Miaka 42 bila ya Steve Biko aliyefariki mikononi mwa Polisi wa kikaburu huko Afrika Kusini

Konzo Ikweta

JF-Expert Member
Oct 3, 2013
735
1,464
Francis Daudi,

Leo Septemba 12, Dunia inamkumbuka Stephen Bantu Biko ambaye alikuwa mwanaharakati mashuhuri wa Afrika aliyefariki mikononi mwa polisi wa kikaburu huko Afrika Kusini miaka 42 ililiyopita.

Biko au Bhiko anachukuliwa kama mfano sawia wa mwanaharakati, Mzalendo na Mmajumui kijana wa Afrika. Yajue mambo muhimu juu ya maisha ya Steve au Stephen aliyefariki akiwa na miaka 30 tu.

1. Alizaliwa Disemba 18, 1946(Leo angekuwa hai angeweza kuwa na miaka 73) katika eneo la Tylden, mji wa Eastern Cape. Baba yake kwa jina Mzingayi Mathew Biko alikuwa karani wa serikali na mama yake ni Alice Nokuzola “Mamcethe” Biko.

2. Steve alifukuzwa shuleni akiwa na kaka yake aliyeitwa Khaya kwa makosa ya kujihusisha na masuala ya kisiasa. Alienda Natal na kumaliza masomo yake kisha kujiunga na Chuo kikuu cha Natal kwenye shule ya udaktari(University of Natal Medical School) akiwa hapo chuoni alianzisha vuguvugu la Black Consciousness Movement, akilenga kuinua hali ya mtu mweusi na kupinga ubaguzi wa rangi ulioongozwa na serikali ya kikaburu. Mwaka 1972 alifukuzwa chuo kisha serikali ikampiga marufuku kukusanyika na watu, haitoshi ikazuia machapisho yake katika vyombo vya habari.

3. Biko alilazimishwa kurudi kwao, huko aliendeleza harakati za chini chini na vuguvugu lake la Black Consciousness Movement lilipelekea wanafunzi 20000 kuingia katika maandamano ya Soweto mwaka 1976 ambapo wanafunzi 176 waliuliwa na polisi wa kikaburu.

4. Mwezi Agosti 18, 1977 alikamatwa kwa kuhusishwa na ‘Ugaidi’ na matukio mengine yaliyotishia utawala wa kikaburu. Alipelekwa Port Elizabeth kufanyiwa mahojiano ya ‘kipelelezi’.

Inaelezwa wakati wa ‘KUHOJIWA’ alipata majeraha makubwa kichwani. Hali yake ilipokuwa mbaya alifungwa minyororo akiwa uchi na kupelekwa hospitali ya kipolisi katika mji wa Pretoria yapata maili 700. Alifariki dunia akiwa sakafuni tarehe 12 Septemba 1977(tarehe na Mwezi kama wa Leo).

5. Mwaka 1978 kesi iliyofunguliwa na wanaharakati ilinguruma kwa siku 15 tu kisha mahakama ikaeleza hakuna ushaidi wa Bhiko kuuliwa, mwaka 1997 mmoja kati ya polisi waliohusika alitoa ushuhuda kuwa, Steve alipokuwa akiojiwa alifungwa kwa minyororo kwa saa24 akiojiwa na aliachiliwa kichwa chini miguu juu kisha kujipigiza kichwani. Familia ya Biko ililipwa fidia ya 65,000 rand( takribani shilingi 10,049,706 za Tanzania).

6. Biko alifariki akiwa amemuoa Bi Ntsiki Mashalaba waliyezaa watoto wawili na pia alikuwa na mahusiano na Dr. Mamphela Ramphele mwanaharakati mwenzake aliyeachwa na ujauzito. Lakini pia Biko alikuwa na mahusiano na wanawake wengine wawili aliozaa nao mtoto mmoja kila mmoja.

Hivyo basi Biko alijaaliwa watoto 5 tu katika maisha yake ya miaka 30 hapa Ulimwenguni.

7. Mwisho, alizikwa katika mji Eastern Cape kwenye bustani maarufu ya Stephen Biko, Na maandiko yake mengi yalichapishwa katika kitabu I Write What I Like na kuna filamu inaeleza maisha yake inayoitwa Cry Freedom.

Leo ni miaka 42 ya kumbukumbu ya mtu aliyejitolea maisha yake katika kuinua hali ya mtu mweusi. Nilipokuwa Namibia, nilikutana Bavelile, yeye ni mjumbe wa vijana wa ANC toka Eastern Cape(Kwa sasa Naibu Waziri, Wizara ya Nishati na Madini), nikamuuliza kuhusu Biko, akaniambia Biko bado anaishi. Mapambano yanaendelea dhidi ya vizazi vya makaburu ili kurudisha ardhi kwa Waafrika kwani ulikuwa ni Unyang'anyi.

Karibu katika page hii

Asante sana.

Francis Daudi
+255768035253
 
Juzi kwenye disco DJ mmoja akajichanganya akaweka nyimbo ya SA aisee nusura wamtoe kizazi, sasa sijui wewe watakufanya nini hapa baada ya watu kuona na kujua tabia za SA
 
Mkuu, Steven Biko alikuwa mwana harakati katika kupigania Uhuru wa mtu mweusi dhidi ya serikali ya kibaguzi na makaburu wa SA.
Lakini leo Zulu's are fighting against black foreigners kwasababu tu wao hawana kazi ama hawaja fanikiwa. Na hapo issue kunwa ni hawa black SA's ni wavivu wa kupindukia na wapenda ngono pamoja na kulewa masaa mengi kuliko kufanya kazi.
 
