Miaka 48 ya JWTZ | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Miaka 48 ya JWTZ

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Moshe Dayan, Aug 31, 2012.

 1. Moshe Dayan

  Moshe Dayan JF-Expert Member

  #1
  Aug 31, 2012
  Joined: Feb 10, 2008
  Messages: 811
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 45
  [​IMG]

  Jeshi la Wananchi wa Tanzania, kesho litatimiza miaka 48 tangu kuanzishwa kwake.

  Ikumbukwe kua JWTZ lilizaliwa baada ya uasi ulotokea January 1964 wa jeshi la kikoloni (Kings African Rifle), chini ya muingereza.

  Madai ya "waasi" yalikuwa kwa ujumla ni kuhusu kupinga uongozi wa kijeshi wa waingereza (nchi tayari ilikuwa huru) maslahi duni na kuboresha mazingira ya kufanyia kazi, mwalimu Nyerere aliona madai yana msingi, na akavunja jeshi la kikoloni na likaundwa jipya ambalo halikua na uongozi wa weupe na hapo ndipo likazaliwa jina la JESHI LA WANANCHI TANZANIA, vuguvugu la uasi lilizuka tena january 1983, makamanda na askari walikua na madai ambayo hata kwangu yalikua ya msingi sana, ila sitapenda kuyazungumzia kwenye mada ya leo.

  Mkuu wa majeshi wa kwanza alikua mkuu sarakikya(alistaafu kama major general) na mkuu wa majeshi saivi ni jenerali davis mwamunyange.

  Jeshi lina kamandi (command) tatu, ila lina matawi makuu matano, nayo ni:
  1. Land forces command
  2. Naval command
  3. Air defence command
  4. Military intelligence
  5. National service (JKT)

  Jeshi limepigana vita nyingi za wazi(all out war-total war) e.g kagera war, comorro na pia covert operations, in mozambique, seychelles (regime change), congo drc, nigeria, etc, pia jeshi limefanya peace-keeping missions, eg darfur, Lebanon, etc

  Vita ambayo inakumbukwa zaidi ni ile ya kagera ambayo chokochoko zilianza mwaka 1972 na ilipofika november 1978 majeshi ya uganda yaliingia tanzania.jeshi lilijipanga vizuri na april mwaka 1979 kampala ilianguka kwa majeshi yetu

  pamoja na mapungufu machache yaliyopo, ningependa wananchi mulitie moyo jeshi letu na kuwa na imani nalo KWANI ILIPOBIDI NA INAPOBIDI JESHI LETU HULINDA MIPAKA YETU NA MAISHA YA MTANZANIA KWA GHARAMA YOYOTE

  Tusahau wachache wanaoharibu sifa ya jeshi ila tuwakumbuke wengi wanaofanya kazi kwa bidii kuitumikia nchi yetu, na tuwakumbuke mashujaa wote waliokufa kwenye mapambano.

  [​IMG]

  "The only easy day was yesterday" uzalendo kwanza, good day!
   
 2. Fyengeresya

  Fyengeresya JF-Expert Member

  #2
  Aug 31, 2012
  Joined: Oct 10, 2011
  Messages: 704
  Likes Received: 160
  Trophy Points: 60
  Ni jambo zuri kuhamasisha suala hili kwani wale ni watoto wetu hata kama wamekosea, ni dada na kaka zetu n.k kazi walizofanya kwa asilimia kubwa karibia mia kabisa ni nzuri sana kuliko mabaya yanayofanywa na jeshi hili ukilinganisha na polisi maana asilimia ya uovu yaweza lingana na uungwana wao.
   
 3. Moshe Dayan

  Moshe Dayan JF-Expert Member

  #3
  Aug 31, 2012
  Joined: Feb 10, 2008
  Messages: 811
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 45
  Ni kweli comrade..., kwenye matukio kama haya ni hekima kukumbuka mazuri ambayo jeshi limeyafanya...,

  pamoja sana,
   
 4. wwww

  wwww JF-Expert Member

  #4
  Aug 31, 2012
  Joined: Mar 20, 2012
  Messages: 350
  Likes Received: 204
  Trophy Points: 60
  Kweli umenikuna sana ndugu yangu kwa uzalendo wako unaouonyesha kwenye Jeshi letu pekee, tena pekee kabisa kwa uzalendo hapa nchini. Kimsingi hili jeshi ni katika majeshi bora hapa Duniani pamoja na zana zao duni walizonazo.

  Mimi kwa akili yangu niliyonayo ukitamka JWTZ mwili unasisimuka kwa vile maisha yangu na watoto wangu nimeyakabidhi kwa hili jeshi. Watoto wangu wanafahamu chombo pekee kwenye nchi hii kinacholinda maisha yetu ni JWTZ na si kingine chochote.

