Mhe. Zitto Kabwe: Asante Umetufungua macho!

Mhe. Zitto Kabwe: Asante Umetufungua macho!

Wanasiasa ni hatari, yaani ndo maana wakati wa uchaguzi wanamwaga rushwa kama hawana akili nzuri, pilau na wali kuwaonga wapiga kura, kumbe ni kwa maslahi binafsi.
 
Watu walafi wanaitafuna tu nchi bila kuangalia maslahi ya vizazi vya baadaye
 
Heading ya habari yako kuwa Tetesi siyo fair
 
Kwa hiyo mihela yote ya kodi wanaimaliza wao..bila hata kukatwa kodi...ama kweli siasa ni dhahabu kuliko ueledi wa fani nyingine yoyote hapa bongo.

Kwani ulikuwa hujuwi hili? Unafikiri kwanini kina Mulugo wana foji vyeti ili wapewe uwaziri? Sasa mtu kama Pinda ana umuhimu gani katika nchi hii mpaka aje kulipwa milioni 26 kwa mwezi?
 
Angalia gharama za maisha wakati Mwl analipwa $ 1,600, akili za kibavicha hizi kwani umesikia kazi ya urais ni kazi ya kueneza neno la injili au wito? Wewe ulitaka rais alipwe tsh ngapi mbona haulizi wala kushangaa mwananchi wa kawaida kama Dr Slaa analipwa tsh 12 million na hazimtoshi bado anakopa ruzuku ambayo imekususdiwa kuimarisha vyama Tanzania.Tumia kichwa kufikiri kijana

Mkuu heshima yako. Naombe utuwekee na uwiano kati ya kima cha chini enzi za Nyerere na leo kwa J.K. Ndo tutajua nani mlafi.
 
Mchanganuo tu? Mbona dogo hilo. Haya. Mchanganuo huu hapa:

Wakati Dola moja ya Kimarekani ilipokuwa sawa na Shilingi 2/25, Julius Kambarage Nyerere alikuwa analipwa Mshahara wa Tsh. 4,000/- kwa mwezi. Kwa hiyo ni sahihi kuwa Nyerere alikuwa analipwa Dola Za Kimarekani $1,600 kwa kazi ya urais kwa mwezi.

Angalizo ni kwamba Mshahara wa Rais Mwadilifu ulikuwa Dola 1,600 kwa mwezi.

Wakati Dola ya Kimarekani ni sawa na Shilingi 1,600/-, Jakaya Mrisho Kikwete analipwa Tsh. 30,000,000/- (kama taarifa zilizopo ni sahihi), Ina maana Kikwete analipwa Dola za Kimarekani $18,750 kwa mwezi kwa kazi ya urais.

Angalizo ni kwamba Rais mlafi sana analipwa $18,750 kwa mwezi. Kima cha chini kwa mfanyakazi wa kawaida ni chini ya $300. Hesabu za uwiano zinafundishwa darasa la sita na la saba kwenye shule zote za msingi Tanzania.

$1,600 kwa $18,750 kwa mwezi mmoja imekaaje hiyo. kwa kazi ya kusafirisafiri, kuhuzuria vikao hapa na pale, na kuongoza baraza la mawaziri. We unamwona rais mwenye mapenzi mema na wananchi wake hapo? Chakula anapewa bure pale Ikulu, Safari analipiwa bure na Ikulu, MATIBABU NI BURE, kinyozi wake analipwa na Ikulu, hana gharama za mafuta, upenyo wa kutumia hela hizo kuhonga vibinti hana kwa sabu anachungwa sana hapati muda kuwaona Kempinski.

Hivi rais mlafi huwa unakuwaje? That is kama taarifa za huyo Mbunge ni sahihi....

Ahsante.. Ahsante..
 
WanaJF, kama kweli anayosema Mhe. Zito ni ukweli kuwa mshahara wa Rais Kikwete ni zaidi ya sh 30,000,000/= kwa mwezi na Mhe. Pinda ni zaidi ya sh. 26,000,000/= kwa mwezi na bila shaka Mawaziri nao wapo kwenye sh. 20,000,000/= kwa mwezi kila mmoja.

Nasema Mhe. Zito asante umetufungua macho! Kisha watu tunajiuliza kwa nini Watanzania wengi tu masikini? Kama ni kweli, basi hakika viongozi wetu hawatendei haki Taifa hili masikini sana Duniani. Watanzania tuamke!!!!

