM pungufu lingine kubwa lililojitokeza ni kuonghezeka kwa gap ya wasionacho na walionacho, ingawa pia ni tatizo kubwa lililoanzia kimataifa kwa kuwa na mataifa yaliyonacho na yasiyonacho yaani "developed and undeveloped world" ambapo mwaka 1975 GNP for Germany ilikuwa ni USD $ 3,390 kulinganisha na Tanzania USD $ 120. Yaani kunakuwepo na wananchi wachache ambao wana vast opportunities and their loved ones while others possesed nothing to that effect. Katika miaka ya karibuni wananchi wa Tanzania wamejionea Matajiri wachache wakiongezeka kwa kasi kubwa sana, huku masikini pia wakiongezeka kwa kasi kubwa na kwa wingi sana. Haya ni matatizo makubwa mawili ambayo yamekuwa yakiiandama Serikali ya CCM kwa miaka yake 52 ya kuwepo madarakani na wala sio siri kwamba pamoja na kujaribu sana kupigana nayo bado chama hicho kinahangaika sana kupata jawabu la kudumu la kumaliza matatizo haya mawili, ambayo hata vyama vya upinzani vimeshindwa kuyatumia kwa faida yao kutokana na wananchi wengi wa Tanzania kukata nayo tamaa na kuamua kwamba wanasiasa wote wapo sawa tu.
Mnyonge mnyongeni lakini CCM chini ya Mwenyekiti wake Rais wa sasa wa Tanzania Dk. Jakaya Kikwete, na Katibu wake mkuu wa kwanza wa miaka ya karibuni mwenye uwezo mkubwa wa kufanya kazi kimekuwa kikionyesha njia kwa kutawala kwa mfano na sio maneno maneno mengi kama ilivyokuwa huko nyuma, hasa baada ya Baba wa Taifa kuachia ngazi mwenyewe. Kinana baada ya kuchaguliwa tu alianza Ziara za kutembelea Mikoani, Wilayani na Vijijni na mpaka sasa ninaponadika waraka huu yupo Mkoa mpya wa Njombe akiendelea uongozi huu mpya wa kuongoza kwa matendo na mfano.
Kwa mfano mwishoni mwa Mwaka 1961 Baba wa Taifa ndiye aliyeweka msingi huu wa kuongoza kwa mfano, alipojiuzulu Uwaziri Mkuu na kwenda Mikoani, Wilayani na Vijijini kukiimarisha chama cha TANU ambacho hatimaye Mwaka 1962 aligombea na kufanikiwa kuwa Rais wa kwanza wa Jmahuri ya Tanganyika.
Baba wa Taifa alitumia muda mwingi sana akiwa ndani na nje ya CCM kukosoa Viongozi wabovu na miundo mibovu katika Cham hicho, kama anavyofanya sasa Kinana, badala ya kukaa ofisini kusubiri kuletewa matatizo ya wananchi yeye ameamua kuwa kama Baba wa Taifa kwenda kuwafuata wananchi na kusikia kero zao na kuzisema na kuzikubali wazi kwamba ni mapungufu ya Serikali ya chama chake na kwamba yupo tayari kuyakabili. Kwa mfano majuzi akiwa Mikoa ya Kusini alifika mahali penye kilimo kikubwa sana kwa Mkoa ule akaambiwa hakuna Waziri yoyote wa Kilimo aliyewahi kufika pale toka tupate uhuru pamoja na kilimo chote pale, ilimpelekea Kinana kuamua na kusema wazi mbele ya Taifa kwamba atawaita Viongozi hao wanaolalamikiwa kwenye Kamati Kuu ya CCM kujibu tuhuma hizo kitendo ambacho kilipelekea Viongozi hao wanaotuhumiwa na wao kujibu tuhuma hizo mbele ya Taifa hata kabla kufika huko Kamati Kuu ya CCM. Hii inaitwa Demokrasia ambayo sio tu imewashinda Vyama karibu vyote vya Upinzani nchini hapa, bali hata Vyama vingi vikongwe vi;livyoanza kutawala wakati mmoja miaka 52 iliyopiuta na CCM.