  Kwa hali iliyopo kwenye majeshi mengine kama Polisi, Magereza na Usalama wa Taifa ambayo yamegubikwa na rushwa na uharifu mkubwa dhidi wa wananchi wao ni JWTZ ndiyo nguzo pekee ya watanzania iliyobaki. Kimsingi mimi naliheshimu JWTZ kulipo taasisi yoyote hapa Nchini ikiwa ni pamoja na RAIS.

  Vilevile napenda kuchukua nafasi hii kumpongeza Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange kwa ujasiri alionao katika kulinda wananchi wake ikiwa ni kuboresha maisha ya askari hasa wa ndazi za chini kwenye Mishahara, nyumba za kuishi, usafiri na vifaa vya kutendea kazi (Zana za Kijeshi) ambao wamekuwa katika maisha ya shida kwa muda mrefu sana. Huyu ni Mkuu wa Majeshi wa mfano kabisa hapa nchini kwanza kwa kutojihusha na masuala ya kisiasa na kuwa na msimamo kuhusu maisha ya watanzania.

  Nafahamu vizuri ambavyo amekuwa akishawishiwa kulinda maslahi ya wakubwa lakini amekuwa na msimamo wa kwake kuhusu watanzania na kusimamia hilo.

  Hata hivyo nitakuwa mchoyo wa fadhila nisipowapongeza makamanda wote wa JWTZ kwa kazi nzuri wanazozifanya kwa ajili ya watanzania, ingawa mara nyingi wamekuwa wakibezwa na baadhi ya wananchi wasiokua na uzalendo na nchi na wasiofahamu umuhimu wa Jeshi hilo lakini nawaomba wasife moyo kwani wengi tunawaunga mkono kwa kazi nzuri wanayofanya kwa watanzania.


  JESHI PEKEE LILILOBAKI KWA MASLAHI YA WATANZANIA NI JWTZ NA SI VINGINEVYO.
   
 5. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #5
  Aug 31, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,326
  Likes Received: 1,793
  Trophy Points: 280
  Shin Bet? An Israel trained "katsa"?

  Well, mimi nni mmoja wa vipenzi vya jeshi letu. Nisichoelewa ni kwanini historia yake haiandikwi ikachezewa filamu kama zile za Korea, au Gen. Douglas McArthur, Dwight Eisenhower etc...

  Tukilijua vizuri tutalipenda zaidi. Wengine wanalijua kwasababu ya vipigo wanavyopata wananchi kutoka maeneo mbalimbali.
   
 6. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #6
  Aug 31, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,801
  Trophy Points: 280
  Mkuu, hujataja kuwa majeshi yetu yameshiriki mstari wa mbele kuikomboa msumbiji, angola, namibia, afrika ya kusini n.k

  nampa pongezi za dhati kabisa HASHIM MBITA, ndiye alikuwa akiratibu silaha kuwafikia wapigania uhuru.
  Laiti angekuwa fisadi, angekuwa trilionea leo.
   
 7. Malcom Lumumba

  Malcom Lumumba JF-Expert Member

  #7
  Sep 1, 2012
  Joined: Jul 26, 2012
  Messages: 4,836
  Likes Received: 8,187
  Trophy Points: 280
  hata kama jeshi letu lingekuwa dhaifu kiasi gani ila ndilo lililotuokoa kwenye vita vya Kagera na Rai yangu kwa watanzania wenzangu ni kwamba hakuna jeshi lisilokuwa na mapungufu dunia hii kwanza mengine ndo hayana discipline they only rely in manpower,expenditure and equipments which is good ila sisi tuna- depend on our DO or DIE spirit,.......we don't fight by weapons alone but by heart and determination.
   
 8. A

  Ame JF-Expert Member

  #8
  Sep 1, 2012
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 3,352
  Likes Received: 659
  Trophy Points: 280
  And I have this vague picture in my mind (Bado na meditate niko kwenye hatua yakujiambia pole pole mpaka nikifikia stage ya Hagaah nita roar clearly kutoa spiritual command; Jesus have mercy on me!) ndilo litakalo simamia zoezi la ukombozi hapo mambo yatakapoparanganyika kabisa pale kila fiasadi atakapo nyanyua silaha yake ya mwisho na yenye nguvu (stage ya liwalo na liwe) kumwangamiza fisadi mwenzake ili apate nafasi ya kupenya bila kujua ndiyo hivyo tena mwana si riziki na power has changed hand.......!
   
