Mheshimiwa raisi kupata jiko valentine day...

Mheshimiwa raisi kupata jiko valentine day...

Sajenti

JF-Expert Member
Joined
Apr 24, 2008
Posts
3,651
Reaction score
416
Raisi wa Malawi Bingu wa Mutharika anategemea kufunga ndoa siku ya valentine tarehe 14 Februari 2010. Raisi Bingu atafunga ndoa na waziri wake wa utalii Calist Chipola. Bingu wa Mutharika mwenye umri wa miaka 76 aliwahi kuwa na mke wa ndoa huko nyuma lakini bahati mbaya mama huyo alifariki dunia....Source: BBC News
 
Safi kabisa, hakuna kitu kizuri kama kuwa na mwenzi wa maisha. Na kama akifariki basi ni kifo kimewatenganisha na shurti apate mwenzi mwingine. Na kwa umri huo ni lazima awe na mwandani wa kumtunza. Umeamua jambo jema mzee. Heshima mbela kabisa. Hapa sipo upande wa Jacob Zuma, hata kama anadumisha mila!!! Binadamu tuwe na kiasi!!
 
Nilidhani Mkuu wa Kaya!

Ha ha ha Mkuu MM,

Huku kwetu huwa hawaweki hadharani!!! Ambaye alinivutia kwa kuweka hadharani ni marehemu mzee wetu Rashid Mfaume Kawawa na Samwel Malecela tu, na wote hawa walifiwa na wake zao. Hao wengine ni mbugani tu au majuu unasikia jamaa kaenda kuoa, kama wanadumisha mila kama Jacob Zuma, basi waweke wazi maana hakuna wa kuwazuia madam dini zao na kipato kinaruhusu. Halafu kama ni kiongozi basi angalao tujue ni mzigo gani tunao wa kuibeba familia yake.
 
Mhh! Huyu huku nasikia tayari katoa draw na Zuma. Ila ni kimya kimya, utasikia eti kaenda kufungua hoteli ya kisasa! Duuh!
 
Nilidhani Mkuu wa Kaya!
...Mkuu wetu wa kaya sijui anaogopa gharama kuwa akisema anapata jiko lingine atalazimika kutualika watu wengi kwenye mnuso... Maaana jamaa ni kimya kimya tu!!!..
 
Nilidhani Mkuu wa Kaya!

hahaaaa huyu wetu yuko ngoma droo za Zuma mbona muda tu ila anaogopa kutangaza watu watahoji sana..we unadhani kwa nini miguu yake inakosa nguvu anaanguka majukwaani??yuko very bizinesi kwenye mambo yetu yaleeee ya kitengo
 
Raisi wa Malawi Bingu wa Mutharika anategemea kufunga ndoa siku ya valentine tarehe 14 Februari 2010. Raisi Bingu atafunga ndoa na waziri wake wa utalii Calist Chipola. Bingu wa Mutharika mwenye umri wa miaka 76 aliwahi kuwa na mke wa ndoa huko nyuma lakini bahati mbaya mama huyo alifariki dunia....Source: BBC News

Mie tatizo langu ni hapo tu.., isije kuwa ni yaleyale ya kupeana uongozi kwa interest za kitandani.
 
Sasa huo uwaziri atajiuzulu au?
hapana bwana kwani vina mahusiano gani? Mbona Mhe Kaguta kampa mama uwaziri na maisha ya ndoa yanaendelea. Kila la kheri Mhe. Bingu kwenye ndoa yako ila msimamo wako uendelee vilevile kwenye kupambana na ufisadi mama hasije leta ushauri mbofumbofu
 
Back
Top Bottom