Mheshimiwa Rais, Watendaji wako na Watanzania wote tulifanye hili haraka sana...

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,571
108,922
Nianze kwa kuwapa pole sana Watani zangu wapendwa Wana Mkoa wa Kagera kwa Janga kubwa lililowapata la kutokewa na Tetemeko kubwa la Ardhi hivi majuzi. Najua fika kuwa hata Mkoa wangu wa Mara tulikumbwa na kwa majirani zetu Mkoa wa Mwanza nao liliwakumba ila halina ubishi kuwa Mkoa wa Kagera ndiyo umeathirika zaidi.

Nimekuwa nikipokea taarifa mbalimbali kutoka Mkoa wa Kagera na naomba niseme tu ukweli kwa Watanzania wenzangu Wapendwa hali ya Maisha kwa Waathirika wa tetemeko la Ardhi huko si nzuri na kama una moyo mwepesi kama Mimi ukipewa Ushuhuda utaishia tu kutokwa na machozi ya huruma kwa hawa Watanzania wenzetu.

Watu wengi sana wamepoteza mali zao na kibaya zaidi 90% ya hawa Waathirika ni Watu wenye kipato cha chini sana japo kuna Wachache ambao wana uwezo wao ila katika Janga lolote huwa hakuna cha Tajiri wala Masikini kwani kila mmoja huwa na machungu ya aina yake.

Kuna matukio mawili nimeyaona hivi punde hakika yamenitoa machozi tukio la kwanza kuna Familia moja nimeiona imewabidi walale katika mtaro mmoja kwa kujibanza ili tu kujisitiri na wakikosa msaada wowote na tukio la pili kuna familia moja ambayo nyumba yao imebomoka kila kila sehemu na wakawa kwa nje wana Nguruwe wao wako zizini hivyo kutokana na mazingira magumu na kukosa mahala pa kulala iliwabidi wawauze haraka hao nguruwe ili wapate kulala humo katika hilo Zizi ambalo urefu wake ni hatua zako mbili tu za miguu na kuna Watoto wawili wadogo sana.

Ndugu Watanzania wenzangu hawa Ndugu zetu wana Kagera wapo sasa katika Kipindi kigumu nadhani kuzidi chochote kile na wanahitaji mno maombi na misaada yetu ya hali na mali hivyo nimeona kama Mtanzania nami nije na ombi langu hili MAALUM kwa Kada kuu tatu za Kijamii.

Mheshimiwa Rais, Watendaji wako na Watanzania kwa ujumla najua fika kuwa Ofisi ya Waziri Mkuu kupitia Kitengo chake cha Maafa wana Fungu maalum la Maafa kama haya ila tuache binafsi sidhani kama kweli hiki Kitengo peke yake kitaweza kumaliza matatizo ya Wana Kagera wote na vile vile sina uhakika kama Waathirika wote watafikiwa.

Hivyo basi ili kuwasaidia hawa Ndugu zetu Wapendwa wana Kagera naomba kwa Heshima na Taadhima naomba haya yafanyike haraka bila kuchelewa:

