Kamanda
Mara kwetu, Tafadhari kwa heshima na taadhima na kwa niaba ya wapenda mabadiliko wote wa Jimbo la Serengeti Mara, tunamwomba Mhe.Vincent Nyerere kwa kuwa ndiye Mlezi wa Jimbo letu la Serengeti tunamhitaji afanye ziara huku Jimboni kwetu hususani maeneo ya Vijijini ambako ndiko kuna wapigakura wengi wanaotuunga mkono.
Mfano Wananchi wa Kata za Nyansurura, Kisaka, Machochwe, Rung'abure, Kebancha, Nyamoko, Kitunguruma, Kisangura na baadhi ya maeneo ya Vijiji vilivyoko kandokando ya Hifadhi ya Serengeti kama vile Merenga n.k, Wananchi wa maeneo hayo wanamhitaji Mhe.Vicent wakiamini kabisa kwamba yeye ndiye anayeweza kuwafikishia Kilio chao kwa viongozi wa juu, tofauti na Mbunge wa sasa wa CCM ambaye Serikali ya Chama chake imebariki zoezi la Operation tokomeza iliyowaua ndugu zao bila hatia, huku ikiwafukuza kwenye ardhi yao ya tangu enzi za mababu zao mpaka leo ili kuwapisha wanyama wa porini.
Kwa tafsiri nyingine ni kwamba, Mbunge huyu wa Jimbo hili Stephen Kebwe, yeye na Chama chake wameamua kwa upamoja wao, kuwathamini wanyama wa porini wapate mahali pa kuishi kuliko wananchi ambao ndio wapigakura waliompa huyu Kebwe nafasi ya kuwa Mwakilishi wao, lakini amewasaliti na kupotea kabisa Jimboni, na amekwenda kuishi Dar Es Salaam, hivyo anatarajiwa kurudi tena nyakati za Uchaguzi mwaka kesho.
Mhe.Vicent Nyerere,
Kwa kuwa Wana-Serengeti wameonyesha Moyo wa hali ya juu wa kutuunga Mkono, ni wakati mwafaka sasa wa sisi kama Chama kuwa karibu nao ili kuwasikiliza kero zao ana kwa ana, ni muda mrefu sana Wakazi wa maeneo tajwa hapo juu wamekuomba uwafikie kwenye maeneo yao.
Hivyo tunaomba uitikie wito wao sasa na uweze kuwafikia Wakazi wa Serengeti ndani ya Ratiba ya ziara zako.
Naamini wananchi hawa watapata faraja sana ya kufikiwa na Mbunge wa Chama chao wanachokiunga mkono, tena Mbunge ambaye ni mmoja ya wana-ukoo wa Baba wa Taifa Mwl.Nyerere.
Ahsante sana, ni matumaini yetu Viongozi na Wanachama wa Chadema Serengeti kuwa, mara upatapo ujumbe huu utaufikiria namna ya kuitikia wito wa wapigakura wetu.
Na;
Katibu Mwenezi Chadema,
Kata ya Nyansurura,
Francis Garatwa,
Mugumu, Serengeti,
0767881009/0785881009.
06/07/2014.