Mhhhh! Bado tuna safari ndefu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mhhhh! Bado tuna safari ndefu

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by BAK, Nov 28, 2011.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Nov 28, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,718
  Likes Received: 82,646
  Trophy Points: 280
  Wanawake wasema: Waume zetu wana haki ya kutupiga
  Imeandikwa na Grace Mkojera; Tarehe: 25th November 2011
  Habarileo

  ASILIMIA 47 ya wanawake wanakubali kwamba mume ana haki ya kumpiga mkewe pale mwanamke anapozembea kuangalia watoto.

  Aidha asilimia 29 wanakubali kwamba mume ana haki ya kumpiga mkewe iwapo atakataa kufanya tendo la ndoa na asilimia 20 watapigwa ikiwa wataunguza chakula.

  Taarifa hiyo imo katika hotuba ya Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto kwa niaba ya Naibu Waziri wa wizara hiyo, Kijakazi Mtengwa aliyoitoa wakati wa uzinduzi wa kampeni ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia zilizofanyika ukumbi wa Don Bosco, Dar es Salaam jana.

  Mtengwa alisema takwimu hizo kutoka utafiti uliofanywa mwaka 2010 na Idara ya Takwimu kuhusu hadhi ya wanawake nchini ulibaini pia asilimia 46 ya wanawake wanaafikia kwamba mume ana haki ya kumpiga mkewe iwapo mke atajibishana naye, asilimia 43 ya wanawake wanaafiki mume ana haki ya kumpiga mkewe kwa sababu ya kuondoka bila kuaga.

  “Hizi ni fikra potofu kwa wanawake na wanaume na zinapaswa kupingwa kwa nguvu zote, Serikali kwa kushirikiana na wadau wake wa maendeleo inafanya jitihada mbalimbali katika kupambana na ukatili dhidi ya wanawake na watoto,” alisema.

  Alisema katika kupambana na tatizo la ukatili wa kijinsia zipo mbinu mbalimbali zinazoweza kutumiwa ili kusonga mbele katika kufikia malengo ikiwa ni pamoja na kutumia mbinu shirikishi jamii ili kuhakikisha kunakuwa na ushiriki wa makundi yote katika jamii, kwa kutumia mbinu hizi wananchi wataweza kubuni mikakati ya kijamii ambayo ndiyo italeta suluhisho la kudumu la tatizo hilo.

  Kwa upande wake Mwenyekiti wa Shirika la Wanawake katika sheria na Maendeleo Afrika (Wildaf), Naomi Kaihula alisema vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake sio tu kwamba vinadhoofisha kiafya, bali pia vinaathiri uwezo wao wa kushiriki na kuchangia katika kuleta maendeleo kiuchumi ndani ya familia zao na nchi.

  Takwimu nyingine zinaonyesha kuwa makosa ya ubakaji yamekuwa yakiongezeka kutoka 3,721 mwaka 2002 na kufikia 8,878 mwaka 2007 wakati huo makosa ya ulawiti yaliongezeka kutoka 490 mwaka 2002 kufikia 567 mwaka 2007.

   
 2. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #2
  Nov 28, 2011
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,591
  Likes Received: 797
  Trophy Points: 280
  Utafiti huo ungefanyika humu l mean JF nisingetegemea matokeo tofauti, it is so sad! Safari ni ndefu sana tu.
   
 3. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #3
  Nov 28, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,650
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Nachelea kuamini hayo matokeo ya hizo tafiti lakini tena baada ya kuona mitazamo ya baadhi ya kina dada/wamama wa humu sishangai kabisa.

  It is frightening but then again to each his/her own. After-all, what do I know?
   
 4. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #4
  Nov 28, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  Huo utafiti hao wanawake walikuwa wanahojiwa wakati wana usingz wa wamelewa. Mtu mzima na akili zako huwezi kukubali mangumi.
   
 5. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #5
  Nov 28, 2011
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,591
  Likes Received: 797
  Trophy Points: 280
  Hussy, utakibali kuacha ndoa yako na watoto kisa mume kakutwanga ngumi kwa kosa ulilofanya? I tell u hata humu humu, baadhi yetu tunaamini, mwanamke akikosea; say kubambwa na SMS from a lover (si ndio kosa kubwa ktk relation) mume ana haki ya kumtwanga!

  Personaly siamini kama kuna kosa lolote ambalo adhabu yake ni kupigwa; kuachwa YES.
   
 6. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #6
  Nov 28, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  aisee, labda inategemea na malezi. Kuna watu pamoja na kuwa watu wazima bado wanatandikwa na wazazi. Si ajabu hata wakiolewa wataona kupigwa ni jambo la kawaida. Pia mazingira wanayoishi. Wanaona mama zao wanapigwa, inajengeka akilini mwao mwanamke akikosea lazma apigwe.
  Binafsi baada ya kubalehe sijawahi kupigwa tena (ingawa nilikuwa nakosea mara moja moja). Kabla ya hapo sikumbuki kama nimekula vichapo, sijawahi kuona mama amepigwa wala kukaripiwa. Kwangu mimi kupigwa ni kosa kubwa na siwezi kulivumilia hata kidogo.
   
 7. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #7
  Nov 28, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  @kaunga, kuna wadada wanaaccept vipigo kabla hata hawajaolewa. Ina maana wakiolewa kwao itakuwa ni jambo la kawaida. Mi mapenzi ya vipigo yatanishinda.
   
 8. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #8
  Nov 28, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,650
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Wanawake bana...wengine wanajidai hawakubali vipigo lakini infidelity wanaikubali (kwa kusamehe mara sabini)
   
 9. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #9
  Nov 28, 2011
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,660
  Likes Received: 1,494
  Trophy Points: 280
  kha....hivi Hus, kumbe huwa unabalehe na tayari? mbona mjombako sijui?:photo::poa
   
 10. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #10
  Nov 28, 2011
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,660
  Likes Received: 1,494
  Trophy Points: 280
  hapo hakuna kipigo sasa....
   
 11. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #11
  Nov 28, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,650
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Kubalehe ndo kuvunja ungo?
   
 12. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #12
  Nov 28, 2011
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,874
  Likes Received: 6,228
  Trophy Points: 280
  wewewewewewewewewewe eti? wanaume wana haki ya kufanya nini? weeeee hawawezi kuwa serious!!!
   
 13. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #13
  Nov 28, 2011
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Unategemea nini iwapo wengi wetu hatuzijui hata haki zetu ndani ya ndoa? Utafiti huu ungeenda sambamba na kuangalia kama wanawake wanazielewa haki zao katika mahusiano kisha ndo wahojiwe kama ni sawa kupigwa na mume.
  Bado tunayo safari.
   
 14. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #14
  Nov 28, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  aunt anajua.
   
 15. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #15
  Nov 28, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  infi=vipigo?
   
 16. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #16
  Nov 28, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 444
  Trophy Points: 180
  Mwanamke akitaka kupigwa on her own accord lazima nitamtandika mpaka ataingia uvunguni mwa kitanda
   
 17. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #17
  Nov 28, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  Do so wanakubalia kwa hiyari ............kukung'utwa!
   
 18. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #18
  Nov 28, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Mada kama hii iliwahi kuletwa tena kwahiyo hata sishangai. . . plus niliwahi kuweka mada kuuliza nini kinaweza kumfanya mtu amuache mwenzi wake na kipigo hakikupewa priority.

  Mawazo ya "mume ndo mwenye haki" . . . "mume ananimiliki" na kuogopa kuacha/achika ndio vyanzo vya kuona wanastahili kipondo. Inasikitisha kweli.
   
Loading...