Miaka 5 ya Wananchi kupambana na Hali zao

Miaka 5 ya Wananchi kupambana na Hali zao

Zitto

Former MP Kigoma Urban
Joined
Mar 2, 2007
Posts
1,562
Reaction score
10,897
ACT Wazalendo na Bajeti za Serikali ya CCM Awamu ya Tano

1. Mwaka 2016 kukiwa na shamra shamra kubwa za Serikali mpya makisio ya Bajeti yaliongezwa kwa 31%, Chama chetu kilipofanya Uchambuzi wa Bajeti ya Kwanza ya Serikali ya Awamu ya Tano tulihitimisha kuwa #TumeanzaVibaya kwani ongezeko hili litakamua Watu na kuumiza Biashara hatimaye Maisha kuwa magumu.

2. Mwaka 2017 Maisha yakawa magumu sana, mzunguko wa Fedha ulishuka kwa sababu ya kasi ya ukuaji wa ‘money supply- M3 kushuka na Mikopo kwa Sekta binafsi kuanguka mpaka ukuaji hasi. Ulikuwa Mwaka wa #VyumaVimekaza kiasi hata sisi kama Chama hatukufanya Mkutano wa kuchambua Bajeti.

3. Mwaka 2018 tulifanya Ziara kwenye mikoa 16 nchini kutembelea Wananchi katika Kata ambazo ACT Wazalendo ilishinda viti vya Madiwani. Tulikuta hali mbaya sana ya Maisha kwani vipato vya wananchi vilikuwa vimeanguka kutoka na masoko ya bidhaa zao kuanguka, mbaazi, dengu, choroko na mazao yote ya mbogamboga. Mikopo kwa Sekta binafsi kutoka taasisi za Fedha iliendelea kuanguka, mabenki kufungwa ama kuunganishwa na biashara nyingi kufungwa. Tulikuwa #TunavunaTulichopanda

4. Mwaka 2019 tulitaraji kuwa Serikali ingefanya mabadiliko katika mfumo wa Bajeti kwani tayari mashirika ya Fedha ya kimataifa yalianza kuona hali mbaya ya Tanzania kiasi cha IMF kukadiria Uchumi kukua kwa 4% tu. Hata hivyo Serikali iliendelea na mambo yake #YaleYale

5. Mwaka 2020 tumevamiwa na Korona. Sekta ambayo ni Kuku anayetaga mayai ya dhahabu, Sekta ya Utalii, imeumia sana na watu zaidi ya laki 5 kupoteza ajira na Makampuni ya Kitalii kuwa kwenye Hatari ya kufilisika. Tulitaraji Bajeti ya Mwaka huu ingekuwa na Hatua mahususi za kuhami maisha ya watu na Uchumi Lakini imekuwa Bajeti inayohitimisha miaka 5 ya Utawala wa CCM, miaka ya #PambanaNaHaliYako
 
Magufuli kafaulu kununua watu wa kumsifia na kuchafua upinzani ila kafeli kwenye kila kitu miradi ya ujezi hajakamilisha hata mmoja uku mikopo tushaanza kulipa,

uchumi mfu yaani budget ya kilimo kwa miaka 5 imetekelezwa kwa 17% serious? kilimo kinachoajiri 80% kinafail kwa 83%

Transparent ovyo kwenye miradi mikubwa ya madini, ununuzi wa ndege na ujenzi! wenzetu wanapiga tu mapambio wakati uyu ndiye rais aliyefail kuzidi wote toka uhuru.
 
Unajua huwa najiuliza ni kipi kinafanya maisha kuwa magumu ? Ni serikali na mfumo wake au kuna sababu nyingine ?

Naona huwa tunajishughulosja sana na matokeo kuliko vyanzo halisi, ila kujua vyanzo halisi vinataka elimu kubwa mno.
 
chanzo kikuu cha umaskini wa nchi hii ni ccm, yaani ccm kuendelea kuongoza nchi hii ni sawa na kuchagua umaskini...tuache kulalama wakuu, ni muda wa kuiondoa ccm madarakani kwa namna yyte ile... biashara haziendi kilimo uzalishaji umeshuka.. yaani kila kitu kishuka...kwnn hawa mashetani waendelee kututia umaskini??....njooni na povu wanaccm hasa wale mnaokula na kulala kwa dada zenu...lkn kwa wanaojitambua njooni mumpinge zitto kwa ushahidi ulioshiba na si blaa blaa tu kisa unaenda choo bila gharama yyte....enyi akina Mgonjwa mtambuka, bia yangu , kipara kipya..USSR.. Yehova .mama ntilie wa kawe.. tafadhari sana msilete ushabiki hata Kama mnakula kwa dada zenyu...stop stop stop [emoji9][emoji9][emoji23]
 
