Miaka 30 bila mpenzi !!

Miaka 30 bila mpenzi !!

Tetra

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2012
Posts
1,526
Reaction score
771
::
Mapenzi ya siku hizi
Yana kila utelezi
Huniacha domo wazi
Nikitokwa na chozi
Najiuliza tangu juzi
Miaka 30 bila mpenzi
Vip,ntashinda huzuni?
::
Nipatapo mchumba
Akili yangu huyumba
Uhusiano hugomba
Yemsomi mi kayumba
Hunichoma ka mwiba
Miaka 30 bila mpenzi
Vip ntashinda huzuni?
::
Nilimpata mwingine
Pato likaleta mengine
Kapenda waleti nene
Nikaachiwa giza nene
Miaka 30 bila mpenzi
Vip ntashinda huzuni?
::
Nikasema sina bahati
Kaja wa penzi la dhati
Jambo moja kanishiti
Kakibamia haka taiti
Miaka 30 bila mpenzi
Vip ntashinda huzuni?
::
Natamani pata mtoto
Nitimize yangu ndoto
Nisiipite dunia ka mto
Moyo unawaka moto
Miaka 30 bila mpenzi
Je nitashinda huzuni?
::
Umri unaenda upesi
Uzee wanitia wasi
Pesa zanikimbia kasi
Naanza jenga utu hasi
Miaka 30 bila mpenzi
Vip ntashinda huzuni?
::
Mola nimemwomba
Mapambio nimeimba
Mafungo ka majumba
Kimya kila nilipoomba
Miaka 30 bila mpenzi
Vip ntashinda huzuni?
::
Nakata tamaa sasa
Dunia kwangu ni tasa
Sina alama ya kuacha
Nikiaga hii yetu dunia
Furaha inanitoweka
Miaka 30 bila mwenzi
Vip ntashinda huzuni?
=
 
MKuu mapenzi yana wenyewe... Endelea tuu kutunga mashairi ndo yanakufaa zaidi..
 
Naona walalamikia
mapenzi kukukimbia
pasipo kutarajia
ila mimi nakwambia
USILIE

Mapenzi unayo wewe
Sema tu unakiwewe
Kwanza jipende wewe
halafu ndio mpenziwe
USILIE

Upendapo bila shuruti
Bila kutegemea sharti
Hutalalamikia tamati
hata lisponyooshwa shati
USILIE

Unapotafuta sana kosa
mapungufu hutayakosa
kila umopataye analokosa
kama wewe mwenye kukosa
USILIE

Usitafute mtakatifu
asokuwa na mapungufu
wapaswa jitia upofu
kwani mapenzi ni upofu
USILIE

miaka yako thelathini
kamwe sio themanini
hivyo bado ukiamini
utampata wa moyoni
USILIE

usitafute sana mpenzi
kwani utajitia majonzi
Muachie YEYE mwenyezi
atayafuta yako machozi
USILIE
 
::
Nakushukuru Kaunga
Ushauri sitoupinga
Moyo unanidunda
Nakuwa kama kinda
Kaunga
::
Themanini ya badae
Inaanza leo sishangae
Upweke kwa aujuae
Haumfai apendae
Kaunga
::
Sitafuti mkamilifu
Jambo moja linalokifu
Yangu mapungufu
Wanayapa utukufu
Na kuniacha mpofu
Kaunga
::
Siyalazimishi mapenzi
Sitatafuta mpenzi
Dunia mekuwa kizuizi
Huzuni n yangu pumzi
Kaunga
=
 
Last edited by a moderator:
....sina mali, sina deni kwaiyo siyo masikini...nmejifunza kupenda nijipende mimi kwanza....people come and go like seasons, i dnt need a reason so i learn to let go...
 
....sina mali, sina deni kwaiyo siyo masikini...nmejifunza kupenda nijipende mimi kwanza....people come and go like seasons, i dnt need a reason so i learn to let go...

::
Da! Queen Kan
For God's sake,,nifafanulie kidogo
=
 
Last edited by a moderator:
tulia Tetra tulia
hayo ndiyo ya dunia
30 si kitu yafaa kuvumilia
shaka ondoa

unajua ni nini
wala usijiulize kwanii
wako yupo nanii
shaka ondoa

kakibamia si tija kwake katakuwa dushelele
atakuwa nawe daima na milele
yeye na wewe furaha mbele
haa haa haa!maombi mbele
ndiyo nguzo njema!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom