Mhede anafanya jambo TRA, viwango ya kodi vishushwe sasa

Masokotz

JF-Expert Member
Nov 26, 2018
3,495
5,529
Mimi ni mfuatiliaji wa masuala ya kodi hapa nchini.

Kuna mambo kadhaa ambayo naona TRA wanayafanya sasa tena kwa kasi kubwa sana. Mambo haya kwa hakika yataongeza kasi ya makusanyo ya KODI kwa asilimia 300. Katika mtazamo huo nafikiri sasa ni wakati wa Serikali kufikiria namna ya kushusha iwango vya kodi ili kuhamasisha zaidi watu kutumia mfumo huu mpya.

Baadhi ya mambo hayo ni pamoja na:

Wafanyakazi kuwa na TIN numbers, Kuwezesha E filing ya Tax returns, nafikiri pia waruhusu self-assessment etc.

Sasa nafikiri ni wakati sasa wa kuondokana na habari za EFD pekee badala yake wawawezeshe wafanya biashara kuweza kutoa receipts online katika tovuti ya TRA. Fiscal receipt bila kuwa na ulazima wa kuprint.

Mfano: Mimi ni mfanya biashara, niliyesajiliwa na TRA basi niweze tu kuingia online na kuingiza TIN number ya mteja wangu na kumtolea Risiti bila kuhitaji kuwa na printer wala EFD. Ingawa na zenyewe ziendelee kuwepo kwa aina ya biashara ambazo zinahitaji.

Tufanye ulipaji kodi uwe ni rahisi na kushusha viwango vya kodi ili kupanua wigo wa walipa kodi.
 
Hauko systematic katika uandishi wako, umechanganya mambo mengi. Seems una hoja but its presentation is a problem!
 
Hauko systematic katika uandishi wako, umechanganya mambo mengi. Seems una hoja but its presentation is a problem!
Mkuu, nimeandika kwa kifupi tujadili ila unaweza kuongezea nyama pia.

Karibu
 
Back
Top Bottom