Moshe Dayan
JF-Expert Member
- Feb 10, 2008
- 815
- 698
- Thread starter
- #21
Kweli umenikuna sana ndugu yangu kwa uzalendo wako unaouonyesha kwenye Jeshi letu pekee, tena pekee kabisa kwa uzalendo hapa nchini. Kimsingi hili jeshi ni katika majeshi bora hapa Duniani pamoja na zana zao duni walizonazo.
Mimi kwa akili yangu niliyonayo ukitamka JWTZ mwili unasisimuka kwa vile maisha yangu na watoto wangu nimeyakabidhi kwa hili jeshi. Watoto wangu wanafahamu chombo pekee kwenye nchi hii kinacholinda maisha yetu ni JWTZ na si kingine chochote.
Kwa hali iliyopo kwenye majeshi mengine kama Polisi, Magereza na Usalama wa Taifa ambayo yamegubikwa na rushwa na uharifu mkubwa dhidi wa wananchi wao ni JWTZ ndiyo nguzo pekee ya watanzania iliyobaki. Kimsingi mimi naliheshimu JWTZ kulipo taasisi yoyote hapa Nchini ikiwa ni pamoja na RAIS.
Vilevile napenda kuchukua nafasi hii kumpongeza Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange kwa ujasiri alionao katika kulinda wananchi wake ikiwa ni kuboresha maisha ya askari hasa wa ndazi za chini kwenye Mishahara, nyumba za kuishi, usafiri na vifaa vya kutendea kazi (Zana za Kijeshi) ambao wamekuwa katika maisha ya shida kwa muda mrefu sana. Huyu ni Mkuu wa Majeshi wa mfano kabisa hapa nchini kwanza kwa kutojihusha na masuala ya kisiasa na kuwa na msimamo kuhusu maisha ya watanzania.
Nafahamu vizuri ambavyo amekuwa akishawishiwa kulinda maslahi ya wakubwa lakini amekuwa na msimamo wa kwake kuhusu watanzania na kusimamia hilo.
Hata hivyo nitakuwa mchoyo wa fadhila nisipowapongeza makamanda wote wa JWTZ kwa kazi nzuri wanazozifanya kwa ajili ya watanzania, ingawa mara nyingi wamekuwa wakibezwa na baadhi ya wananchi wasiokua na uzalendo na nchi na wasiofahamu umuhimu wa Jeshi hilo lakini nawaomba wasife moyo kwani wengi tunawaunga mkono kwa kazi nzuri wanayofanya kwa watanzania.
JESHI PEKEE LILILOBAKI KWA MASLAHI YA WATANZANIA NI JWTZ NA SI VINGINEVYO.
spot on! U understand comrade!