Mheshimiwa mwanahaki mfalila amenikuna vilivyo! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mheshimiwa mwanahaki mfalila amenikuna vilivyo!

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Rutashubanyuma, Sep 25, 2010.

?

JE WAPINZANI WAKATI WAO UMEFIKA?

 1. *

  WACHUKUE NCHI LEO

  80.0%
 2. HOJA ZA KUWA WASUBIRI VILEVILE ILITUMIWA NA MKOLONI KUIZUIA TANU

  10.0%
 3. *

  CCM MAMBO BADO SAFI

  20.0%
 4. LOLOTE NA LIWE

  0 vote(s)
  0.0%
 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Sep 25, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,789
  Likes Received: 416,597
  Trophy Points: 280
  MHESHIMIWA MWANAHAKI MFALILA AMENIKUNA VILIVYO!

  (Mwanamakala Rutashubanyuma Nestory wa Arusha.)


  Kwa asilimia mia ninamuunga mkono Mheshimiwa Mwanahaki MSTAAFU Mfalila. Unapoona viongozi wa juu wa Nchi wanaanza kujitokeza hadharani na kudai upinzani ukamate Ikulu ni dhahiri CCM imepoteza uhalali wa kututawala na lililobakia ni JK naye ajitokeze hadharani na kukikana chama chake kwa masilahi ya Taifa ambalo nina uhakika analipenda kwa moyo wake wote. Hakuna mashaka kabisa CCM imekuwa mstari wa mbele wa kutoa misamaha ya kodi kwa wakubwa lakini inapokuja mnyong'e kama mwanafunzi au mgonjwa wanasewma kila mmoja abebe msalaba wake. Wenye tuhuma nzito za ufisadi JK amewakumbatia kuanzia Lowassa ambaye ni hivi majuzi ametamka hadharani hajaona kiongozi kama yeye!!!!!!!!Hata Nyerere hafui dafu kwa Lowassa!!!!! Akina Chenge "Bw. vijisenti" yumo kwenye tiketi ya Ubunge kupitia CCM. Akina Karamagi na Dr. Msabaha ni wananchi tu wamewatema lakini CCM kupitia vikao vya juu bado ilikuwa inawaona ni lulu!!!!Bw. Pesambili Mramba pamoja na kuwa na kesi ya jinai Mahakamani bado CCM inaona anafaa wakati Nyerere alituasa "Mke wa Kaisari hapaswi kutuhumiwa." Misamaha ya kodi kwa wachimba madini wakubwa kwa mwaka haipungui BILLIONI 700. Ongezeko la bilioni 30 tu linahitajika ili elimu ya juu iwe bure kabisa. Hapo bado tunabaki na bilioni 670 kila mwaka. Hizi ni takwimu ambazo zinamfanya JK aufyate mkia na wala asithubutu kutokea kwenye MDAHALO maana ndipo atamkabidhi Dr. Slaa Ikulu rasmi.

  "DR. SLAA DARES TO DREAM BUT JK DARES TO HIDE IN INFRASTRUCTURAL PROMISES...WHAT A SHAME"


  Nenda Ikulu Dr. Slaa...Nenda Ikulu Dr. Slaa ukalianzishe taifa la pilI jipya la watanzania ambalo lipo tayari kuthubutu na kujenga a "welfare society" ambayo elimu na afya zitakuwa bure kwa wananchi wote vinginevyo tutakuwa manamba ya wageni kwenye huu utandawazi ambao CCM inaamini hatuna namna ila tuwapishe wakoloni mamboleo watutawale. Tusisahau TRL, Zain, Barrick, Netgroup Solutions na wengineo kama TICKS ambao ajira zote nyeti waMEzifyeka na sisi tunaambulia uboi tu. Vilevile, kazi za kandarasi zote kubwakubwa ni wachina tu ndiyo wanaula sisi tunaambulia makombo ya wageni. Misamaha ya kodi za madini kwa wachimbaji wakumbwa ipatayo bilioni 700 kwa mwaka inatosha kutoa elimu, afya na maji bure kwa watanzania wote si mjini au vijijini. GO DR. SLAA GO...AT LEAST YOU CAN DARE TO DREAM WHILE JK CAN ONLY DARE TO BEG....DR. SLAA IS A HOMEBODY WHILE JK IS A WANDERLUST RAKING FOR MORSELS
   
Loading...