Msaada wa kisheria; Ni muda gani unaruhusiwa mtu kukata rufaa kutoka Mahakama kuu kwenda Mahakama ya rufaa kwa kesi za madai?

Bhujegwe

Member
Nov 23, 2013
22
75
Ninawiwa kusaidiwa kujua ni muda upi kisheria ambao mtu aliyeshindwa kesi ya madai Mahakama Kuu-Ardhi atakuwa ndani ya muda kukata rufaa kwenda Mahakama ya Rufaa.

Swali langu linajengwa na case ground ifuatayo japo kwa ufupi sana. Mnamo mwaka 2014,Jamaa yangu Mjasiriamali aliomba na kupewa mkopo tshs.10m kutoka benki ya Posta Tanzania tawi fulani huko jijin Mwanza. Ambapo aliweka nyumba yake ya makaz km dhamana ya mkopo huo (ambayo ktk mkataba wao na benki walikubaliana na kusainiana kuwa ilikuwa na thaman ya tshs 50m),kwa mkataba wa marejesho ya mwaka mmoja.

Hata hivyo baada ya miez 3 tokea kupata huo mkopo, jamaa alivamiwa dukani na majambaz dukan na kunyang'anywa kias kikubwa cha fedha. Lilikuwa tukio la waz na liliripotiwa Polis station-Nyakato ambao walifika dakika 15 baada ya wizi huo kutendeka.
Licha ya ugumu wa kibiashara,jamaa aliendelea kujikongoja kupeleka marejesho kidogo kidogo ingawa anakiri kwa sehemu hakuweza kwenda sawa tena na makubaliano ya kimkataba.

Kwa maelezo yake benki waliuza nyumba yake miezi 4 kabla ya Mkataba wao kuisha kwa tshs 9.9m na ni ktk wakati ambao deni lilikuwa limebakia tshs. 7.5m tu. Kwenye mauzo hayo hakupewa pesa yoyote iliyozid!

Hiyo ni nyumba ya vyumba 4 vya kulala huku masterbedroom ikiwa ni self,ikiwa na dinning,kitchen na sitting room,tiles,ceilling bord,umeme na maji ndani choo na bafu kwa nje na kiwanja kikiwa na nyumba nyingine ya vyumba 2 pembeni.

Licha ya kuwa amehangaikia kuanzia baraza la ardhi na nyumba la Nyamagana had Mahakama Kuu-Ardhi bado amejikuta akiangukia pua.

Binafs nimehis hukumu za kushindwa kwake ni matokeo ya yeye kutopata Mawakili wenye nguvu za Kisheria ili kumsaidia kutetea haki yake na hasa nikizingatia kuwa aliyeichukua hiyo nyumba ni kigogo mmoja wa CCM (Nasikia alikuwa Katibu wa CCM Wilaya ya Bunda wakati huo). Na ndiyo maana ilitumika nguvu kubwa ya kumtoa nje pasipo kibali cha mahakama.

Niko kutafuta namna ya kumsaidia huyu jamaa ili ajarib kuitafuta haki ikiwa bado mlango wa kisheria utaruhusu. Kwa maelezo yake,aliandika barua ya malalamiko ofisi ya TAKUKURU kuomba msaada lakini akajibiwa kuwa suala lake linapaswa kushughulikiwa ktk mfumo wa kimahakama ilimradi lilishapelekwa huko. Lakini hata wao walikiri anazo sababu za msingi kwenye shauri lake.
Hukumu ya Mahakama Kuu-Ardhi ilisomwa mwaka jana mwezi June.

Je,kungali kuna mlango wa kisheria kulifuatilia na kukata rufaa Mahakama ya Rufaa?

Naombeni hekima,busara na huruma zenu ili tumsaidie,kwa vile tu yeye alikwama pale Mawakili walipompa hesabu ya zaidi ya tshs.5m km gharama za kesi!

Huyu ni mtu anahangaika na nyumba za kupanga na kwa familia yake ya wategemezi 15 anapitia wakati mgumu huku mtu mwingine kwa kutumia cheo chake tu akifaidi nyumba aliyoijenga kwa jasho na damu akitumia vihela vya kudunduliza.

Msaada wenu wa Mawazo ndugu zangu!!!
 
Vitalis Msungwite

Verified Member
May 11, 2014
2,187
2,000
Muda wa kukata rufaa wa kimahakama ni ndani ya siku 30(sijui kwa mahakama za juu utaratibu upoje), lakini kuna utaratibu wa kukata rufaa nje ya muda wa kisheria.

