Consigliere
Platinum Member
- Sep 9, 2010
- 12,692
- 26,584
Naam mkuu ndio maana nikashauri kama tatizo ni hakuna mafuta na baadhi ya mitambo imezimwa.., basi inabidi hata tufahamu gharama ya kuendeshea mitambo hio kwa siku hata moja tu..!! na sisi wanajamiii na wananchi tuchangishe na kuendesha hio mitambo kwa siku moja kwa kufanya hivyo tutakuwa tumeonyesha njia ya kufanya ambapo serikali itaona aibu na hata waheshimiwa wetu itabidi waone aibu kwa kula maposho wakati wananchi tunakopa ili tu, tupate mwanga hata wa siku moja
ʞontɹact Sniper;2377613 said:Wanapiga makasia kwa furaha na kasi kuelekea kule ambako maji yanaelekea,.... maskini hawajui ule unaoonekana kuwa wepesi wa makasia na kasi ya maji unatupeleka kwenye maporomoko ya maji ambako kuna mawe na miamba........
Mkuu wazo lako liko murua kabisa la at least wananchi kuchangia kwa siku moja kuendesha mitambo ile au kununua mafuta
Ila tatizo lililopo je viongozi wetu wana utashi huo wa kujua kuwa wananchi wanaangamia kwa kukosa nishati ya umeme au wanakisikia kilio cha wananchi wao waliowaweka madarakani kuhusu umeme au ni kile kilio cha samaki machozi yanaenda na maji.
Je viongozi wetu wana utashi kumaliza tatizo au ni kwamba washachukua 10% zao na wanaendeela na shughuli zao maana hawana shida ya umeme kwao?
Sniper suluhisho hapa ni nini
Tuendelee kulalamika malalamiko ambayo hayafiki kokote au tuamke na kusema sasa enough is enough hapa tulipofikia panatosha tunahitaji mabadiliko na suluhisho la hapa tulipofika
Hivi ni kweli maandamo ndio yatakayotuletea umeme....? (labda..) je kama yasipofanikiwa tutafanya nini..?, je ni kweli tutaandamana tena na tena na tena..?
Halafu kumbuka hawa jamaa ni wazee waku-spin mambo tukiandamana kudai maendeleo yetu wenyewe wanasema ni fujo ( na wapo watu wanaoamini uongo huo kwamba maandamano ni fujo)
Hivyo basi Je kweli hatuwezi kutumia njia nyingine ya attack japo kuonyesha kwamba tunapingana nao ila positively...?
Mfano mitambo yote iliyosimama kwa sababu ya kukosa mafuta wananchi kuchanga pesa na kuendesha mitambo hata kwa siku moja tu...!!! ili kuonyesha kwamba Tanzania bila giza inawezekana na viongozi wetu ni wasanii
Ni kweli mkuu hii nchi ishapotea na the all system needs to change..., sababu hali ilivyo sasa hata akija malaika kuongoza nchi..., system ni corrupt kiasi ambacho hata yeye anaweza akabadilika na kuwa corrupt.ʞontɹact Sniper;2377821 said:
Tujiulize haya kwa lengo la kujua kama kweli tupo tayari kwa mabadiliko na tuna weza kuwa ni mibadalala mizuri.
Vingenevyo tunaweza tukamtoa mgonjwa na kuweka maiti.....
Tujiulize kabla ya kufanya maamuzi
Ni kweli kabisa viongozi wetu hawajali kabisa...!! (ila kama kuna kitu wanachojali ni kuona kwamba huenda wasirudi madarakani baada ya miaka mitano ijayo)... Na viongozi hawa wamekuwa wakiwadanganya wananchi kwamba hili tatizo haliwezi kupata solution kwamba ni mvua ndio imesababisha na hili ni jambo la kawaida...
Hivyo basi wananchi hata siku moja tukionyesha kwamba hawa jamaa ni wasanii itabidi waanze kufanya kazi yao ukizingatia kwamba nafasi zao zitakuwa mashakani...
Hivyo basi ni nani wa kutuongoza zaidi ya Waziri Kivuli wa hii Wizara!!!??
<br />
<br />
Mkuu yaani bado unahimiza kuchangishana tena ...no please.Si kubaliani nawe hata kidogo,tunapaswa kuishinikiza serikali kutumia vizuri kodi wanazotunyonya kuhakikisha wanaboresha maisha yetu na si vinginevyo...tuchange!hiyo fedha tutaitoa wapi wajameni...Ebu tuamkae waTANZANIA tunaburuzwa mpaka fikra zetu bah!
