Iwachu Heza
New Member
- Aug 7, 2012
- 1
- 2
Mheshimiwa tulitegemea bajeti yako itatuokoa kwa kilio cha muda mrefu lakini ajabu umeamua kukaa kimya.Pamoja na bajeti nzuri na maoni mazuri kila mwaka lakini mwaka huu umetuangusha kutokana na mambo makuu yafuatayo;
1.Hukuongelea chochote kuhusu mwekezaji mpya ndani ya TTCL kama ulivyoahidi mwaka jana kuwa TTCL inatafutiwa mwekezaji mpya.
2.Hukuongelea chochote kuhusu ndoa isiyo na tija(uwekezaji wa Airtel aka Zain aka celtel aka msi ndani ya TTCL),kuna tetesi kuwa aliyekutangulia aliongelea ndoa hiyo na kutaka kuivunja lakini mafisadi walishinda na yeye kuondolewa kitini na kupewa wewe na tetesi zaidi zinasema hao mafisadi ndio waliozuia Airtel kuondoka ndani ya TTCL huku wakizuia hata TTCL isikopeshwe wakati inakopesheka.
3.Hukuongelea chochote kuhusu utendaji wa maofisa wakuu ndani ya TTCL,ambao ulipata kuongea na wafanyakazi wa TTCL mikoa tofauti na kusema ni kikwazo lakini umekaa kimya tuu,huku kampuni ikiendelea kusuasua.Kuna tetesi kuwa mmoja wa maofisa hao ni mwalimu wako ukiwa chuo hivyo unamlinda.
4.Wengine mnaojua zaidi ongezeni hapa ili kilio cha wanyonge kisikike.