Tukirudi kwenye kesi, bank huwa wanathaminisha dhamana na wanakupa mkopo ambao ni robo au 30% ya thamani ya dhamana yako. Lengo ni kuwa katika kuuza Mali ili kufidia deni lao wasipate changamoto ya wateja.

Kwahiyo bei ya nyumba waliuza kihalali na ndugu hakuiridhisha bank kuwa anaweza kumaliza mkopo uliobaki ndani ya miezi 4 ambao ni 75% ya mkopo wote. Kwahiyo hana chake labda atafute angle ya kisheria ya kuingilia.

Kuhusu chajuu, ndugu yako na wewe lazima mjue kuwa bank hawakuuza nyumba bali dalali aliyepewa kazi husika. Hivyo kiasi cha million 2 kilichozidi kinaweza kuwa kilitumika katika mchakato wa uuzaji. Iwapo ndugu yako mwenyewe angeuza nyumba kwa hiari kabla ya watu wa bank huenda angeuza kwa bei nzuri na chajuu kungekua kikubwa. Alitakiwa auze mapema na kuwapelekea bank pesa yao mapema hivyo hana chake hapo wala hela ya juu hapati.

Kwa kukazia hapa mtaani kuna TREKTA na tela lake vimeuzwa kwa mill 5.5 baada ya mdaiwa kushindwa kulipa million 4 alizokua anadaiwa, lakini hata mia hakupata kwasababu chajuu ni ghalama za mchakato.

Kuhusu sababu za kufeli kurejesha. Ndugu yako anatakiwa akuoneshe mkataba ulisemaje katika mambo kama hayo. Kama mkataba haukuwa na kipengele cha kuzungumzia changamoto za kibiashara kma wizi, moto, ajari/uharibifu wa bidhaa na hasara zitakazojitokeza au kifo cha mkopaji basi hana chake.

Kama kesi ilianza mahakama za awali mpaka rufaa bado ameshindwa mshauri apambane na maisha tu. Vilevile kuhusu mteja kuwa wa chama usichokipenda haina mashiko kisheria. Mteja anaweza kuwa adui yako, Ex wako, mgoni wako, ndugu yako au mtu usiyemjua lakini suala ni mteja bhaaasi. Kwahiyo hoja hiyo haitamsaidia iwapo tu mteja huyo alipatikana kisheria.
 
Bhujegwe

Member
Nov 23, 2013
22
75
Nikushukuru kwa maelezo yal

Nikushukuru kwa maelezo yaliyonyooka. Lakini pengne nisaidie zaid kwenye eneo hili;
1. Kipengere kinachosema nyumba iliyowekwa dhamana ya mkopo isiiuzwe chini ya 75% ya bei ya soko kinahusika eneo gani.
2. Benki inatakiwa kupitia hatua zipi kisheria kabla ya kuuza nyumba ya mteja?
LAKINI pia niweke mambo sawa,nikueleweshe kuwa mimi sina itikadi yoyote ya chama cha siasa. Na nimetaja title ya mhusika ktk kufafanua ukigogo wake tu. So usini-link na maslahi ya kisiasa
 
Vitalis Msungwite

Verified Member
May 11, 2014
2,187
2,000
1. Kipengere kinachosema nyumba iliyowekwa dhamana ya mkopo isiiuzwe chini ya 75% ya bei ya soko kinahusika eneo gani.

MAJIBU: kipengele hicho kinahusika wakati wa mchakato mzima. Lakini ili kujua kama nyumba imeuzwa kwa bei ya 75% ya soko lazima zoezi lifanywe na mmiliki kwa hiari lakini bank wakija na dalali wao wakauza basi hata wakikudanganya hutakua na sehemu ya kurukia. Kwasababu wewe kama mmiliki huna vyanzo vya kuiridhisha mahakama kuwa nyumba au Mali yako ilikua na thamani fulani sokoni wakati fulani.

Mfano; Nyumba ya jamaa yako ilitathiminiwa kuwa ni million 50 mwaka 2014. Baada ya miaka kadhaa kupita thamani yake huenda ilishuka mpaka mill 30/25 kutokana na watu wengi kujiingiza kwenye biashara ya kujenga na kuuza nyumba. Sasa basi kama soko la nyumba limeyumba kwa kiwango hicho, huwezi kuuza nyumba hiyo kwa million 18 kama 75% ya million 25 wakati deni lako ni asilimia 50 ya Mali na mteja au mdaiwa hatoi ushirikiano kwa mamlaka za ufilisi.

Kuhusu taratibu za kisheria za kufuatwa na bank sizijui. Lakini Mara nyingi bank hutumia masharti ya mkopo katika utekelezaji wa majukumu yake.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom