Miafrika ndivyo tulivyo

Kiranja Mkuu

JF-Expert Member
Feb 18, 2010
4,066
4,085
Waua ndugu wao wakimtuhumu kwa uchawi


POLISI mkoani Rukwa, wanawashikilia watu sita wa familia moja, katika Kijiji cha Kalumbaleza, wilayani Sumbawanga, kwa tuhuma za kumuua kwa kumpiga kwa mawe na marungu, ndugu yao waliyekuwa wakimtuhumu kuwa ni mchawi.


Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Rukwa, Insunto Matage, alisema tukio hilo lililotokea juzi alasiri, wakati watu hao wakiwa katika maandalizi ya mazishi ya mtoto Clavery Mpenuke, aliyekufa kwa ugonjwa wa malaria.


Mantage alisema baada ya kifo hicho, ndugu na jama wa marehemu walimtuhumu, Joseph Mpenuke (55) kuwa ndiye aliyemroga mtoto huyo na kwamba muda mfupi baadaye, walianza kumshambulia kwa mawe na virungu hadi walipomuua.

Kwa mujibu wa kamanda kitendo hicho kilifuatiwa na cha watu hao kuchoma moto mwili wa marehemu.

Alisema polisi wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo, kabla ya kuwafikisha mahakamani watu hao kujibu mashtaka.

Kamanda Mantage, aliwataka wananchi mkoani Rukwa, kucha mara moja kujichukulia sheria mikononi na badala yake wafuate taratibu.
 
Back
Top Bottom