NCCR walipojaribu kumkosoa Mwenyekiti wao Mrema, chama hicho kiliishia kusambaratika na kubakia kivuli tu sasa hivi, CUF nao walipojaribu kukosoana kama CCM ya sasa, kina Rashid waliishia kufukuzwa chama na sasa hivi tunajionea Chadema inavyoakribia kusambaaratika kutokana na viongozi wake kina Zitto na Kitila kujaribu kukosoa vuongozi wa sasa. Zambia UNIP kilikuwa ndio chama tawala kilichaoanza na CCM, lakini viongozi wapya walipojaribu kukosoa muundo wa kizamani wa chama hicho kikaishia kusambaratika na mpaka leo kimebaki kivuli chake, KANU Kenya yale yale Viongozi wake walipojaribu kukosoa kikaishia kubaki na kivuli chake mpaka leo. Wakati wa utawala wa Mwalimu kulikuwa na Viongozi wengi ambao hawakukubaliana naye, lakini Mwalimu hakuwahi kuwaita mamluki, wahaini au wasaliti kama ambavyo tunasikia kutoka vyama vyetu vya upinzani wanapotokea wakosoaji ndani ya vyama hivyo. Kulitokea kesi moja tu ambayo Waziri wa CCM Kambona aliamua mwenyewe kwa hiari yake kukimbia nchi kwenda Uingereza baada ya kutokubaliana na Azimio la Arusha. Mwalimu angewaita wale waliomkosoa baada ya kuacha UWaiziri Mkuu kama kina Sykes kuwa ni mamluki, wahaini na wasaliti basi ingekuwa ni vigumu sana kwa hili Taifa kupata uhuru.
Na pia chini ya uongozi wa JK na Kinana CCM imepitia wakati mgumu sana wa kukososlewa sio mara moja wala mara mbili Viongozi wake wakuu kama WAziri Sita, WAziri Mkuu wa zamani na mbunge wa sasa Lowassa, Mbunge wa Ludewa Filikunjombe, Wabunge Wapiganaji na wengineo wamejitokeza hadharani kukosoa sana chama hicho, lakini hatujawahi kusikia Mwenyekiti na Katibu wake Mkuu wakiwaita ni wahaini, wasaliti, Mamluki au Mapandikizi. Kwa mfano CCM ilipoamua kubadilisha katiba yake kwa ajili ya uchaguzi wa wajumbe wake wa NEC, mmoja wa waasisi wa chama hicho Mzee Kingunge Ngombale Mwiru alijitokeza wazi na kusema hakubaliani kabisa na mabadiliko hayo akiwa na maana hakubaliani kabisa na MWenyekiti wake wa Taifa ambaye pia ni Rais wa Jamhuri na Mzee Kingune alienda mbalia hata kusema kwamba anaomba aandikwe kwenye historia ya chama hicho kwamba alikataa kata kata mabadiliko hayo, lakini hatukusia MWenyekiti wake akimuita majina ya Mamluki, Mhaini au Pandikizi kama sio Msaliti. Isipokuwa Viongozi hao wamekuwa wasikivu na wenye uvumilivu mkubwa sana kama ule wa Baba wa Taifa. Kwa ajili ya kawaida unajiuliza chama kama Chadema kweli ni chama cha Demokrasia au ni chama kinachoogopa Demokrasia? Sijawahi hata siku moja kusikia CCM wakigombana kisa Katiba yao, katiba yao ipo wazi na inatekelezwa ipasavyo na Viongozi wake wakuu mpaka wa chini, sasa ninajiuliza hivi hawa Chadema wakishika dola itakuwaje hasa ninaposikia kwamba Viongozi wao wakuu wa Taifa wameshiriki sana kuipindisha katiba ili waendelee kuwepo madarakani bila uchaguzi si watapindisha katiba ya Jamhuri na kujiwekea kipindi cha tatu badala ya viwili vya katiba.
