Hivi huu mtindo wa kumtambulisha ama kumuita mtu kwa kutumia fani yake mbele ya jina lake umeanza lini? Manake siku hizi mtu ukiwa mhandisi basi utaitwa 'mhandisi' flani wa flani...ukiwa mhasibu utaitwa 'mhasibu' flani wa flani.
Labda mimi kumbukumbu yangu ni ndogo lakini hapo zamani wahandisi, wahasibu, n.k. hawakuitwa kwa fani zao. Ila sasa naona huu utaratibu umeshika kasi sana. Sijui kwa nini tu?
Kwenye suala la mtoa hoja, Woman of Substance - Member of Jamii Forums, watawala wetu wanaiga wenyewe wanachokiita "mfumo wa Jumuiya ya Madola". Kwa sababu wanapokopi na kupaste ndio wanajikuta wana matatizo kwa sababu kule kwenye House of Commons huwa wanafanya hivyo hivyo "Honorable Member of Parliament for Northfolk Norman Lamb," sasa na sisi tumechukua hivyo hivyo.
Kwenye suala la NN - hili tumeligusa hapa mara nyingi lakini limetokana na utofautishaji ambao wanaupata watu ambao ni Madaktari wawe wa tiba au utaalamu na hivyo na sisi tumeonelea kuwa ni vizuri kuwatofautisha - reasoning ikiwa - wote ni wasomi waliobobea. Kwamba kama Daktari sababu ya usomi wake anaitwa "Dr. so and so" kwanini basi Injia naye kwa sababu ya usomi wake asiitwe "so and so"?
Lakini nyuma ya hili liko kasumba ambayo unaiona kwa Wanigeria ambayo na sisi tumeiiga - wao hujikuta wanatambulisha siyo Udaktari tu bali vyeo vyote vya jadi.. so utakutana na
Dr. Chifu, (cheo kingine cha jadi) so and so..
Vinginevyo, tutajuaje wana ujiko?
WOS
Nadhani ni tatizo la lugha watu kufanya written coomucantion iwe ni spoken na sometime Spoken commucatin kama ilivyo wanaiweka kweneye maadishi.
Inawezekana kuwa sahhii gazeti kuandika hayo yote lakini sio kwenye kuongea. Au kama alivyosema mchangiaji mmoja copy ana patse nzima nzima ya kingereza bila kungalia itakaa vipi katika kisahili
nawasilisha
- Viongozi wetu kama walivyo wabunge wanahitaji commuication skills. kitu kingine utaona wengi majibu yao ni ya kuandikiwa.
- Viongozi wetu wanahitaji kujua wananchi hatuhiaji kujua matabaka , taaluma au vyeo au fani vya hao walio mjengoni.
Mtazamaji IT technician ,Jf senoir expert member
Nashukuru sana kwa mchango wako ndugu yangu ...( vyeo vyako navitambua hivyo itifaki imezingatiwa lol)
utanisamehe pale juu nilisahau kitu kimoja hope sijasahu kingine
Mtazamaji ,IT technician , (Diploma) Jf senoir expert member
mkuu..
mimi nimekutana kabisa na mtu
ambae bussiness card yake amejaza title tele
na title ya mjumbe wa halmashauri kuu ya ccm....
tunapoelekea ni kuwa watu wataanza kuitwa
mheshimiwa mmiliki wa gazeti la ijumaa,john shigongo
mheshimiwa mmiliki a coud media joseph kusaga...
na wengine itakuwa mheshimiwa diwani na mmilikiwa bar ya batotoz john robert...
very upuuzi
Halafu utambulisho huo output ni zero, loo!Hmm..okay!Kwenye nchi za wenzetu ambazo zimekomaa kisiasa na kidemokrasia, kwenye mabunge yao wabunge huwa hawajitambulishi kwa fani zao. Mfano bunge la Marekani (chemba zote mbili) limesheheni wasomi wa ukweli lakini hata siku moja sijawahi kumuona Newt Gingrich akijitambulisha kama Dr. (wa PhD) Newt Gingrich, Speaker, US House of Representatives au Dr. (surgeon) Bill Frist, Senate Majority Leader, au sijui Advocate Barack Obama, US Senator, Illinois....Sisi tunapenda sana ujiko wa kwenye makaratasi kuonyesha tumesoma. Hovyo kabisa....
TBC hapa kuna Waziri akutumia muda mrefu kweli kwenye majumuisho ya Wizara yake...
anataja waheshimiwa kibao waliochangia kwenye majadiliano, kwa majina...na kumalizia..Mheshimiwa ....."mbunge".Hii imefanya atumie muda mrefu sana wakati sisi wananchi tunachotaka ni kusikia hoja na siyo majina.
Najiulizayafuatayo:
1. Kuna ulazima gani kuwataja majina na ubunge wao?
2. Je mtu asiye mbunge angeweza kuchangia?
3. Nini mantiki ya orodha hiyo badala ya kujibu hoja?
Tuelimisheni wajuaji wa mambo.
******Niwie radhi bibie Samawati.... nakutakia kila la kher!