Miaka 18 ya kifo cha baba wa Taifa

Miaka 18 ya kifo cha baba wa Taifa

technically

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2016
Posts
13,722
Reaction score
58,933
Miaka zaidi ya 18 sasa toka baba wa taifa atutoke naukumbuka sana mwaka huo 1999 wakati radio tanzania ilipotoa tangazo la kifo chako yalikua ni majonzi ya hali ya juu kwa watanzania wote na watu kipindi hicho walijawa na hofu kubwa uku wengine waliokuwa wazee wakiamini tutavamiwa tena na nchi kuingia kwenye vita kama mwaka 1978.

Wote ni mashahidi jinsi gani tulishuudia Tanzania yenye mshikamano wa hali ya juu kipindi kile kuanzia Wanajeshi,Police na hata wanasiasa tukamzika babu yetu kwa amani kabisa .

Rais Mkapa akihaidi kuendeleza falsafa yake ya kupambana na Umasikini,Ujinga na Maradhi lakini kilichofuata watanzania wote walikiona ikawa historia

ufisadi na kuuza nchi na ushenzi wote ukaasisiwa na Ben hakika ni majonzi kwa vizazi vijavyo..

Najiuliza tu maswali mengi sana yasiyo na majibu iliwezekana vipi kipindi cha nyerere police walikuwa hawana uwezo wa kusumbuana na RAIA wa nchi kamatakamata lakini kwa sasa imekuwa kawaida uonevu juu ya RAIA wa nchi hii?

Iliwezekana vipi nyerere Kuwapa elimu bure wanafunzi wote vyuo vikuu ambao sasa hivi ndio wanawanyima wezao mikopo ya kusoma vyuo vikuu? Pamoja na mapato kuongezeka?

Inakuwaje watu wanasoma na kumaliza uku nchi haina Sera ya kuwafaidi wasomi wake angalau kwa 25%ya waitimu wote wapo mtaani nyerere alitumia uchawi gani kuajiri hata darasa la saba huko nyuma?

Miaka 18 ya kifo cha nyerere watoto bado wanakaa chini wengine kutembea kiromita 10 kufuata shule kwenda kusoma wakati watawala wakipewa almasi ya dola 400 milioni huku wengine wakijenga uwanja wa ndege wa billion zaidi 50 kijijini kwao walipozaliwa..

Miaka zaidi ya 18 police wamekuwa adui wa wananchi maradufu kwa sababu ya uminyaji wa democracy na kupigwa Risasi kwa wapinzani wa serikali imekuwa kawaida na ukihoji unapewa kesi ya uchochezi....

Miaka 18 ya kifo chako babu watu wanatekwa wanateswa wengine kupotea ndani ya taifa lako baba kama livyotokea kwa Ben Saanane hakika ni majonzi makubwa sana.....

Miaka 18, ya kifo chako nchi imegawanyika kwa misingi ya kikabila na kivyama yaani wewe ukiwa na hoja ya kitaifa lazima ubatizwe majina na kila aina Mala gamba mala nyumbu ..

Miaka 18 watawala wanapanga kugeuza katiba kutoka kutawala miaka 5 mpaka miaka 7 nikakumbuka hotuba yako uliyosema kwa katiba tulivyoitengeneza hakuna Rais anaweza tawala miaka zaidi ya 10 lakini haya yanatokea sasa watawala wanajipanga kufanya uhaini juu ya wananchi wao."

Hakika tunakukumbuka sana baba yetu, babu yetu pumzika kwa amani popote ulipo naamini tutaendelea kupambana na kupaza sauti mpaka tupate haki za kweli na si unafiki wa sasa wa baadhi yetu kulialia kimoyomoyo..

R.I.P Baba wa taifa Mwalimu Nyerere..
 
Tutakukumbuka sana Mwalimu Julius Kambarage Nyerere
 
Ngoja nikaae siti ya mbelee nitafte na comment mana bilashaka hii ndo thread ya tar 14/10
 
Duuuuh. .kumbe tayari 18yrs old imepita!!!
Katika kipindi chote hicho, maendeleo makubwa niliyoyashuhudia nchini kwangu ni teknolojia ya kutoka ANALOGIA kwenda DIJITALI, na hasa kubadili simu kutoka Button type kwenda Smart phone, kama kuna maendeleo zaidi ya haya, wananchi wenzangu watanijuza!

Flyover inayojengwa mahala fulani ni teknolojia ya miaka 39 iliyopita ya nchini Nigeria. Kujengea kila kitu site, siku hizi watu wanafanya ASSEMBLING tu hata ya madaraja makubwa, nchini SA, flyover kama ile ilichukua miezi 3 kukamilika, nchini kwangu ni miezi 18.

Tutakukumbuka milele daima....
 
Sitakaa nisahau, siku hiyo Mzee Lido-lofa, anatuingiza mjini kuwa mwalimu hajafa ila anapumulia mashine. Kumbe ilikuwa mikakati ya kutengeneza miundo mbinu na kuandaa guest house na hotel za kufikia wageni wa nje.
Ukweli ni kwamba Mwalimu hakufariki 14.10.99 bali alikuwa amekwisha kata pumzi kabla haya ya hiyo tarehe.
Sijuo Wabongo tulikuwa tumeficha wapi uwezo wetu wa kufikiri na kuhoji.
 
