Mi ni mhanga wa nyumba nitawezaje kukata rufaa

Mi ni mhanga wa nyumba nitawezaje kukata rufaa

Levi isaya

Member
Joined
Apr 1, 2013
Posts
18
Reaction score
0
Mwana jf mm na tatizo ambalo nafikiri wana siasa wameingiza mikono yao ili wanihujumu,mm nina nyumba yangu ya vyumba sita mitaa ya G/mboto, manispaa inataka kunitoa ili kupisha utanuzi wa hospital. wamenilubuni wanasiasa na manispaa wamenipa milion 25 bila kiwanja ili nitoke, nimekubali shingo upande ili kupisha maendeleo kwenye kata hiyo,ila kwa maisha ya sasa ni hela ndongo sana katika ujenzi na ni bora wangenipa kiwanja lkn wameshindwa kunipa wamesema manispaa aina viwanja. Ss mm nauliza jinsi ya kukata rufaa ili waniongeze hela maana nishachukua hizo hela.
 
Kupokea hizo hela umefanya kosa ,Mtanzania anayohaki ya kuishi popote pale,hivyo ikiwa ni hospita na wameptia serikalini katika upanuzi wa au ujegaji wa hospita,ni lazima wakujengee nyumba sehemu ingine ,au tafuta nyumba inayouzwa katika eneo hilo uwapelkee wainunue na kukukabidhi, au wakutafutia kiwanja sehemu yeyote ile hapo DSM ,wakupe na hela za kujengea jaribu kupitia mikataba ya kibenki na pia usikubali wakupe hela wambie wakujengee wao ,ndio mambo yaendavyo ughaibuni. Na katika eneo lako hilo bei ya nyumba ni shilingi ngapi ? Kama ni kutendewa haki basi wakununulie nyumba tu ingetosha.

Sa kama walikuuliza unataka wakununulie nyumba au unataka hela ,kwa tamaa zako ukawambia unataka hela basi ujue ndio imetoka .
 
Ucwe mkali kaka ni ivi baada ya kuitaka nyumba wakaja kupiga tathmin ya iyo nyumba na kuchanganua wakitumia wataalam wao wa vipimo na kukuta iyo nyumba ina kiasi icho.so nipe ushaur kaka
 
Ucwe mkali kaka ni ivi baada ya kuitaka nyumba wakaja kupiga tathmin ya iyo nyumba na kuchanganua wakitumia wataalam wao wa vipimo na kukuta iyo nyumba ina kiasi icho.so nipe ushaur kaka
Pole mkuu mimi naona ulikosea sana sana kupokea hizo hela. Kitendo cha kupokea hela inaonyesha
tayari umekubaliana nao.
 
Kosa kubwa ni kuchukua Kimya kimya halafu ndo inakuja kuomba ushauri
 
Ucwe mkali kaka ni ivi baada ya kuitaka nyumba wakaja kupiga tathmin ya iyo nyumba na kuchanganua wakitumia wataalam wao wa vipimo na kukuta iyo nyumba ina kiasi icho.so nipe ushaur kaka

Achana na tathmini yao wewe ni lazima uwe na hoja ,kwa mfano kununua nyumba katika eneo hilo utainunua kwa bei gani ,muhimu wambie wakununulie nyumba kama hiyo au inayolingana na hiyo ,wambie huna haja ya hela unataka ukabidhiwe nyumba na si vinginevyo ,ila angalia usije ukakosa vyote maana serikali yrtu ni ya wababe na kutendewa haki ni vigumu.

Au wakupe kiwanja na hela ya kujengea ,vinginevyo kama hela umeshapokea ndio tunasema imetoka ,sijui wakikwambia uludishe hiyo hela kama bado unayo !
 