  1. Mheshimiwa Rais endesha Harambee ambapo Wewe, Makamu wako, Waziri Mkuu wako, Mawaziri wako, Wakuu wako wa Mikoa, Wakuu wako wa Wilaya na Watendaji wako wote wa Ngazi zote wachangie Pesa za kutosha tu ambazo zitapelekwa moja kwa moja kwa Waathirika.
  2. Makampuni Binafsi yote Makubwa hapa nchini Tanzania nanyi pia mjipange kwa Umoja wenu na mchangishane Pesa za kutosha ambazo zitakusanywa na kupelekwa kwa Waathirika.
  3. Wizara ya Ardhi na Shirika la Nyumba nadhani hiki ni Kipindi chenu cha kuonyesha ni jinsi gani mnawajali Watanzania hasa katika Vipindi vigumu kama hivi. Nashauri Waziri wa Ardhi Lukuvi agiza haraka Watendaji wako wa Ardhi wa Mkoa wa Kagera watafute eneo maalum ambalo watalipima haraka na ambalo linaweza likakidhi haja ya hizo Kaya zilizoathirika na Tetemeko la Ardhi kisha kwa Mamlaka uliyonayo waambie Shirika la Nyuma ( NHC ) wakajenge nyumba za kutosha hilo eneo ambazo zikikamilika watakuja kuishi hawa Ndugu zetu waliopatwa na hili Janga.
  4. Vyama vyote vya Siasa huu nadhani sasa ni wakati murua wa kuonyesha kuwa kweli nyie mpo kwa maslahi ya Watanzania hivyo basi nanyi itisheni harambee zenu haraka na Pesa zote zipelekwe katika mfuko maalum wa kusaidia wana Kagera waliopatwa na haya madhila.
  5. Kwa sisi Watu wa kawaida na wa Mikoa yote nchini Tanzania katika kila Mkoa kuweke utaratibu maalum ambao kila Mtanzania basi aweze kuchangia tu kuanzia Shilingi 1,000/ hadi Shilingi 5,000/ ila kwa wenye uwezo zaidi wako huru kutoa zaidi ya hapo.
Na ningependekeza utaratibu huu uwe unatumika hasa yanapotokea majanga ya asili kama haya sehemu yoyote hapa Tanzania. Watanzania wenzangu tushikamane na tufanye harambee za kutosha ili tuungane na Wana Kagera hasa katika kipindi hiki kigumu chao.

Nitashukuru kama hili Ombi langu litazingatiwa na kama kuna mwenye mawazo mazuri zaidi ya haya yangu ya nini kifanyike ili tu hawa Waathirika na wao waishi maisha mazuri na waendelee kufanya Shughuli zao za kawaida.

Sote ni Watanzania na tushirikiane kuwasaidia Ndugu zetu wa Kagera walio katika kipindi kigumu kwa sasa.

Akhsanteni Watanzania wenzangu na Mwenyezi Mungu awabariki nyote.
 
serikali ya walalahoi ya Kenya imeamua kuwasadia kuwarudishia makazi lakini muhimu ya walalahoi ya Tanzania imetuma lambi lambi za mdomo mtupu
 
serikali ya walalahoi ya Kenya imeamua kuwasadia kuwarudishia makazi lakini muhimu ya walalahoi ya Tanzania imetuma lambi lambi za mdomo mtupu

Sasa " Poti " huu siyo wakati wa kuanza kulaumiana na badala yake tushirikiane tuweze kuwasaidia Ndugu zetu wa Kagera. Nakuomba sana " Poti " wangu tuache kila jambo kulihusisha tu na itikadi za Siasa. Post yako inaonyesha moja kwa moja kuwa Wewe ni Anti-Government hii iliyopo na unaonyesha ni wa upande wa pili. Kwani walioathirika kule Kagera ni Wana CCM au CHADEMA tu peke yao? Badilika " Poti " na Siasa zetu zisitufanye tukawa wa " hovyo hovyo " katika kufikiri.
 
Sasa " Poti " huu siyo wakati wa kuanza kulaumiana na badala yake tushirikiane tuweze kuwasaidia Ndugu zetu wa Kagera. Nakuomba sana " Poti " wangu tuache kila jambo kulihusisha tu na itikadi za Siasa. Post yako inaonyesha moja kwa moja kuwa Wewe ni Anti-Government hii iliyopo na unaonyesha ni wa upande wa pili. Kwani walioathirika kule Kagera ni Wana CCM au CHADEMA tu peke yao? Badilika " Poti " na Siasa zetu zisitufanye tukawa wa " hovyo hovyo " katika kufikiri.
Basi tuko pamoja ila hili lipite wakati mwingine tuzungumze tukiwa huru kuna sehemu haiko sawa
 
Back
Top Bottom