CHAMA CHA MAPINDUZI, ccm itaendelea kudumu kudumu zaidi , ni tofauti na vyama vingine kabisa ambavyo vinapitapita leo mitaani vikiomba kura, ni ukweli usio pingika kwamba vyama hivi vya mlengo wa kushoto hawana sera ambazo wenyeakili wakizisoma zinaweza zikawaingia, sera za wenzetu ni danganya toto kwa maana ya ELIMU BURE, AFYA BURE , SERIKALI YA TANGANYIKA , UFISADI, na mengine mengi ambayo wanayoyajua wao.
wanaposema suala la elimu bure , mimi siwaelewi kabisa maana shabaha yao ya kusema elimu iwe bure sijui wanaitoa wapi labda kwa faida ya wale wasiojua haya mambo ya vyama vingi yalipoletwa na hao wanaitwa mabwana wakubwa yalikuja na misururu ya mambo mengine kama watu wachangie katika elimu, afya, mfumo wa vyama vingi uanzishwe, mashirika yasiyojiweza yabinafsishwe, haya yalikuwa ni matakwa ya wakubwa IMF NA WORLD BANK, sasa sisi kama waTanzania na waafrika kwa ujumla tulikaa nao kwa pamoja na kukubaliana ili mambo hayo hapo juu na mengine yaende kwa kufuata kanuni za nchi husika.
sasa hawa wanaosema elimu bure sijui wanamkakati gani na nchi yetu maana Tanzania kama Jamuhuri ya muungano ni mwanachama wa mashirika hayo hapo juu, sasa wenzetu wanaotaka elimu bure wanataka kutuambia watajitoa huko......? sasa wakijitoa huko tutakuwa mgeni wa nani sisi waTanzania hili sio suala la kubeza hata kidogo au kulifanyia mzaha....mkiamini hivyo itakuja kutugharimu vibaya ndio maana mimi hawa CHADEMA nawaona ni wababaishaji tu, hili la elimu hata nchi kama Marekani wanachangia si hapa kwetu tu ndio maana Rais wao Obama katika kitabu chake cha Audacity of Hope Anaelezea jinsi wamarekani wanavyotaabika usiku na mchana kuhakikisha wanapata kipato kitakacho wafanya wawalipie watoto wao ada za shule na yeye ameingia madarakani na kuliboresha zaidi sio kwamba wasilipe kabisa hapana.
Kadhalika suala la afya duniani kote watu wanachangia ,pia kuna na health care Insurance sembuse linchi kubwa kama Tanzania unaposema afya bure inabidi tukutizame mara mbili au tatu coz it may be ur brain is working unclockwise sorry 4 sying that but dat's is the reality my friends.
Wapinzani katika Tanzania ya leo wanazungumzia SERIKALI YA TANGANYIKA , katika yote hili ndio limenikera sana maana laiti hata mwalimu angekuwepo hai leo suala hili bado angeendelea kulipigia kelele CHADEMA wanataka kuigawa nchi hii ambayo imejizolea heshima kubwa duniani kwa utulivu iliyokuwa nayo, wasisahau miaka ile ya1991,1992 1993,1994, ndani ya CCM kulikuwa na wapuuzi wakilitaka hili lakini kwa uimara wa Mwalimu Nyerere waligonga mwamba na likafa kabisa leo wenzetu hawa wa chadema wanalifanya kama mtaji wa kuombea kura naamini kabisa wameishiwa sera sasa wanataka kutulaghai wananchi......., nawaambia watanzania HATUDANGANYIKI.
CCM chama kikubwa chama dume,dume la mbegu kitaendelea kutawala nchi hii zidi na zaidi
LAMPARD.