Ucwe mkali kaka ni ivi baada ya kuitaka nyumba wakaja kupiga tathmin ya iyo nyumba na kuchanganua wakitumia wataalam wao wa vipimo na kukuta iyo nyumba ina kiasi icho.so nipe ushaur kaka
Kikubwa ni kwamba tayari ushapokea hela, jambo lililoonyesha kwamba uliridhika na hela uliyopewa. Hakuna serikali itakayointertain hilo. Kwa sasa nenda kakomae mwenyewe tu kuhakikisha unapata mahali pengine pa kuishi. Bila shaka unawakumbuka wale wakazi wa kipawa, waliopokea hela halafu wakaanza kukaa barabarani kutaka waongezwe. Nafikiri unakumbuka walichofanyiwa. Namna nzuri ilikuwa ni kutokukubaliana na tathimini iliyofanywa. Maana kiwanja pekee inaweza kuwa ni karibu na nusu ya hiyo hela kutegemeana na mahali kilipo, sasa wewe ulifikiri ukipokea milioni 25 kiwanja utanunua bei gani na ujenge kwa bei gani? Pole, imekula kwako hiyo. Sijui kama hata ukienda mahakamani utashinda hiyo kesi.
 
Achana na tathmini yao wewe ni lazima uwe na hoja ,kwa mfano kununua nyumba katika eneo hilo utainunua kwa bei gani ,muhimu wambie wakununulie nyumba kama hiyo au inayolingana na hiyo ,wambie huna haja ya hela unataka ukabidhiwe nyumba na si vinginevyo ,ila angalia usije ukakosa vyote maana serikali yrtu ni ya wababe na kutendewa haki ni vigumu.

Au wakupe kiwanja na hela ya kujengea ,vinginevyo kama hela umeshapokea ndio tunasema imetoka ,sijui wakikwambia uludishe hiyo hela kama bado unayo !
Tatizo lake ni kwamba hela tayari keshachukua. Labda aende tena akawaambie anarudisha hela ili wafanye hayo wenyewe. Jambo ambalo nadhani huwa halikubaliki pia. ILikuwa aseme haya kabla ya kupokea hela. Nina experience ya matatizo yaliyotokana na mabomu ya gongolamboto ambapo nilipewa hela isiyotosha hata nusu ya gharama ya uharibifu nilioupata. Na wale jamaa walikuwa wakali kabisa, hawataki mjadala.
 
ungekuja jf mapema ungepewa ushauri wa kukufaaaa....samahaniiiii sina ukabila ila to be honest hapo angekuwa mchaga angevuna million nyingi sana.....
mf kunajamaa <fro kilimanjaro >nyumba yake imepakana na lilipo jengo la crdb tabata jamaa walitaka kumnunuaa mkwara wake wa kwanza aliwaambia yeye mwenyewe alikuwa anafikiria jinsi ya kununua ajengo lao kabla wao awajamfuata yaani wamewahi mawazo yake ...ebu fikiria kama ungekuwaa wewe utafanya nini ilibidi jamaaa wageuze kama walikuwa na vimilioni mia sijui ila walikimbia...mkuuu inatakiwa ujiami usiwe muogaaaaaaaa kama unauhakika mali ni yakwako ...hapo imekula kwako labda ujifanye ulikubali maleria ikiwa kichwani
 
Mwana jf mm na tatizo ambalo nafikiri wana siasa wameingiza mikono yao ili wanihujumu,mm nina nyumba yangu ya vyumba sita mitaa ya G/mboto, manispaa inataka kunitoa ili kupisha utanuzi wa hospital. wamenilubuni wanasiasa na manispaa wamenipa milion 25 bila kiwanja ili nitoke, nimekubali shingo upande ili kupisha maendeleo kwenye kata hiyo,ila kwa maisha ya sasa ni hela ndongo sana katika ujenzi na ni bora wangenipa kiwanja lkn wameshindwa kunipa wamesema manispaa aina viwanja. Ss mm nauliza jinsi ya kukata rufaa ili waniongeze hela maana nishachukua hizo hela.

Mkuu mbona usipeleke hii mada kule jukwaa la sheria ukutane na ma-Guru wa fani hii ya sheria unayotaka ushauri kuliko kuileta huku ambapo wengi tutakujibu kwa utashi na wala si kisheria?
 
Mkuu mbona usipeleke hii mada kule jukwaa la sheria ukutane na ma-Guru wa fani hii ya sheria unayotaka ushauri kuliko kuileta huku ambapo wengi tutakujibu kwa utashi na wala si kisheria?

mkuu hapo umenena maana hawa watu wananijibu kunya tu mi nataka ushauri tu jinsi ya kuandika barua ya madai wao wanapolomosha maneno ya ajabu mi nishakosea najuta kweli nimekosea ndo maana naomba ushauri jinsi ya kuandika barua ya rufaa
 
Back
Top Bottom