 9. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #9
  Sep 1, 2012
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Hashim Mbita, kama ambavyo maafisa wengi wa utawala wa awamu ya kwanza walivyokuwa, alikuwa ni mwadilifu sana. Kamanda huyu alikuwa mwandishi wa habari wa Nyerere kwa kipindi fulani, kwa hiyo unaweza kujua alikuwa na akili ya namna gani, ingawa Mkapa naye aliwahi kuwa mwandishi wa habari wa Nyerere.

  Mbita nitamkumbuka sana kwa uongozi wake thabiti huko OAU wakati angali meja wa JWTZ
   
 10. dopamine-B

  dopamine-B Member

  #10
  Sep 1, 2012
  Joined: Sep 1, 2012
  Messages: 18
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 5
  JWTZ,, muulize Idd Amin....
   
 11. gobore

  gobore JF-Expert Member

  #11
  Sep 1, 2012
  Joined: Aug 17, 2009
  Messages: 730
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Naombba nirekebishe hapo, ni kweli jeshi Lina kamandi tatu ila Lina matawi Sita! Umesahau Central Command(NGOME) nayo hua inahesabika Kama tawi la Sita kimuundo
   
 12. S

  Sometimes JF-Expert Member

  #12
  Sep 1, 2012
  Joined: Dec 28, 2010
  Messages: 4,567
  Likes Received: 360
  Trophy Points: 180
  Bravo JWTZ! Najivunia kuwa Mtanzania.
   
 13. malema 1989

  malema 1989 JF-Expert Member

  #13
  Sep 1, 2012
  Joined: Jan 27, 2012
  Messages: 848
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 45
  nawakumbuka sana Jenerali Silas Mayunga, Tumainieli Kiwelu, Mirisho Sarakikya, Abdallah Mohamedi Twalipo, Brigedia Jenerali Moses Nnauye(baba yake na Nape), Jenerali Kimario, Msuya na wengineo wengi kwa utumishi wao uliotukuka ndani ya JWTZ na Tanzania nzima!!
   
 14. Nzenzu

  Nzenzu JF-Expert Member

  #14
  Sep 1, 2012
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 859
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hii post ipo kizalendo sana. Nimeipenda!
   
 15. Nzenzu

  Nzenzu JF-Expert Member

  #15
  Sep 1, 2012
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 859
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  To be honest JWTZ ndio taasisi pekee ambayo haijawa corrupted. Mimi kama kijana wa kitanzania natamani sana kuitumikia, elimu yangu ni ya juu ila uzalendo wangu ni PHD. Taratibu zikoje za kujiunga? Umri? MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU BARIKI JWTZ!
   
 16. Gang Chomba

  Gang Chomba JF-Expert Member

  #16
  Sep 1, 2012
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 8,790
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280

  Pole.
  Unajivunia kuwa Mtanzania wakati Twiga na wanyama wengine wakipandishwa kwenye Ndege na kutokomea umangani, unajivunia kuwa mtanzania wakati watu wanakomba pesa nchini na kwenda kuzificha nje ya nchi kwa maslahi yao na familia zao.

  Nyerere alisema “Siku inakuja ambapo watu watachagua kifo
  kuliko fedheha na ole wao wale watakoiona siku
  hiyo!. Na ole wao wale watakaoifanya siku hiyo
  iepukike''.

  Sasa hiyo siku haiko mbali, na ole wao hao JWTZ wajaribu kuizuia.
   
 17. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #17
  Sep 1, 2012
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Huo utabiri wa mwalimu mbona umeuweka kimafumbo? Funguka zaidi mkuu.
   
 18. tatanyengo

  tatanyengo JF-Expert Member

  #18
  Sep 1, 2012
  Joined: Mar 30, 2011
  Messages: 1,140
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Mambo ya jeshi ni siri. Kumbuka sakata la Meremeta kule kwenye mgodi wa Buhemba-Mara
   
 19. tatanyengo

  tatanyengo JF-Expert Member

  #19
  Sep 1, 2012
  Joined: Mar 30, 2011
  Messages: 1,140
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Umenikumbusha siku moja kuna wananchi walikuwa wanahijiwa huko Tabora wakasema WANAJUTA KUWA WANA-TABORA
   
 20. Moshe Dayan

  Moshe Dayan JF-Expert Member

  #20
  Sep 1, 2012
  Joined: Feb 10, 2008
  Messages: 811
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 45
  Hahaaaa, nimependa post yako, unaonekana unasoma vitabu, kuna mtu alikua anaitwa patton, alikua general wa marekani kipindi cha world war 2, tactics zake za vita za wakati huo hadi leo zinasomwa kwenye vyuo mbali mbali vya kijeshi duniani, alikua maarufu kwa kiko mdomoni all the tym kama winston churchill vile
   
Loading...