Mheshiwa Rais Magufuli, taifisha shule zote za umoja wa wazazi

BEHOLD

JF-Expert Member
Nov 17, 2013
5,056
10,721
Na hili wala sio la leo, Ilishapendekezwa na kuazimiwa kwenye vikao vya Chama kuwa Shule zote za umoja wa wazazi aidha zichukuliwe na serikali au zibinafishwe!

Kinachoendelea hivi sasa watu wanatapeliwa hapo Umoja wa Wazazi kwa ahadi kuwa watapewa shule waendeshe. Vinara wa utapeli huu ni Mwenyekiti, Naibu katibu Mkuu na Wakuu wa Idara zake.

Zipo pia shule zimeuzwa, wafanyakazi hawakupata malipo yao, Mfano Hedaru.

Ukitaka kujua hili Mheshimiwa fuatilia tu hata kwa inteligensia utajua.

Nashauri, kama ulivyofanya kwa Omumwami, taifisha shule zote tena kwa usimamizi maalum ili angalau watu wapewe haki zao na aibu hii iondoke!
 
Na majengo yote maana si yalijenga kwa kodi za wananchi wakati wa chama kimoja?
 
Asiishie kwenye shule tu ataifishe Viwanja vya mpira pia..majizi yalijimilikisha kama vyao kumbe vya wananchi
 
Kumbe kwa kuwa mmekosa maslahi binafsi? Basi ataifishe na taasisi nyingine za kiserikali ambazo zimeshindwa kufikia malengo ya uendeshwaji wake!
 
Hiyo ilikuwa kama kumchangia mwanaume harusi, Akishaoa mke ni wake si wenu! LOL
Ngoja tuwaite watu watengeneze thread iliyoshiba, utaniambia kama hata amrisha audit haraka na kuyarejesha serikalini hima.
 
Zinamilikiwa na Umoja wa Wazazi Tanzania. Msimamizi mkuu ni Katibu Mkuu wa umoja huo!

Mwenyekiti wake ni Abdalah Bulembo.
sio umoja wa wazazi Tanzania ni umoja wa wazazi wa chama cha mapinduzi tz
 
Haya haya...CCM Kambarage, CCM Kirumba, Sheikh Amri Abeid Memorial Stakihumu, Nangwanda Sijaona, Jamhuri, Ali Hassan Mwinyi, Sokoine na Maji Maji
 
Tunaomba otodha ya shule zinazomilikiwa na jumuiya ya wazazi.
 
Sangu sec,ivumwe sec, igawilo sec na meta sec zamani N/A ya watoto wa machifu Nayo eti ya wazazi wa ccm zote zipo mbeya town.
 
Back
Top Bottom