Mheshimiwa Rais tafadhari fukuza hao wanaokuandalia majina ya wateule katika nafasi mbalimbali

chilumendo

JF-Expert Member
Oct 26, 2013
2,903
3,078
Mheshimiwa raisi toka umeingia madarakani kumekuwepo mkanganyiko wa teuzi zako ambapo kuna kipindi uteuzi unapofanyika ndani ya siku chache mabadiliko yanafanyika ukianzia yule mkuu wa mkoa wa shinyanga,uje yule mkurugenzi wa NSSF, yupo yule ulimpeleka bandarini haukupita muda tukasikia umemtoa pale umemteua RAS sijui wapi? Mara sijui sijui jina la mkuu wa wilaya limekosewa.

Sasa kituko kikubwa ni leo ambapo umetoa majina ya wakurugenzi ambapo kuna majina mengine yamejitokeza sehemu mbili yaani kwa wakurugenzi na kwa Das. Sidhani mweshimiwa rais kama linajitokeza kwa bahati mbaya bali kutakuwa uzembe wa hali ya juu kwa wasaidizi wako, na bila kupepesa macho chanzo cha watumishi hewa ni hao wasaidizi wako, kama wanashindwa kuchambua majina miambili tu je litakapokuja la watumishi zaidi ya 2000 kufanya uteuzi si wataboronga zaidi.

Nakuomba mweshimiwa raisi ufanye haraka kuna siku watakuja kukuaibisha fukuza hao
 
Hizi comedy sijui zitaisha lini!!?

Bado teuzi za Tarafa, kata na vijiji. Sijui nani atawateua hawa!!
 
Mheshimiwa raisi toka umeingia madarakani kumekuwepo mkanganyiko wa teuzi zako ambapo kuna kipindi uteuzi unapofanyika ndani ya siku chache mabadiliko yanafanyika ukianzia yule mkuu wa mkoa wa shinyanga,uje yule mkurugenzi wa NSSF, yupo yule ulimpeleka bandarini haukupita muda tukasikia umemtoa pale umemteua RAS sijui wapi? Mara sijui sijui jina la mkuu wa wilaya limekosewa.

Sasa kituko kikubwa ni leo ambapo umetoa majina ya wakurugenzi ambapo kuna majina mengine yamejitokeza sehemu mbili yaani kwa wakurugenzi na kwa Das. Sidhani mweshimiwa rais kama linajitokeza kwa bahati mbaya bali kutakuwa uzembe wa hali ya juu kwa wasaidizi wako, na bila kupepesa macho chanzo cha watumishi hewa ni hao wasaidizi wako, kama wanashindwa kuchambua majina miambili tu je litakapokuja la watumishi zaidi ya 2000 kufanya uteuzi si wataboronga zaidi.

Nakuomba mweshimiwa raisi ufanye haraka kuna siku watakuja kukuaibisha fukuza hao
Utumbo
 
Mweshimiwa # Mheshimiwa all in all Ujumbe uko poa. Sugu alishasema serikali hii ni ya …......Natania tu TCRA jamani siko serious
 
Sina cha kushangaa kwenye makosa kama hayo huko serekalini, huo ni udhaifu wa kawaida kabisa huko serekalini. Rais yuko serekalini ndani ya miaka zaidi ya 20 kwa hiyo sio mgeni wa mambo hayo kwani hata yeye huenda ameshafanya makosa kama hayo mengi sana. Kwa maneno marahisi huko serekalini kufanya mambo kwa uzembe ni sehemu ya utendaji wao.
 
Mkuu wa Ikulu ni yeye je atajitumbua kwa kushidwa kusimamia taasisi anayoiongoza???? kama makosa ni yake je atajitumbua?? kumbuka majina ya mawaziri aliyaandika kwa mkono!!!? hapa atashindwa kuchapisha mwenyewe????
 
SIKUKUU ZILIVYOKUWA HAZINA KIKOMO NCHI HII IPO SIKU WATAMCHAPISHIA HOTUBA YA SIKUKUU YA NANENANE ATAISOMA KWENYE SIKUKUU YA KUPAMBANA NA WALEVI DUNIANI
 
Rais tutajie huyo anaesababisha haya madudu tujue km ni qualified au ni mmoja wa 'vijana wetu' kapachikwa kwenye position asioimudu.
 
Raisi wetu ni mjuzi, na anafanya mambo yoote mwenyewe... hao wasaidizi wake wamekaa kama sanamu tu...
 
Back
Top Bottom