Nakumbuka jinsi tulivyosoma bure kuanzia std1 hadi university huku serikali yako mwalimu ikigharamia gharama zote. Leo watoto na wajukuu zetu tukishuhudia wakichambuliwa kama karanga na bodi ya mikopo huku wanaobahatija wakipewa pesa kiduchu. Hakika tutumkubuka mwalimu kwa mengi. RIP MZEE.
 
Miaka zaidi ya 18 sasa toka baba wa taifa atutoke naukumbuka sana mwaka huo 1999 wakati radio tanzania ilipotoa tangazo la kifo chako yalikua ni majonzi ya hali ya juu kwa watanzania wote na watu kipindi hicho walijawa na hofu kubwa uku wengine waliokuwa wazee wakiamini tutavamiwa tena na nchi kuingia kwenye vita kama mwaka 1978.

Wote ni mashahidi jinsi gani tulishuudia Tanzania yenye mshikamano wa hali ya juu kipindi kile kuanzia Wanajeshi,Police na hata wanasiasa tukamzika babu yetu kwa amani kabisa .

Rais Mkapa akihaidi kuendeleza falsafa yake ya kupambana na Umasikini,Ujinga na Maradhi lakini kilichofuata watanzania wote walikiona ikawa historia

ufisadi na kuuza nchi na ushenzi wote ukaasisiwa na Ben hakika ni majonzi kwa vizazi vijavyo..

Najiuliza tu maswali mengi sana yasiyo na majibu iliwezekana vipi kipindi cha nyerere police walikuwa hawana uwezo wa kusumbuana na RAIA wa nchi kamatakamata lakini kwa sasa imekuwa kawaida uonevu juu ya RAIA wa nchi hii?

Iliwezekana vipi nyerere Kuwapa elimu bure wanafunzi wote vyuo vikuu ambao sasa hivi ndio wanawanyima wezao mikopo ya kusoma vyuo vikuu? Pamoja na mapato kuongezeka?

Inakuwaje watu wanasoma na kumaliza uku nchi haina Sera ya kuwafaidi wasomi wake angalau kwa 25%ya waitimu wote wapo mtaani nyerere alitumia uchawi gani kuajiri hata darasa la saba huko nyuma?

Miaka 18 ya kifo cha nyerere watoto bado wanakaa chini wengine kutembea kiromita 10 kufuata shule kwenda kusoma wakati watawala wakipewa almasi ya dola 400 milioni huku wengine wakijenga uwanja wa ndege wa billion zaidi 50 kijijini kwao walipozaliwa..

Miaka zaidi ya 18 police wamekuwa adui wa wananchi maradufu kwa sababu ya uminyaji wa democracy na kupigwa Risasi kwa wapinzani wa serikali imekuwa kawaida na ukihoji unapewa kesi ya uchochezi....

Miaka 18 ya kifo chako babu watu wanatekwa wanateswa wengine kupotea ndani ya taifa lako baba kama livyotokea kwa Ben Saanane hakika ni majonzi makubwa sana.....

Miaka 18, ya kifo chako nchi imegawanyika kwa misingi ya kikabila na kivyama yaani wewe ukiwa na hoja ya kitaifa lazima ubatizwe majina na kila aina Mala gamba mala nyumbu ..

Miaka 18 watawala wanapanga kugeuza katiba kutoka kutawala miaka 5 mpaka miaka 7 nikakumbuka hotuba yako uliyosema kwa katiba tulivyoitengeneza hakuna Rais anaweza tawala miaka zaidi ya 10 lakini haya yanatokea sasa watawala wanajipanga kufanya uhaini juu ya wananchi wao."

Hakika tunakukumbuka sana baba yetu, babu yetu pumzika kwa amani popote ulipo naamini tutaendelea kupambana na kupaza sauti mpaka tupate haki za kweli na si unafiki wa sasa wa baadhi yetu kulialia kimoyomoyo..

R.I.P Baba wa taifa Mwalimu Nyerere..
umeandika upupu.
 
Pumzika kwa amani mzee wetu! Ulijitahidi sana kujenga Taifa lenye umoja, mshikamano na upendo! Ingawa sera zako za uchumi hazikufanikiwa kamwe hatutakusahau kwa mapenzi yako ya dhati kwa Taifa hili!
 
Ninachokumbuka ni sheria za kumsadia mtumishi Wa silkl asifukuzwe kwa urahisi ksbb kasalary kalikuwa kadogo...mzee ukaona kitendo cha kuajiriwa slkln hasa kada za chini kV less assumed respectable jobs ilikuwa ni adhabu tosha...
RIP mzee wangu...nilikulilia japo nilikuwa form 1...
 
Tutakukumbuka daima JK Nyerere. Ijapokuwa umekufa ungali unanena.
mleta uzi umechanganya mambo ya msingi na propaganda za kijima
 
Back
Top Bottom