mhhhhh hii kali kweli!

mhhhhh hii kali kweli!

mashakaDaima

Member
Joined
May 3, 2013
Posts
38
Reaction score
5
jamaa mmoja aliyekuwa ameoa alipatwa na maswaibu pale alipokuwa anakojoa kitandani kila siku kiasi kwamba mke akaamua kutaka kumuacha, jamaa kuona vile akaamua kwenda kuomba ushauri kwa rafiki ili kunusuru ndoa yake. Jama akamuuliza kwani tatizo ni nini hadi imekuwa hivyo jamaa akaanza kila ikifika saa nane usiku naota kuna jamaa mmoja baunsa anakuja usiku na panga na kuniambia nikojoe lasivyo ananiua hivyo basi kwa kuogopa huwa najikuta nimekojoa na nikiamka asubuhi nakuta nimeharibu mashuka na godoro so ke amechoka kufua na ametangaza nia ya kuniacha kwa hiyo naomba ushauri wako je nifanyaje? Jamaa akamwambia si huwa anakuja na panga sasa na wewe chukua panga ulale nalo jamaa akija tu unamwanzishia na yeye jama kweli siku hiyo akalala na panga mida kama ile ya siku zote baunsa akaja akamwambia kojoa kabla sijakuua jamaa akakumbuka kuwa na yeye ana panga hivyo akalichukua na kuanza kukimbizana j baunsa baada ya kushindwa kukimbia akadumbukia chooni sasa jamaa akaamua amkomeshe akasema sasa na wewe leo nakupa adabu akachuchuuma na kuanza kujisaidia ile tu kumaliza akakurupuka kutoka usingizini na kujikuta kaharibu mambo . Je wewe unadhani mke wake atafanyaje?
 
Asingekubali ushauri

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
hahahahaaaaa, mke ataona huo ni mgomo jamaa hamtaki hivyo atang'ang'ania
 
Nimechekaje?
Hii ni soo. Hapo inabidi mke awe anamvalisha pampasi tu maana hakuna namna.
 
Back
Top Bottom