Joseph ambaye ni mgonjwa amekutwa ameanguka barabarani baada ya kuzidiwa alipokuwa akitoka hospitali. Utamuona kuwa japo amekosa usafiri na mtu wa kumuangalia bado ameanguka akiwa amevaa nguo za kijana akiashiria dole gumba.
Huduma za afya ni tatizo kubwa kwa watanzania wengi na huenda alivaa magwanda haya akifiria kuwa kutakuwa na favour fulani. Ila pia huenda magwanda hayo kwake yalikuwa ni muafaka katika kushine kwa yatakuwa bado mapya baada ya uchaguzi kuisha mwezi mmoja uliopita. Tufanye kazi sasa katika kuboresha huduma za afya na maisha ya watanzania vinginevyo nina hakika huyu bwana Joseph 2015 atakuwa amebadilika na kuwanyima kura waliompatia magwanda haya mwaka huu.
Mkuu nakubalina na wewe kwa 100% ila huduma bora za afya ni sera zinazosimamiwa na vyama. Mfano huduma za dharura kama gari la wagonjwa na huduma ya kwanza pindi mtu kama huyu akianguka basi mara moja First Aid squad wanakuwa wamefika. Pili huyo amenguka njiani kwa kuwa hana pesa ya kukodia taxi ambayo ingemfikisha nyumbani salama. Haya yote yanapaswa kuwa sera za vyama na serikali zinazojadi huduma kwa raia wake zinakuwa na wasiwasi pindi mambo kama haya yakitokea.