Mheshimiwa Rais, pitia Mwanza uone

Bonson

Senior Member
Apr 20, 2013
183
147
Heri ya mwaka mpya Mheshimiwa.

Mwishoni mwa mwaka jana, viongozi wa Jiji la Mwanza walichukua hatua ya kuwaondoa MACHINGA wote katikati ya mji. Ni kweli viongozi wa mkoa hawakua wamefanya maandalizi ya kutosha kwa ajili ya machinga japokua nia yao ilikua nzuri na ya kimaendeleo.

Siku chache baada ya Jiji kusafishwa, Mheshimiwa ulitoa agizo la kuwarudisha MACHINGA WOTE na ukatoa ruhusa wao kufunga hata barabara ili wafanye biashara. Mmmmhhh!! Kilichotokea Mh. Rais ni kwamba Jijini la Mwanza halipitiki sasa. Machinga wanapanga bidhaa hadi barabarani Na imekuwa shida kwa wenye MAGARI, maduka (walipa kodi), Na watembea kwa miguu. Machinga wanapanga bidhaa hadi kwenye vituo vya mafuta; Mwanza sasa ni shidaaaa!!

Kwa bahati mbaya, viongozi wa Mkoa (RC, DC, OCD) hawana sauti tena. Hivyo Na wenyewe wanaangalia tuu hali itaishiaje. Mheshimiwa nakuomba uje ulete utaratibu Jijini Mwanza.

Mungu Ibariki Tanzania
 
Ni miji yote Rais amefanya iwe michafu....

Alisisitiza usafi ila yeye ndio karuhusu tena uchafu.....Machinga wanachafua miji, mitaa inaonekana michafu.....

Inasikitisha sana
 
CBD (Central Busness District) inamipango yake...Huwezi kuruhusu watu kuuza bidhaa hovyo, tena chini barabarani ....Barabara zilizojengwa kwa gharama kubwa...

Swali la kujiuliza! Je! Barabara ndio sehemu ya kupangia bidhaa ....?

Mhe! Angeacha mamla za miji na majiji zifanye shughuli zake na mipango yake....


Nenda Kigali, Namibia, Nairobi hata Bujumbura...ni miji misafi sana....Barabara zinaonekana kweli ni barabara, hakuna machinga wanapanga bidhaa chini...

Imagine, barabara zikitaka kufanyiwa usafi itakuwaje? Angali watu wametandaza bidhaa chini...? Miji yetu inanukaa....

Mhe! Acha mamlaka na watu ukiowateua wafanye kazi zao....
 
AcheniUNAFIKII....hivi watanzania kwanini tunapenda MAJUNGU sana.......kamwe hatuufahammu msimamo wetu ni nini...maana SERIKALI IKIFANYA HIVI wapuuzi fulani wanataka hivi,,,,,Hao wamachinga wakiondolewa mtakuja mtapiga kelele huu....leo wameacha mnakuja mnapiga kelele humu...HIVI MSIMAMO WETU NI NINI??????
 
AcheniUNAFIKII....hivi watanzania kwanini tunapenda MAJUNGU sana.......kamwe hatuufahammu msimamo wetu ni nini...maana SERIKALI IKIFANYA HIVI wapuuzi fulani wanataka hivi,,,,,Hao wamachinga wakiondolewa mtakuja mtapiga kelele huu....leo wameacha mnakuja mnapiga kelele humu...HIVI MSIMAMO WETU NI NINI??????
Mkuu, issue hapa sio kutotaka wamachinga wafanye kazi; bali tunaangalia swala la mipango miji. Sijui upo mkoa gani; lakini kwa sasa Mji wote wa Mwanza unaelekea kuwa soko horera; soko lisilo na utaratibu. Pia tusisahau kwamba walipa kodi ni watu wenye maduka ambayo mbele yao ndipo ambapo wamachinga wanapanga bidhaa zilezile na kwa bei bwereree!!
Tuache ushabiki wa kisiasa na tuangalie hali halisi ya mambo!! Asante.
 
Back
Top Bottom