Ina maana Mshahara wa Raisi upo chini zaidi ya Mkurugenzi wa TANROAD?? Mmmmmh Siamini hii kitu na kama ni hivyo ndio maana Safari za Nje haziishi
 
Angalia gharama za maisha wakati Mwl analipwa $ 1,600, akili za kibavicha hizi kwani umesikia kazi ya urais ni kazi ya kueneza neno la injili au wito? Wewe ulitaka rais alipwe tsh ngapi mbona haulizi wala kushangaa mwananchi wa kawaida kama Dr Slaa analipwa tsh 12 million na hazimtoshi bado anakopa ruzuku ambayo imekususdiwa kuimarisha vyama Tanzania.Tumia kichwa kufikiri kijana

Haka KA Zitto KENYEWE KANAFIKI TU , MBONA HAKATAJI MSHAHARA WA MBOWE ? NA DR.SLAA? KAMA DR. ANANYAKUA HELA ZOTE HIZO NA BADO KAJIKOPESHA M140.. SI HATARI HIYO?
 
Last edited by a moderator:
sijui nani alinimezesha sumu kuna mtu alinidanganya raisi analipwa m8:
 
sijui nani alinimezesha sumu kuna mtu alinidanganya raisi analipwa m8:
Ninarudia, kama ni kweli Mhe. Rais na Waziri Mkuu wanalipwa hayo mamilioni ya walipa kodi bila haya na wanaona ni haki yao, hakika Mwenyezi Mungu atawalipa hapa hapa Duniani. Ni Roho ngapi za Watanzania wanateseka kwa sababu ya umasikini????? Mhe. J.K, hivi yanayosemwa ni kweli?
 
mungu tunamuongozea majukumu ambayo mengine sisi tunaweza kuyamudu sasa mshara wa raisi na mungu wapi na wapi lipo ndani uwezo wetu hili tukiamua upunguzwe inawezekana
 
Ninarudia, kama ni kweli Mhe. Rais na Waziri Mkuu wanalipwa hayo mamilioni ya walipa kodi bila haya na wanaona ni haki yao, hakika Mwenyezi Mungu atawalipa hapa hapa Duniani. Ni Roho ngapi za Watanzania wanateseka kwa sababu ya umasikini????? Mhe. J.K, hivi yanayosemwa ni kweli?

mkapa yeye alikua analipwa sh ngapi????
 
Hivi mkapa mshahara wake ulikua ni sh ngap???

Je mshahara wa rais hua unapangwa na rais mwenyewe ndie anaejiamulia au ni nani anaehusika na kupanga kima cha mshahara wa rais?
 
WanaJF, kama kweli anayosema Mhe. Zito ni ukweli kuwa mshahara wa Rais Kikwete ni zaidi ya sh 30,000,000/= kwa mwezi na Mhe. Pinda ni zaidi ya sh. 26,000,000/= kwa mwezi na bila shaka Mawaziri nao wapo kwenye sh. 20,000,000/= kwa mwezi kila mmoja.

Nasema Mhe. Zito asante umetufungua macho! Kisha watu tunajiuliza kwa nini Watanzania wengi tu masikini? Kama ni kweli, basi hakika viongozi wetu hawatendei haki Taifa hili masikini sana Duniani. Watanzania tuamke!!!!

Mkuu haya ni yakweli.ndio maana mpaka sasa si Pinda wala ikulu iliyokanusha zaidi ya kuwatumia Tughe kumtishia zitto.hasara sana kuwa na viongozi wa namna hii.
 
WanaJF, kama kweli anayosema Mhe. Zito ni ukweli kuwa mshahara wa Rais Kikwete ni zaidi ya sh 30,000,000/= kwa mwezi na Mhe. Pinda ni zaidi ya sh. 26,000,000/= kwa mwezi na bila shaka Mawaziri nao wapo kwenye sh. 20,000,000/= kwa mwezi kila mmoja.

Nasema Mhe. Zito asante umetufungua macho! Kisha watu tunajiuliza kwa nini Watanzania wengi tu masikini? Kama ni kweli, basi hakika viongozi wetu hawatendei haki Taifa hili masikini sana Duniani. Watanzania tuamke!!!!

Hapo hujaumia zaidi bila kuambiwa kwamba mishahara hiyo ya Rais naWaziri Mkuu pamoja na Wabunge wao HAIKATWI KODI. Yaani hawalipi kodi. Kutokulipa kodi kwa hawa wakuu kuna maanisha kwamba ni wananchi pekee ndiyo wanaojenga nchi yao, hawa wasiolipa kodi wanaibomoa. Tusidanganyane kwamba eti kutokana na majukumu yao hawastahili kulipa kodi au kwa sababu yoyote ile. Kule Marekani ambako kila jambo tunajaribu kuiga, viongozi wetu hawataki kuiga kwa Rais wetu kulipa kodi kama Obama anavyolipa.
 
Back
Top Bottom