ZITTO HUU NI MWAKA WA NGAPI UNA CHAMA CHAKO LAKINI KIMEKUSHINDA JAPO KUJIPENYEZA ZAIDI KWA WANANCHI? MATOKEO YAKE WEWE UMEKUWA MKUBWA KULIKO CHAMA CHAKO
 
Magufuli kafaulu kununua watu wa kumsifia na kuchafua upinzani ila kafeli kwenye kila kitu miradi ya ujezi hajakamilisha hata mmoja uku mikopo tushaanza kulipa,

uchumi mfu yaani budget ya kilimo kwa miaka 5 imetekelezwa kwa 17% serious? kilimo kinachoajiri 80% kinafail kwa 83%

Transparent ovyo kwenye miradi mikubwa ya madini, ununuzi wa ndege na ujenzi! wenzetu wanapiga tu mapambio wakati uyu ndiye rais aliyefail kuzidi wote toka uhuru.
Angalau amefanikiwa kuhamisha huduma nyingi za kiserikali mkoani Dodoma
 
Moderators tafadhali futa huu uzi ni repetition ya uzi wake wa Jana....
 
Moderators wanazingua sanaa Mbunge Paskali
No tusiitane majina haya, bado it's too early, subiria
  1. Nitangaze nia
  2. Nipitishwe na chama
  3. Niteuliwe na NEC
  4. Nichaguliwe
  5. Niapishwe
Ndipo tuitane majina haya.
P
 
Magufuli kafaulu kununua watu wa kumsifia na kuchafua upinzani ila kafeli kwenye kila kitu miradi ya ujezi hajakamilisha hata mmoja uku mikopo tushaanza kulipa,

uchumi mfu yaani budget ya kilimo kwa miaka 5 imetekelezwa kwa 17% serious? kilimo kinachoajiri 80% kinafail kwa 83%

Transparent ovyo kwenye miradi mikubwa ya madini, ununuzi wa ndege na ujenzi! wenzetu wanapiga tu mapambio wakati uyu ndiye rais aliyefail kuzidi wote toka uhuru.
KILIMO, na bado hujagusa ELIMU.
Watu hawaoni majeraha yanayosababishwa leo, na matokeo yake ujinga mkubwa utakaotuandama kwa miaka mingi ijayo.

Nyimbo za VIWANDA, ni lini mara ya mwisho ulipomsikia akitamka chochote kuhusu viwanda, baada ya zile ngonjera za mwanzo na kumkabidhi Mwijage na vyerehani vyake!

Miaka hii mitano, kuna orodha yoyote ya uwekezaji tunayoweza kuichambua hapa JF, UWEKEZAJI wa ndani, ni miradi ipi; na hao wa nje wapo kweli waliojitokeza ukiacha wale aliokuwa amewaanda Kikwete?

Niseme wazi, bahati yetu ni kwamba Coronavirus huenda akawa na faida kwetu kiaina. Kaweka breki kidogo hata huko kwa wenzetu ambao mikakati yao ni kutufanya sisi tuwe soko.

Baada ya hapa, tusipozinduka, tutadidimia kimoja.
 
No tusiitane majina haya, bado it's too early, subiria
  1. Nitangaze nia
  2. Nipitishwe na chama
  3. Niteuliwe na NEC
  4. Nichaguliwe
  5. Niapishwe
Ndipo tuitane majina haya.
P
Pamoja na kuwa hiyo ndio nia yako baada ya kukosa kuteuliwa kwenye nafasi hata uDC, at least leo umesema kweli ingawa si kosa kuanza kuzoea majina hayo. Mimi binafsi nakutakia mafanikio mema katika jitihada zako za kujiunga na Band Wagon ya kumaliza njaa. Good luck!
 
Mwaka 2016 Zito alisema Magu adhibitiwe nilikuaga sijamwelewa kutokana na dhana ya upya wa serikali nadhani mpaka sasa hivi kama wapo ambao hawajaelewa alichosema Zito mpaka dakika WAPAMBANE NA HALI ZAO.tena wamenyeke hasa in (Magu`s voice) mpaka akili ziwakae sawa.
 
Back
Top Bottom