Miaka 32 ya CCM - Upinzani wa Kweli "utatoka" CCM!

Unaizungumziaje kauli hii ya Baba wa taifa Mwalimu J.K Nyerere aliyoitoa mnamo mwaka 1994.!

Je si Mwalimu aliyeanzisha Azimio la Arusha na leo liko wapi? Si Nyerere aliyeanzisha viwanda hasa Textiles leo ziko wapi? Si Nyerere aliyeanzisha JKT na wakaiua hao wanakufundisha kutumia mstari mmoja Kabla ya kauli hiyo, Je si Mwalimu aliyepiga vita rushwa, ufisadi na uhujumu Uchumi wakati wa Waziri Mkuu Marehemu Sokoinne? Je ebu tiririka utwambie pale ambapo Mwalimu alibariki Ufisadi, Rushwa, Madawa ya Kulevya na ugawaji holela wa raslimali za taifa kwa akina Bush, Obama na Clinto pamoja na Wachina?

Ndugu yangu acheni mchezo wa kupokea buku 7 toka Lumumba Project.
Mwalimu alisema "Watanzania wanataka Mabadiliko, wasipoyapata ndani ya CCM, Watayatafuta hata nje ya CCM"
 
Wapinzan hata wazikiri uchi hawawezi pata hii nchi kamwe ccm ikipasuka upinzani utapatikana nchini
 
"Ufalme hauwezi kufitini ufalme wake mwenyewe na Shetani hawezi kujipinga". Hayo maneno yaliwahi kusemwa miaka 2000 iliyopita na myahudi mmoja aitwaye Yesu, sijui Nyerere alikuwa hasomi Biblia?
 
Nchi haichukuliwi kwa kuzikiri kama CCM wanavyodanganywa na akina Maji Mafupi.
Hoja ndiyo kitu pekee kiwezacho kuwapa nguvu ya kutwaa Dola.
Hapo CHADEMA ilipofikia imefika kwa sababu ya kujenga hoja na si kuzikiri.

Tatizo kubwa linao wakabili wananchi wengi nchini Tanzania ni kushindwa kuunganisha matatizo yao yote yanayowakabiri na historia ya utendaji wa CCM.
Kwa mfano;
Ugomvi wa ardhi kati ya wawekezaji na wananchi, wananchi wengi wanauona ni kati yao na wawekezaji. Lakini ukweli wenyewe ni kwamba CCM ndo imeochestrate ugomvi huo.

Wewe mpaka leo bado wananchi wanalazimishwa kuchangia kukimbuza mwenge,lile nyamkera la CCM uchawi wa mizimu ya akina Nyerere. Wanauita alama ya Taifa wakati Materorist(GREENGADI) wa CCM ndo wanaoukimbiza huku wanajeshi w JWTZ ambao nao siku hizi ni Tawi la CCM na Lupango ya kutesea mashujaa wanaMtwara, wakibabatizwa kwa mbali.

Kwa mwananchi anayetafunwa machana na usiku'
Mazoea ya kuishi kwa maumivu makali, mazoea ya kuishi maisha nusu, mazoea ya kutii bila kudadisi na kuamini kila kisemwacho na kila kiongozi wa serikali CCM; aidha,Udumavu wa uwezo wa kuchambua na kutafakari matukio,hoja na historia nzima ya utawala wa CCM na matukio ya hivi karibuni ya CCM kulala kitanda kimoja na kufanya UZINZI na kila mwenye POCHI, huku sehemu ndogo sana ya wananchi wanaojiona wajanja
wakifaidi kutoka kwa kila kinachodondoka kutoka kwenye kitanda cha uzinzi wa CCM, ndo kiini haswa cha hoja za kudhani CCM itaendelea kutawala hata ikiwa kuzimu.

Wapinzan hata wazikiri uchi hawawezi pata hii nchi kamwe ccm ikipasuka upinzani utapatikana nchini
 
Upinzani wa ukweli utatoka CCM kama huu uvumi unao endelea ukawa ni ukweli
Lowasa akichomoka CCM kwenda ukawa kupitia chama chochote atapata sapoti kubwa sana kutoka ndani ya ccm hivyo ataondoka na wajumbe wengi sana na hii inawezekana hata baadhi ya wajumbe wa kamati kuu.
na CCM inaweza jikuta ndo chama pinzani.
Na hawa UKAWA wakijionga force na kuweza unda serikali CCM kurudi madarakani itakuwa ni historia

Huu ni mtazamo tuu
 
Kwa mujibu wa falsafa za Hayati Mwl. JK Nyerere, upinzani wa kweli utatokea ccm; Haikosi kwa maneno haya alimaanisha kwamba watakaoingia upinzani kwa wingi tokea ccm watauimarisha na kuupa nguvu. Hilo hufanywa na watu madhuti na sio wababaishaji au oili chafu kama tunavyotaka kuaminishwa. Mwl. hakusema makapi yatatoka ccm kuja upinzani bali wajenzi imara wa demokrasia ya kweli watatua upinzani na kuupa mwanzo mpya. Siku zote alionyesha kuichoka na kukerwa na ccm kama chama kinachonuka rushwa na kilichopoteza uelekeo na kutamani ipasuke vipande vipande watu watoke waende upinzani upatikane mwanga mpya. Sina hakika sana kama alimaanisha pia kwamba upinzani utachukua dola mara moja lakini ni wazi badiliko hilo ni taraja la kuleta uwiano wa kisiasa ndani ya nchi na kuondoa hodhi ya chama kimoja katika kuamua mustakabali wa nchi; wapinzani watapata madiwani zaidi, wabunge na hivyo kuwa sehemu kuu katika maamuzi muhimu ya nchi. Mimi binafsi sina chama cha siasa na kiujumla bado sijaona siasa za kufaa ndani ya nchi; hatuna dira ya taifa, vipaumbele wala maadili ya uongozi. Saisa bila nguzo hizi tatu katika katiba ya nchi ni vurugu mechi tu; hata akipatikana kiongozi msafi kiasi gani pale Ikulu bado ni shida tu, hakuna cha kumdhibiti asigeuke fisadi akiwa pale. Kwa maneno mengine, pamoja na nguvu ya upinzani kuongezeka bado hatujihakikishii jambo la maana sana katika mustakabali wa nchi yetu; wala haijalishi sana nani anakuja madarakani iwe upinzani au wabakie haohao mambo yatakuwa yaleyale tu; ni mvinyo uleule kwenye viriba vipya. Hata hivyo yafaa tusipuuze kabisa kejeli za oili chafu na makapi kwani ni heri nusu shari kuliko shari kamili. Haidhuru viriba vimekuwa vipya.
 
upinzani wa kweli utatoka ccm ...sasa yametimia, kadi no 6 imeondoka

mawazo ya watu yaheshimiwe...ccm walishindwa kuheshimu mawazo ya watu..ndo maana toka nadhaliwa na kukua sijawahi ona rais anampigia kampeni mgombea wa urais... sasa tunaambiwa ccm wote wako kwenye kampani pamoja na jk.

chama kinachoweza kuwa mbadala wa ccm ni chadema... hili ndo linakuja

ccm wanawaogopesha watz kuwa bila wao hakuna amani...hahaha wapi mpanga mipango miovu mwigulu

kama mwl hakusema haya nipinge hapa
 
Back
Top Bottom