ʞontɹact Sniper;2377821 said:Kelele zilizopigwa zimetosha sana, na sasa hivi zimezoeleka sana na kwa yote mpaka tulipofika, sasa hivi watanzania tunatabilika sana, ndiyo maana huoni dalili ya respond yeyote ile, I trust no Politician, iliyobaki kwa sasa tujipigania, tuna silaha za kutosha sana, nazo ni kama zifuatazo, vijana wasio na ajira, wananchi waliodhurumiwa (mambo mbalimbali) na sheria ikashindwa kuwapigania, watu wenye vinyongo, na wale ambao wanahisi mapambano haya yatawasidia, pamoja na wataalumu katika nyanja mbalimbali ambao wanauhisi uchungu huu wa watu kudhurumiwa bila ukomo.
Ni furaha yangu kama serikali yetu itabadilika na kuwa na sifa zifuatazo....yaani usikivu na uwajibikaji na kutovumilia uzembe, ufisadi wala kutokuwa na rafiki wa kudumu pale maslahi ta taifa yanapoingiliwa.
Ni sisi wenye jukumu la kuiweka madarakani serikali lakini bahati mbaya sana ni kuwa katika kutafuta fursa wenzetu wanakuwa na ajenda mbili, moja ya kuombea ridhaa, nyingine na kubwa kwa ni malengo yao binafsi.
Lakini kabla ya kutengeneza msimamo au kuchukua au kukubaliana kuchukua hatua stahiki dhidi ya serikali tujiulize kwanza ni kitu gani tumekifanya ambacho tunaweza tukatumia kama silaha na sababu ya kufanya maamuzi...Je binafsi tunawajibika ipaswavyo katika maeneo yetu? Je tu waadilifu kwa kiasi gani? Je dhamira zetu za kimapinduzi ni matokeo ya kimkumbo na kimakundi au ni dhamira za kweli na dhato toka katika mioyo yetu?
Tujiulize haya kwa lengo la kujua kama kweli tupo tayari kwa mabadiliko na tuna weza kuwa ni mibadalala mizuri.
Vingenevyo tunaweza tukamtoa mgonjwa na kuweka maiti.....
Tujiulize kabla ya kufanya maamuzi
Siku tukiacha kuwategemea wanasiasa kwa ajili ya solutions za matatizo yetu, Plan C itakuja automatically.
Until then tutaendelea kupigika
Ni kweli usemayo lakini watanzania wanahitaji mtu wa kuwa-mobilize na kuwaonyesha ni nini cha ukweli na ni nini cha uongo..., kiongozi anahitajika kuwaongoza watu hata kama akiwa mwanaharakati..., sababu sasa ni wengi wamechoka lakini hawajui ni nini cha kufanya, na haki zao wanadhani ni favor
Nasikia Baada ya Wenje kuongea Bungeni umeme umerudi mwanza na hii ni baada ya kama siku 5...!!!!!
Sasa swali ni kwamba huu umeme umetoka wapi?, au mvua ya ghafla imenyesha Mtera
Mkuu sisemi kwamba wananchi ndio tubadilike kuwa Tanesco na kuendesha Tanesco...!!! , hapana mkuu bali ni kwamba hata tukiendesha kwa siku moja hii itakuwa symbolic, au wananchi tukichanga tukaleta hata mtambo wa kuzalisha 1MW hii itakuwa symbolic kwamba kama hata sisi masikini tunaweza iweje serikali yenye kodi zetu ishindwe..!!
Sababu kama ni kuishinikiza serikali tumefanya hivyo kwa muda wa miaka kama thelasini..!! au unamaanisha kwamba hii serikali haijawahi kulazimishwa?
Mkuu ukishakuwa na uongozi ambao ni legelege kuanzia juu hata huku chini huwezi pata afadhali yoyote. Kuna uozo mkubwa sana kweney kila sekta na sababu ni kuwa hakuna uwajibikaji kuanzia ngazi za juu mpaka mfagizi wa ofisi. Ni wale wanaokuja wanasign kitabu cha mahudhurio na kwenda kwenye biashara zao na hili lipo karibu kila ofisi
Wananchi wakihamasishwa na wakiwa wanaona uwajibikaji kuanzia kwa watendaji wakubwa sidhani kama utaona kitu legelege na hili likifanyika mkuu sidhani kama kutakuwa na uzembe
Mbona Rwanda wanaweza bana sisi tuna nini tushindwe
Si umeona hapo juu pendekezo langu Gaijin.., alafu nikianza kulipigia debe hili suala nani ataendelea kulima haya majaruba ya mpunga (unajua tena classification and division of labor) (wapo watu ambao hii ndio kazi yao na posho wanakula)Mtumania cha ndugu hufa masikini. Tunaweka matumaini yetu yote kwa wanasiasa, hatuwezi kufika hata siku moja, kwa sababu tunabweteka na kusema Waziri Kivuli yupo atoe solution. Toa wewe mwananchi solution kisha mlazimishe Waziri kivuli na serikali waitekeleze.