mhh nimechoka wala sijafika mbali?

Mapenzi ya mbali yashanichosha sijafika mbali mienzi kadhaa tooo. Naogopa kumwambia nimechoka siwezi tena sijui itakuwaje wadau ushauri. Si atanichukia maana kanambia hawezi kuowa tena nikimuacha. Kasema nitamuumiza sote tunasoma ila nchi tofauti mwenzangu afrika mie nje.sasa sijui itakuwaje mii siwezi nishachoka mapenzi ya simu na email. Wadau usahauri please nifanyaje si nitamuuwa mtoto wa watu au anadanganya maana tumependana on the phone and fb lakini tunajuana nyumbani

Endeleeni kudanganyana na hadithi za Bulicheka na Sindibad!!! Mkichoka anzeni hadithi za 'hapo zamani alikuwepo sungura na fisi..'!
 
Hahaha duuuh maneno hayo hata kwenye kanga yapo...ukimuacha atatafuta mwingine ataoa tu na hv mpo mbali anamega wengine huku may be am not sure ila anakupa moyo hahahahah....fanya matendo kata mawasiliano nae as action speak so loud....atajisepesha fastaaa

Watu wa aina yako huwa siwapendi, Kwanini usimuambie mtu ukweli? kama distance inakushinda unasema, au humpendi tena,unasema. Si kumfanyia action wakati mwenzako anakupenda. Action ni nzuri kwa mambo mengine but si hayo. its best kufunguka,
 
Mapenzi ya mbali yashanichosha sijafika mbali mienzi kadhaa tooo. Naogopa kumwambia nimechoka siwezi tena sijui itakuwaje wadau ushauri. Si atanichukia maana kanambia hawezi kuowa tena nikimuacha. Kasema nitamuumiza sote tunasoma ila nchi tofauti mwenzangu afrika mie nje.sasa sijui itakuwaje mii siwezi nishachoka mapenzi ya simu na email. Wadau usahauri please nifanyaje si nitamuuwa mtoto wa watu au anadanganya maana tumependana on the phone and fb lakini tunajuana nyumbani

Kuna wakati hasa ktk mazingira magumu unapaswa kufuata kichwa na kuusaliti moyo wako ikiwa itafika mahali vikatofautiana, ila unapaswa ujiridhishe kuwa hutakuja kujutia uamuzi wako.
 
Kaa utulie wewe mbona mimi niko mbali huko unakoita nje ya nchi zaidi ya mwaka sasa lakini mambo yanaenda.Kila mtu anaamini kuwa hakuna anae-cheat.Umepata wa kukuzuzua chuoni eti??utajuta!!Shauri yako.

....mpe za uso kiongozi, eti nimechoka ! kama angekuwa mkeo je ??
 
kweli bana mapenzi ya long distance uzushi tuu...mwambie mie ninechoka na siwezi kupoteza muda kwenye fb.
 
Tatizo lako ni kwamba humpendi mkaka wa watu maana kama ungekuwa unampenda, umbali usingekuwa tatizo. Kwani huko mnakosoma hakuna likizo ambazo mngeweza kuzitumia kwa kuchangishana ili mmoja wenu asafiri kumfuata mwenzake.Vinginevyo nakubaliana na aliyesema kuna tatizo zaidi ya hilo ulilotaka tukushauri tena kwa mawazo yangu yawezekana una mtu mwingine na unatumia distance kama kigezo cha kumpiga chini mwenzako.
 
sababu ya ww kuchoka ni ipi?
mawasiliano hafifu?unahisi anakusaliti?
au umefesibuka ukapata wa karibu na ww?
mvumilie kama unampenda nae anakupenda!
kama mna malengo lakaini1

una tatizo kubwa zaidi ya hili tunalolisoma hapa!
muulize aliyenielewa akwambie una tatizo gani!

Keshapata pa kuutua mzigo ndio maana anapiga kelele kuwa amechoka. Angekuwa hajafika kituoni unadhani angetamani kushuka?
 
Keshapata pa kuutua mzigo ndio maana anapiga kelele kuwa amechoka. Angekuwa hajafika kituoni unadhani angetamani kushuka?

kwa hiyo hata msaada kwenye tuta anaomba sio!mradi ashuke!
af nimekumis mama!
 
kwa hiyo hata msaada kwenye tuta anaomba sio!mradi ashuke!
af nimekumis mama!

Hata mie nimekumiss mwanangu. Ngoja nikimbie nisijelaumiwa nachakachua uzi wa watu badala ya kusaidia jinsi ya kupunguza uchovu.
 
Mie mdada but asante kwa ushauri kwani wewe unaishi nje. Swali wewe unaonaje vijana wa nje unawaamini maana ukiishi kwa sie wadada wengi hatujui hasa wanaume na tabia zao maana kila mtu na maisha yake. Ablessed
Kwa kweli watu wengi wanaoishi nje hawaaminiki sana japo sio wote. Kama ulivyosema kila mtu na maisha yake, yaani nimewaona wadada kadhaaa wamekosa choice zao wameishia kuishi na watu ili mradi tu na wengine imeshindikana wanaishi wenyewe tu sio kwamba wanapenda hapana imeshindikana. Halafu kua na mtu unaemjua hadi kwao ni kitu kizuri japo sio lazima, wapo wanaokuja kugeuka baadae . Si unajua maisha hayana formula Angalia moyoni mwako nini hasa kimekukera kwa huyo mwenzako kwani si vizuri kuendelea kusisitiza kua huyo anakufaaa ilihali wewe umeshaona mapungufu yake . Mimi nadhani kuna sababu zaidi ya umbali dear, mtu yeyote utakaemchagua wewe ndie utakaeishi nae so chunguza moyo wako vizuri. Naomba unielewe vizuri sina maana vijana wote wanaoishi nje hawaaminiki . Nimetembea sehemu kadhaa ndio maana nikasema kuwa hawaaminiki hasa baada ya kukutana na madada kadhaa na kuwauliza wanaonaje maisha ya kuishi nje wakaniambia challenge walinazokutana nazo ni kupata wenzi wao . Kwa kweli waliongea kwa uchungu sana sasa huenda niliongea na group ambalo sio sahihi.
 
Kweli Ablessed nishawaona wengi wanoanzisha mahusiano huku yanakua hayatambulikani shagla baghla ila mie pia uyo jamaa simjui kwao walaa tabia sijui zikoje miaka tele tangu niondoke ndo mana nahisi mtihani maana mapenzi yetu ya kuandika hatujawahi onana tukasema nakupenda ingekua ivo maybe moyo wangu usingesita mii naona mapenzi ya kuonana naona tofauti na kupendana umo online naona
 
Last edited by a moderator:

Mbona mauzauza umesema nyumbani mnafahamiana tena haupajui!
 
Last edited by a moderator:
Hujachoka dada ila sema tu umepatwa na mwingine so unatafuta means ya ku justify hayo mapenzi yako mapya na kumtelekeza mwenzako wa awali.

Hii ni usaliti kama usaliti mwingine wowote kwa kutumia kigezo cha distance ama ile wanaita out of site out of mind, lakini kwa kufanya hivyo sidhani kama imetulia unless kama kuna tatizo lingine.
 
The secretary ndio tunajuana shule too wala hamna mmoja kati yetu anopajua kwa mwenzie maana enzi izo hatukuwa wapenzi wala rafiki classmate too haya yote yameanza online
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom