Miaka 50: Ndivyo tulivyothubutu, kuweza na tutakavyosonga mbele | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Miaka 50: Ndivyo tulivyothubutu, kuweza na tutakavyosonga mbele

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by NewDawnTz, Sep 26, 2011.

 1. NewDawnTz

  NewDawnTz JF-Expert Member

  #1
  Sep 26, 2011
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 1,675
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Ndugu zangu watanzania, napenda mfahamu kuwa nchi yetu tumepiga hatua kwenye maeneo mengi na nitaje machache ambayo kwa miaka hii 50 tumethubutu kuyafanya, tumeweza kuyafanya na tutazidi kuyafanya kwa kasi zaidi..........

  Tumethubutu
  kuwagawa Watanzania kwa dini zao, na kufanya kuwa ndiyo lugha yao na fikra yao

  Tumeweza kwa kiwango kikubwa kwani sasa ndiyo lugha kubwa na hata kupigana na kuchomeana misahafu na makanisa imekuwa kawaida….hakika ni mafanikio

  Tutasonga mbele zaidi kwani it is the best strategy kuongoza kwa "ku-frustrate them to a point they willl not be one and agree"……ni kuwagawa mpaka mgawanyike

  Tumethubutu kuondoa ile misingi ya uhuru kwa kuruhusu kuwa nchi huru kwa kila mtu kufanya lolote atakalo kwa maendeleo ya nchi yetu

  Tumeweza kwani sasa kila mtu ni kambale, unaweza kuja na dege lako ukabeba utakacho na kujiondokea, hakuna shida

  Tutasonga mbele zaidi na hata kama mtu anataka kuwekeza/kubinafsishiwa ikulu aje tu. ni maelewano na naamini hatutashindwana

  Tumethubutu kuua mashirika muhimu katika kuendesha uchumi wa nchi hii na sasa yanaendeshwa kama tutakavyo sio kuendana na mahitaji ya maendeleo ya nchi

  Tumeweza kwani si hata ninyi wenyewe mnaona sasa jamani, tumekula zote za Tanesco na si nyie wenyewe mnajionea na kusikia mara RichardMonduli, mara sijui Duwanzi siji SimbilisiSioni

  Tutazidi kusonga mbele jamani tena zaidi na zaidi

  Tulithubutu kutembeza bakuli kupata angalau kibaba kwa ajili ya watoto pamoja na kupata exposure kubwa zaidi kwenye mataifa mbalimbali, si mnajua tena hatufahamiki jamani?

  Tumeweza kwenye hili kwani ninyi wote ni mashahidi kuwa tumefanikiwa sana hapa, vyandarua vya bure nchi nzima, nimebembea kule sijui ndo mnakuitaje kule, nimepiga foto za nguvu na Campbell yule mwanadada maarufu sana kwa mitindo, si mnajionea wenyewe hata juzi nilikuwa na yule mwimbaji maarufu wa hiphop yipyop yule Thumni kule Marekani…..full exposure na utalii na kujulikana kutaongezeka

  Tutasonga mbele zaidi kwenye eneo hili na ninampango sasa kuhakikisha Napata ma-still picture na maminato mengi zaidi na sasa itakuwa zamu ya kina Jay Zee Jigga, nitakwenda kupiga na Sir Alex Fergie, Prof Wenger e.t.c….angalau exposure zaidi jamani tufahamike zaidi ituletee maendeleo ikiwezekana na misaada zaidi na hasa safari hii nitafurahi kama watagawa pampers kwa kila mtoto chini ya mwaka mmoja kwa kweli…itakuwa jambo jema sana

  Tulithubutu kuhakikisha jesho letu la wananchi, polisi na usalama wa taifa kufanya kazi zao kwa ufanisi zaidi na kuhakikisha usalama wetu unakuwa wa uhakika zaidi

  Tumefanikiwa sana katika hili hasa unapokuja wakati wa uchaguzi kwani kwa ushirikiano wa karibu sana na tume ya uchaguzi ninyi wenyewe mlijionea kwa karibu sana, jeshi la wananchi si mnakumbuka wenyewe walivyofanya kazi nzuri, jeshi la polisi ndio sisemi kabisa maana walinitia rah asana nilipokuwa nawaona wakitembeza vichapo kwa wale "vikokoto" wanaojidai kutaka kugeuka miamba na si mnajua wenye ule usalama ulivyo geuka wa CHICHI-EM?

  Tutasonga mbele zaidi kuhakikisha vyombo vyetu hivi vinaendelea kuhakikisha usalama na uhakika wa CHICHI-EM kuendelea kuwa chama-dola cha nchi hii na juhudi hizi zinaendelezwa

  Mwisho kabisa niseme kuwa Tulithubutu kuhakikisha vijana wetu wanapata elimu bora kabisa, kujaza mashule kila kona ili wapate elimu wote angalau ya kidato cha nne na tuwe na wasomi wengi sana

  Tumeweza kwani naamini ni nchi pekee inayoongoza kwa kuwa na shule nyingi za sekondari, kila kata jamani..hebu pigeni makofi tafadhali….all in all nyie wenyewe si mnajionea elimu bora inavyotolewa? Shule zote zina maabara ya kutosha watoto kujifunzia, kila mtoto anapata elimu ya matumizi ya computer kuendana na utandawazi, waalimu wamejaa mpaka inabidi tugeuze baadhi ya madarasa kuwa ndiyo staff, watoto wanakalia madawati international standard kiasi hamu ya kuja shule inakuwa kubwa sana…si mnaonaga wenyewe jamani hata kwenye TV? Vipi kuhusu mfumo wetu wa elimu jinsi unavyowaanda watoto wetu kuwa na maarifa ya kutosha kutumikia nchio yao? Hakika tumeweza

  Tutasonga mbele zaidi kuhakikisha tunaendelea kuzalisha watoto ambao japo kuwa amemaliza kidato cha nne hajui hata kuandika jina lake…..


  Hakika tumethubutu, tumeweza na tutasonga mbele…hata kama una njaa wakati huu ni uzembe wako na hao vikokoto wasikudanganye kuwa ni serikali; kama huna umeme wakati huu usinilaumu mimi wala serikali yangu maana tumejitahidi sana na sisi sio Mungu kuleta mvua, mlaumu Mungu wenu asieleta mvua; kama mtoto wako haendi shule kusoma anazurura na kupata mimba sio kwa sababu hakuna walimu wa kufundisha mashuleni na hivyo watoto wanazurura bali ni kwa sababu ya viherehere vyao……Kwa kweli tumepiga hatua na tutasonga mbele zaidi
   
Loading...