Miaka 30 jela: Je, ni suluhisho ama mateso kwa familia? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Miaka 30 jela: Je, ni suluhisho ama mateso kwa familia?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by n00b, Oct 13, 2009.

 1. n00b

  n00b JF-Expert Member

  #1
  Oct 13, 2009
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 952
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 60
  Kuna mdau aliianzisha hii hoja (naomba ajitokeze ili credits ziende kwake) hivyo naiweka kama alivyoibandika:

  ====================

  Ndugu wana jamii, salamu kwenu nyote mlio kwenye jamvi hili la sheria.
  Leo nimepata kisa ambacho ningependa nikilete hapa kwenye kisima cha taaluma ili nisaidiwe na kama ikiwezekana jamii isaidiwe.

  Kuna sheria inayoruhusu mtu kufungwa miaka thelathini jela kwa kosa la kumpa mimba mwanafunzi. Mimi sipingi ila nataka mnijuze kama hilo limetosha kuondoa tatizo la mimba shuleni ama limeleta matatizo kwa familia. Kisa chenyewe nilichokutana nacho ni cha binti mmoja ambaye nilikutana naye kwenye moja ya miji yetu mashuhuri. Nikiwa nimekaa na rafiki zangu kwa ajili ya kujadili kitu kilichotupeleka hapo alikuja binti huyo na kutusalimu na kisha aliomba kama tunaweza kumsaidia kinywaji.

  Hilo halikutupa shida kwani vinywaji vyenyewe tunavyokunywa ni non-alcoholic kwa hiyo mimi binafsi nilimwambia muhudumu ampe soda anayopenda. Yeye aliguna na kuomba apewe bia kwani si mtoto wa shule (ingawa umri wake ni wa mtu wa shule hata kama ni A-level). Mimi nilikataa kwamba siwezi kulipia bia kwa kuwa siungani na unywaji wa alcohol. Kauli alizotoa hapo zilinisukuma kutaka kudadisi ni shida gani ilikuwa moyoni mwake. Nikahisi kuwa atakuwa na msongo mkubwa wa mawazo unaomfanya kuwa hivyo.

  Tuliongea mambo mengi katika kumdadisi ila kwa kifupi nikupe maelezo aliyonipa na ambayo yamenisukuma kutoa kisa hiki.

  Yeye akiwa kidato cha pili alikuwa akisumbuliwa na mwalimu mmoja aliyekuwa katoka chuo cha ualimu kumtaka awe mpenzi wake na yeye hakupendezwa na mwalimu huyo (yaani, naturally hakuwa anamkubali mwalimu huyo). Basi mwalimu huyo alitumia mbinu alizozifahamu kumshawishi ikiwa ni pamoja na kumuahidi ndoa lakini binti hakuvutiwa.

  Baadae mwalimu alimtuma nyumbani kwake kumchukulia vitabu na hapo ndipo alimfuata kwa nyuma na kufanikiwa kumbaka. Siku hiyo ya kwanza ilikuwa mbaya sana kwa binti lakini baadae alijifunza kuzoea na ukabaki ni mchezo wa kawaida mpaka ilipogundulika kuwa binti ana mimba.
  Walifikiria kuitoa mimba lakini kukawa na hofu ya kufa na pia mwalimu akaomba tu amuoe binti lakini familia ya binti na hasa baba (ambaye ni askari) ilikataa na kumburuza mahakamani ili iwe fundisho kwa wakware wengine.

  Mahakama iliamua kumhukumu mtuhumiwa miaka 30 jela kwa kosa hilo alilofanya ingawa yeye alikuwa radhi kulea mama na mtoto ikiwa mahakama itamuweka huru. Huyo jamaa akaelelekea jela baada ya kama mwaka mmoja wa kazi yake huku mwanafunzi akikatiza masomo kwa ajili ya kulea mimba.

  Binti kurudi nyumbani baba yake akamwambia hataki kumuona hapo nyumbani kwake vinginevyo atamchinja. Naye kwa kujua ukali wa baba yake aliamua kukimbilia kwa shangazi yake ambapo alibahatika kujifungua mtoto wa kike. Hali ya maisha haikuwa nzuri kwa kuwa hakuwa na chanzo cha kipato na hivyo kufikiria kwenda popote kutafuta maisha. Binti akawa ameenda kwenye mkoa mwingine na huko akapata rafiki ambaye alijikuta akimtubukiza kwenye biashara ya ukahaba.

  Kwa hiyo kiufupi huyo binti analea huyo mtoto wake kwa kuuza mwili wake kwa wanaume huku baba wa mtoto huyo akisota gerezani huku akisubiri msamaha wa rais.

  Mimi binafsi hali ya maisha ya binti huyo iliniuma sana na nikajiuliza hivi kuna mabinti wangapi wanaojiuza kwa sababu wamekutana na mazingira kama hayo?

  Je, kama huyo mama akipata UKIMWI na kufa huyo mtoto atalelewa na nani?

  Je, ni watoto wangapi wanabaki wakiteseka kisa baba yao amefungwa miaka 30 kwa kuzaa na mwanafunzi ambaye ndo mama yao?

  Je, kifungo cha miaka 30 kinaisaidia nchi ama kinaongeza mzigo kwa jamii na taifa?

  Suluhisho iwe nini basi ili kuwe na mutual benefit kwa mtenda na mtendwa na kuondoa watoto wa mitaani?


  Kisa nimekifupisha ila natumai kimeeleweka!!
   
 2. eRRy

  eRRy JF-Expert Member

  #2
  Oct 13, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 1,080
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  tazama hii video toa maoni yako[ame="http://www.youtube.com/watch?v=cA-vRSg2X0A"]http://www.youtube.com/watch?v=cA-vRSg2X0A[/ame]
   
 3. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #3
  Oct 13, 2009
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Ni sheria ya kipuuzi. Watakaofungwa ni wasio nacho.

  Amandla........
   
Loading...