engmtolera
JF-Expert Member
- Oct 21, 2010
- 5,150
- 1,437
Mwalimu Mkuu akitoka kwenye ofisi yake
Shule ya Msingi Kitete iliyopo katika kata ya Uchindile, Tarafa ya Mlimba wilayani Kilorombero mkoani Morogoro yenye walimu wawili tu na wanafunzi 29.
Shule ilianzishwa mwaka 1976. Ipo zaidi ya kilomita 150 kutoka Kilombero mkoani Morogoro na kilomita zaidi ya 125 kutoka Mafinga, mkoani Iringa.
Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Idd Mdaba anasema tangu ahamishiwe katika shule hiyo mwaka 2008 kwa ahadi kwamba angehamishiwa shule nyingine baada ya miaka mitatu, amekuwa akifundisha mwenyewe wanafunzi wa madarasa yote yaliyopo katika shule hiyo, Hata hivyo nashukuru mzigo huo umepungua mwezi mmoja tu uliopita baada ya kuletewa mwalimu mwingine mmoja kutoka wilayani Geita , alisema huku Mwalimu huyo Juma Deke akidai kujutia uamuzi wa kuomba uhamisho kutoka Geita ili ahamie mkoani kwake Morogoro kwani hakujua kama angepangiwa shule kama hiyo.
Alisema mbali na shule hiyo kutokuwa na vifaa vya kufundishia na kujifunzia, ofisi ndogo ya mwalimu na madarasa yake matatu yaliyopo, hayajasakafiwa chini na kuta zake, hakuna madirisha na milango na yote kwa ujumla wake yana madawati yasiozidi 20.
Mdaba alisema mazingira hayo yameifanya shule hiyo kukosa wanafunzi wa darasa la kwanza, la tatu na la tano hadi la saba hivi sasa baada ya waliopaswa kuwa wanafunzi wa madarasa hayo kutosajiliwa mwaka wa kwanza wa masomo yao ya darasa la kwanza.
Picha zaidi kuhusu shule hii, tembelea blogu ya Lukwangule (chanzo cha habari na picha ni Frank Leonard).
source: Wavuti - Habari