Kwa haya Kinana anayoyafanya sasa. Ni hoja mufulisi sana kutoka vyama vya upinzani wanaposema kwamba CCM imekaa madarakani kwa muda mrefu kwa hiyo wananchi wameichoka, ukweli ni kwamba muda mchache wa kuwa na vyama vya upinzani nchini wananchi wengi sasa tunajiuliza kulikoni na kama kweli Tanzania tuna upinzani wa kweli au ni wachumia tumbo tu wanaosubiri kugombania ruzuku za kodi ya wananchi kutoka Serikali ya CCM. Wananchi wa Tanzania sasa wanakiamini na kukitegemea sana Chama Cha Mapinduzi na infact hata kabla ya kuanzishwa kwa Wapinzani, wananchi Asilimia 80% walizungumza wazi kwa kupitia kura zao za maoni kwamba hawako tayari kukubali wapinzani, CCM kwa kuheshimu kwamba wakati ulikuwa umefika wa kuwa na Demokrasia ya kweli Tanzania iliamua kwenda kinyume na matakwa ya wengi na kuruhusu wapinzani ambao kadri miaka inavyokwenda wanazidi kujidhihirisha kwamba hawako tayari kukosolewa kama chama Tawala. Kwa mfano Chadema mara kwa mara imekuwa ikijaribu kujilinganisha na TANU iliyodai uhuru ile ya Baba wa Taifa, lakini linapokuja suala la kujikosoa ndipo chama hicho kinapojiweka wazi kwamba hakina uhusiano wowote wa kimatendo na kile cha Mwalimuambacho kinajaribu sana kujilinganisha nacho.
Kwa kumaliza naomba kusema kwamba CCM ya sasa ndio hasa ambayo Baba wa Taifa aliitaka na kuitengeneza au kuiota kuwepo hata asipokuwepo kama ilivyo sasa. Ni CCM inayosikia vilio vya wananchi Mwaka jana ilipobainika kutokea bungeni kwamba kuna Mawaziri Saba ambao ni mzigo kwa Serikali Kamati Kuu ya chama hicho iliyokutana Ikulu chini ya MWenyekiti wake Rais wa Jamhuri, iliyakubali kismingi malalamiko hayo ya wananchi na kuwapumzisha mawaziri hao mara moja.
Miaka michache nyuma yalipotokea malalamiko mengi bungeni kuhusu Waziri Mkuu wa wakati ule CCM haikusita kumpuzisha na imekuwa ikifanya hivyo kwa muda mrefu sana sasa na kukifanya chama hicho kuwa imara sana na kinachokubalika sana na wananchi wengi nchini ambao wamekuwa wakikichagua kwa Miaka 52 mfululizo na kukifanya kuwa chama pekee kikongwe kukaa madarakani kwa muda mrefu sana kuliko vyote Afrika. Ni chama pekee nchini ambacho katiba yake ipo wazi kuhusu tarahe zake za uchaguzi kuanzia Taifa mpaka kata, wananchi wa aina zote wapo huru kugombea nafasi zote za chama hicho bila kubaguliwa ni moja ya sababu kubwa ya kidemokrasia ya kweli inayokifanya chama hicho kuziidi kuwa imara huku vyama vingine vya siasa hapa nchini na Afrika vikyumba yumba na Demokrasia.
Tabia ya CCM kubadilishana uongozi kwa mujibu wa katiba yao kama vile alivyoanza BAba wa Taifa, na kumuachia MWinyi aliyemuachia Mkapa, aliyemuachia Kikwete ni Demokrasia adimu sana barani Afrika ambayo inakifanya chama hicho kuwa tofauti vingine vyote nchini na hata Afrika nzima ambako vyama vingi kutoka nje ya Tanzania vimekuwa vikija kujifunza kwa CCM. Matumaini ya WaTanzania wengi ni kuona chama hicho kikiendelea kuwa ngome ya kimbilio la wanyonge, dhana ambayo siku za nyuma hasa za utawala wa Marais wake waliopita walivuruga kidogo lakini chini ya MWenyekiti wa sasa na Katibu wake Mkuu Kinana chama hicho tayari kimeanza kujionyesha wazi kwamba kiko tayari kuwa chama kilichofikiriwa na muasisi wake Baba wa Taifa hili Mwalimu Nyerere.
MUNGU AIBARIKI TANZANIA
WILLIAM J. MALECELA