Miaka 50 ya Wachina kwenye bandari ya Bagamoyo, na hatima ya rasilimali za nchi yetu

The Gate of Heaven

JF-Expert Member
Jul 14, 2014
234
67
Wakuu mkataba wa bandari inayojengwa bagamoyo kwa hisani ya china unatia shaka sana.

Tunaambiwa kuwa china itatumia bandari hiyo kwa muda wa miaka 50 ndipo iikabidhi kwa serikali ya tanzania. Naomba tujiulize kwa miaka 50 hiyo rasilimali zetu kama magogo, madini, wanyama kama tembo na faru zitasalimika.

Ni kipi hasa kiliisukuma serikali kuingia mkataba wa kitapeli kama huu? miaka 50 sio midogo, hii itawafanya watanzania wa wakati huo wajute kwanini wamezaliwa Tanzania.
 
Haya ndio mambo ambayo yalipashwa kuingia katika katiba hata ya sasa na siyo maandamano yasiyo na mantiki. Nadhani kwa nchi zetu hizi kabla ya kutiwa saini mikopo na mikataba yote iwe inapitiwa na kuidhinishwa na bunge. Hili lingeingizwa katika katiba itakayoendelea kutumika ili tusiendelee kula hasara.
 
" tusiendelee kula hasara" kana kwamba mikataba inakuja automatic..... hao hao wanao ingia hii mikataba ya kitapeli ndo wasio taka mabadiliko unayo yashauri kwenye katiba.... then what next kama sio maandamano.....kama mtanzania kama wewe unae weza post kwenye JF una mawazo kama haya then we still have a very long way to go..... hoja yako ya kimburula tu wewe......
 
Wewe unaonekana kama mwanachama wa chadema maana unahasira za kijinga sana. Unadhani matusi yatakusaidia lolote? Kwa misingi hii hicho chama hakitakuja kuongoza katika nchi hii hata siku moja.
 
Hoja muhim ni kwamba kuna viongozi walio ingia mkataba huo wa kiaka 50 na hao hao ndo wanao pinga mageuzi makubwa ya katiba ya mwaka 77, sasa unatoaje ushauri wa namna hii? .... hapa unatakiwa utoe maoni yanayo tekelezeka... issue sio uchadema au uccm hapa wanao umia ni waTz... mimi na wewe....
 
50 years...miaka 50...kweli nchi imeshauzwa hivi hawa viongozi hii mikataba wanayoingia do their really seat down and read papers or they just take their 20%and sign papers..
 
Wakuu mkataba wa bandari inayojengwa bagamoyo kwa hisani ya china unatia shaka sana.
Tunaambiwa kuwa china itatumia bandari hiyo kwa muda wa miaka 50 ndipo iikabidhi kwa serikali ya tanzania. Naomba tujiulize kwa miaka 50 hiyo rasilimali zetu kama magogo, madini, wanyama kama tembo na faru zitasalimika.
Ni kipi hasa kiliisukuma serikali kuingia mkataba wa kitapeli kama huu? miaka 50 sio midogo, hii itawafanya watanzania wa wakati huo wajute kwanini wamezaliwa Tanzania.
Sielewi uhusiano wa mkataba na uharamia wa magogo, faru, madini n.k uko wapi. Kwani china kutumia bandari maana yake vyombo vya ulinzi vitakwenda likizo? Kama ikitokea magogo na rasilimali zingine vikiibwa tatizo litakuwa serikali na sio mkataba, kwasababu mkataba hauruhusu wizi. na kama wachina watakuwa wanafuata taratibu na kulipa kodi zote inavyotakiwa basi ni swala la kufurahi maana hiyo ndio biashara yenyewe.
 
Haya ndio mambo ambayo yalipashwa kuingia katika katiba hata ya sasa na siyo maandamano yasiyo na mantiki. Nadhani kwa nchi zetu hizi kabla ya kutiwa saini mikopo na mikataba yote iwe inapitiwa na kuidhinishwa na bunge. Hili lingeingizwa katika katiba itakayoendelea kutumika ili tusiendelee kula hasara.
Hueleweki! Hao wanaoandamana si ndio wanaotaka katiba iwekwe sawa? Unaposema "hili lingeingizwa unamwambia nani wakati wanaovuruga rasimu ndio hao unaowatetea?
 
CCM Ni Chama Kilichozeeka Na Kwa Sasa Kinasumbuliwa Na Magonjwa Ya Uzeeni Kama Vile, Pressure, Kisukari, Kuziba Mkojo, Kupoteza Kumbukumbu,n.k., "KIDUMU CHAMA TAWALA"
 
MKATABA HUO WA CCM NA MAFISADI WAKE UNAFANANA NA MIKATABA YA KIKOLONI ILIYOSAINIWA NA MACHIEF WA JADI AKINA MANGUNGO, KIMWERI NA KINJEKITILE NGWALE ENZI ZA UKOLONI. Magamba Tokaaaaaa, Kwa Jina La Bwana Magamba Tokaaaaaaa, Kwa Jina La Bwana Nasema CCM Tokaaaaaaa, Tokaaaaaaa "?X!@.net
\%#
 
\%. Chama Chakavu Tokaaaaaaaa.
 
Back
Top Bottom