Miaka 35-55 inaweza kuwa ya kutisha kwa wanaume. Kitumie vizuri kipindi cha miaka 20-35

Miaka 35-55 inaweza kuwa ya kutisha kwa wanaume. Kitumie vizuri kipindi cha miaka 20-35

Duh miaka 35 mbona mtu mdogo sana ndio kwanza anapaswa kuanza kuoa.

Mimi kaka angu pamoja na kuwa na akili sana darasani, amesota (sio per-se) ila ile potential yake alikuwa hajaifikia. Kuanzia 35 ndio mambo yakaanza kunyooka baada ya kuondoka kwenda nje.

Now he’s 37 mambo ni mazuri hadi yeye anakiri.

Mwaka mmoja au miezi kadhaa inaweza kutosha kufukia mashimo ya makosa, kikubwa ni lazima kufanya kitu tofauti na ulivyokuwa unafanya kawaida.

Badala ya kutishana hebu tutiane moyo wakuu.
NAONDOKA NA HII ✅
 
Kumwamini Mwenyezi Mungu, na kufanya ayatakayo na kuacha asiyoyataka kutakuwezesha kuwa na Afya njema, Uzima na Maarifa ya kuweza kukufanikisha katika Maisha

Kama alivyosema Binti mmoja hapo juu kuwa siku 1 au wiki moja inaweza kubadilisha Destiny ya Mtu

Ukijudge sana Umri utaweza kukata tamaa na kupoteza Patience ilihali Nature na Mazingira yetu ya maisha ndio yanayochelewesha watu kufikia malengo kwa kukosa fursa.
Namimi nimependa ushauri wake ✅
 
Sio kutishana lazima tukumbushane
Uko sahihi, lakini kuna sababu ya kwanini si kila mtu alipaswa kuwa mwalimu/mtoa ushauri/mentor etc.


Our sense of reality ina tofautiana kulingana na background zetu. Kikubwa wote tunaishi na kila mtu anajitahidi kufikia malengo yake. Au wenzetu malengo yenu ni mamoja?

Anyways it was men’s parade and i am here raining. 😀
 
Mimi nikiwa middle 20's ndipo niligundua mimi kama mwanaume nipo peke angu hapa duniani. Hakuna mtu anaekuja kunikomboa. Nilipambana hapo kati sasa hivi nipo early 30's angalao upepo umetulia lakini bado najutia miaka niliyoipoteza kule kwenye early 20's. Ningeshyuka mapema sasa hivi ningekua nipo hatua za mbele zaidi kimaisha.

Kuna dogo moja hivi ni mtoto wa marehemu kaka angu. Baada ya bro kufariki niliachiwa jukumu la malezi ya huyu dogo. Ndio anaingia form 4 mwaka huu. Wakati wa likizo akiwa hapa home siku nzima anashinda anacheza cheza tu hii miziki ya bongo fleva, na fasheni zao hizi za tshirt na jeans oversize halafu chini sendozi zina soli kubwa. Huwa namwangalia nasema angejua dunia inayomsubiri mtaani huyu..., ila ngoja amalizie utoto kwanza. Akimaliza form 6 naanza kumpa nondo.
Six mbali mno mkuu, akifika hadi huko atakua corrupted vya kutosha.

Umri aliopo ndio umri wa kuharibika gambe, ganja, porn & bakari nondo😄

Anza kumpandikiza 'chuki' now, mdomdo zitamwingia, hadi ile anaenda chuo anakua anajitambua.

Ikiwezekana hakikisha unamtolea copy kila bandiko lako la humu achimbe msuli 😊
 
Ukianza kupoteza wazazi au walezi ndo akiri itaanza kuamka na utatambua kuwa umekuwa .
Kuna wakati unapata changamoto na unakuwa unahitaji japo ushauri tu wa wazee lakini unagundua walio kuwa wanakupa ushauri konki haupo nao tena .

R. I. P my lovely uncle
 
Duh miaka 35 mbona mtu mdogo sana ndio kwanza anapaswa kuanza kuoa.

Mimi kaka angu pamoja na kuwa na akili sana darasani, amesota (sio per-se) ila ile potential yake alikuwa hajaifikia. Kuanzia 35 ndio mambo yakaanza kunyooka baada ya kuondoka kwenda nje.

Now he’s 37 mambo ni mazuri hadi yeye anakiri.

Mwaka mmoja au miezi kadhaa inaweza kutosha kufukia mashimo ya makosa, kikubwa ni lazima kufanya kitu tofauti na ulivyokuwa unafanya kawaida.

Badala ya kutishana hebu tutiane moyo wakuu.
Aaah binti tena.! Haya bwana.
 