Francis Daudi,

Leo Septemba 12, Dunia inamkumbuka Stephen Bantu Biko ambaye alikuwa mwanaharakati mashuhuri wa Afrika aliyefariki mikononi mwa polisi wa kikaburu huko Afrika Kusini miaka 42 ililiyopita.

Biko au Bhiko anachukuliwa kama mfano sawia wa mwanaharakati, Mzalendo na Mmajumui kijana wa Afrika. Yajue mambo muhimu juu ya maisha ya Steve au Stephen aliyefariki akiwa na miaka 30 tu.

1. Alizaliwa Disemba 18, 1946(Leo angekuwa hai angeweza kuwa na miaka 73) katika eneo la Tylden, mji wa Eastern Cape. Baba yake kwa jina Mzingayi Mathew Biko alikuwa karani wa serikali na mama yake ni Alice Nokuzola “Mamcethe” Biko.

2. Steve alifukuzwa shuleni akiwa na kaka yake aliyeitwa Khaya kwa makosa ya kujihusisha na masuala ya kisiasa. Alienda Natal na kumaliza masomo yake kisha kujiunga na Chuo kikuu cha Natal kwenye shule ya udaktari(University of Natal Medical School) akiwa hapo chuoni alianzisha vuguvugu la Black Consciousness Movement, akilenga kuinua hali ya mtu mweusi na kupinga ubaguzi wa rangi ulioongozwa na serikali ya kikaburu. Mwaka 1972 alifukuzwa chuo kisha serikali ikampiga marufuku kukusanyika na watu, haitoshi ikazuia machapisho yake katika vyombo vya habari.

3. Biko alilazimishwa kurudi kwao, huko aliendeleza harakati za chini chini na vuguvugu lake la Black Consciousness Movement lilipelekea wanafunzi 20000 kuingia katika maandamano ya Soweto mwaka 1976 ambapo wanafunzi 176 waliuliwa na polisi wa kikaburu.

4. Mwezi Agosti 18, 1977 alikamatwa kwa kuhusishwa na ‘Ugaidi’ na matukio mengine yaliyotishia utawala wa kikaburu. Alipelekwa Port Elizabeth kufanyiwa mahojiano ya ‘kipelelezi’.

Inaelezwa wakati wa ‘KUHOJIWA’ alipata majeraha makubwa kichwani. Hali yake ilipokuwa mbaya alifungwa minyororo akiwa uchi na kupelekwa hospitali ya kipolisi katika mji wa Pretoria yapata maili 700. Alifariki dunia akiwa sakafuni tarehe 12 Septemba 1977(tarehe na Mwezi kama wa Leo).

5. Mwaka 1978 kesi iliyofunguliwa na wanaharakati ilinguruma kwa siku 15 tu kisha mahakama ikaeleza hakuna ushaidi wa Bhiko kuuliwa, mwaka 1997 mmoja kati ya polisi waliohusika alitoa ushuhuda kuwa, Steve alipokuwa akiojiwa alifungwa kwa minyororo kwa saa24 akiojiwa na aliachiliwa kichwa chini miguu juu kisha kujipigiza kichwani. Familia ya Biko ililipwa fidia ya 65,000 rand( takribani shilingi 10,049,706 za Tanzania).

6. Biko alifariki akiwa amemuoa Bi Ntsiki Mashalaba waliyezaa watoto wawili na pia alikuwa na mahusiano na Dr. Mamphela Ramphele mwanaharakati mwenzake aliyeachwa na ujauzito. Lakini pia Biko alikuwa na mahusiano na wanawake wengine wawili aliozaa nao mtoto mmoja kila mmoja.

Hivyo basi Biko alijaaliwa watoto 5 tu katika maisha yake ya miaka 30 hapa Ulimwenguni.

7. Mwisho, alizikwa katika mji Eastern Cape kwenye bustani maarufu ya Stephen Biko, Na maandiko yake mengi yalichapishwa katika kitabu I Write What I Like na kuna filamu inaeleza maisha yake inayoitwa Cry Freedom.

Leo ni miaka 42 ya kumbukumbu ya mtu aliyejitolea maisha yake katika kuinua hali ya mtu mweusi. Nilipokuwa Namibia, nilikutana Bavelile, yeye ni mjumbe wa vijana wa ANC toka Eastern Cape(Kwa sasa Naibu Waziri, Wizara ya Nishati na Madini), nikamuuliza kuhusu Biko, akaniambia Biko bado anaishi. Mapambano yanaendelea dhidi ya vizazi vya makaburu ili kurudisha ardhi kwa Waafrika kwani ulikuwa ni Unyang'anyi.

Karibu katika page hii

Asante sana.

Francis Daudi
+255768035253
Asante sana Mdau, Kuna sehemu nilikiona kitabu chake.
 
wa
Juzi kwenye disco DJ mmoja akajichanganya akaweka nyimbo ya SA aisee nusura wamtoe kizazi, sasa sijui wewe watakufanya nini hapa baada ya watu kuona na kujua tabia za SA
ngekipataje kizazi huko chini mbali kabisa,

hhivi kwa nini walikimbilia kizazi badala ya mikono
 
Back
Top Bottom