Ila humu ndani mnapenda kutisha watu sanaaa na mabandiko yenu ya ajabu ajabu

Mzee wangu alikua mwanariadha na mchezaji mpira sasa kuna picha iyo inaonesha timu yao wakichungua ubingwa nikamuuliza vipi hawa wenzako wapo ? Akanambia wapo hao sijasikia kufa yeyote yule kati yetu
 
Wapo waliokufa hata miaka 20 hawajafikisha,kuishi ni zawadi hata mali ambazo unahisi zitakusaidia zinaweza zikaisha zote na ukabaki mikono mitupu,kuna mzee ujana wake wote alikuwa jela kwa miaka 20 alikuja kutoka ni miaka 45 na sasa tunavyozungumza ana miaka 73 ni tajiri haswa
 
35-55 ni kipindi cha kutisha kwa wanaume wengi

Unagundua:

  • Marafiki wako wa karibu wanakuwa wako busy na familia zao

  • Marafiki zako wengine wameshakata tamaa na maisha hawaoni kutoboa life tena

  • Kama sio wewe basi utasikia watu wa rika lako wakianza kuugua magonjwa ya kudumu kama kansa, kisukari, high blood pressure n.k

  • Habari za vifo na ajali za kuwapoteza wenzako

  • Wazazi na ndugu zako wa karibu wa ukoo na washauri wako wanaanza kuhangaika na afya zao kwa sababu ya umri kusonga na hata kuwapoteza

  • Upande fulani hata wewe unaanza kuona nguvu zako za ujana zikizidi kupungua kila siku

  • Huenda first born wako anakaribia kuoa au kuolewa na bahati mbaya unaweza kupata kijana wako au binti hajielewi teja, jizi, malaya n.k

  • Marafiki zako wanaanza kufa kutokana na masuala ya afya

  • Baadhi ya watu uliowaheshimu huanguka kwenye ulevi na dawa za kulevya

  • Unatambua wewe na mkeo mnaishi tu ili mradi siku ziende

  • Unatambua jinsi watu wengi wa rika lako mlivyo frustrated sana na maisha na majukumu ya kifamilia na watu wa karibu

  • Ikiwa haujawekeza au kujipanga kwa chochote, unaanza kuhisi kama umeshindwa maisha.

35-55 sio kipindi rahisi kwa wanaume wengi.

Unaanza kukumbuka umuhimu wa kukitumia vizuri sana kipindi cha miaka 20-35 kujenga future kabla ya midlife crisis (40-60)
Ni kweli umeyasema haya nipo 35 eeh bwana kuna presha isiyo ya kawaida huku juu.. unatamani uombee poo ila ndio hivyo haiwezekani..alafu ndio kwanza naanza 35 sijui maulana akijaalia nikifika 50 itakuwaje naomba iwe kheri daima..
 
Miaka 35 sio mtu mdogo, hasa kwa lifespan tuliyonayo.

Bahati mbaya sana mfumo wa maisha ya mtanzania unamchelewesha mtu kufikia malengo yake mapema ila 35 ni mtu mzima ambaye anatakiwa kuwa na vijana wadogo wanaoenda shule(junior schools), ameshatulia kwenye career yake, kijamii pia ametulia. Kama kuna makosa badi 35-45 ndio wakati wa kurekebisha maana baada ya hapo hakuna reverse mode tena.

Tuliochelewa kuoa tukiwa na 30+ tuna testimonies za kutosha.
Ka mkubwa nili dhani wewe ni team kataa ndoa 😁
 
Ni kweli umeyasema haya nipo 35 eeh bwana kunanpreshabisiyo ya kawaida huku juu.. unatamani uombee poo ila ndio hivyo haiwezekani..alafu neio kwanza naanza 35 sijui maulana akijaalia nikifika 50 itakuwaje naoma iwe kheri daima..
Ina presha sana maana wengi umri huo 35 wanakuwa na tegemezi kama sio familia yake mwenyewe basi watu wa karibu na muda huo na wewe unataka kuweka mambo yako sawa

Ndani ya miaka 10 kuanzia sasa kufika 45:

Usisahau kujiwekea malengo ya muda mfupi kama ya mwaka 1 au 2 na ya muda mrefu miaka 5 hadi 10 focus humo

Pia mtangulize sana Mungu tunza afya yako ishi na watu vizuri

Hakikisha family comes first kama unayo
 
Kila mwanadamu ana hatma yake na kamwe hazilingani wala fanana hata siku moja. Ukifwatilia jinsi jamii inavyo tafsiri au amini swala Zima la mafanikio na umri utakufa na stress siku si zako au kujihumu sivyo na kumkosea Muumba ingawa si vibaya kukumbusha kuhusu majukumu kulingana na nyakati husika.
 
Bonge la uzi kwangu binafsi kufungulia 2026.. uzi umenifanya ni log in tena baada ya kamuda kidogo, shukrani mtoa mada. Pepo la mafegi tokaaa utokomee, Amen.
 
Back
Top Bottom